Hivi ndivyo ilivyokuwa

Hivi ndivyo ilivyokuwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
"Nashukuru nimemwona Abdul Sykes vizuri katika picha hizi.

Sikubahatika kumuona akiwa hai alikuwa na ukaribu sana na baba yetu mdogo Mzee Mrisho kuliko ndugu zake.

Wao walizoeana sana kila wakati yuko kwa Mama Sakina, Bi. Chiku bint Said Kisusa na Mzee Mrisho akiwa pale Lumumba/Mchikichi kabla hajahamia Narungombe/Sikukuu.

Sala ya alfajri wakisali wote Kitumbini.

Bwana Abdul akimpitia mzee Mrisho Lumumba.

Wakati huo huo Sharrif Juneid akikaa hapo hapo kwa Mama Sakina.

Hii ndio nyumba yake kwanza Dar-es-Salaam kuishi Shariff Juneid akikaa hapo na Shariff Abdallah Attas aliyekuwa mume wa Mama Sakina."

Hizo picha nimemtumia msomaji wangu mmoja na yeye akaniandikia hayo maneno hapo juu.

Huyu Shariff Attas alikuwa akifanya kazi kama mkusanyaji wa ushuru wa nafaka Kariakoo Market Abdul Sykes akiwa ndiye Market Master.

Kazi hii Abdul Sykes aliichukua kutoka kwa Mwingereza Brian Hodges.

Picha ya kwanza kulia ni Mzee Mrisho.

Picha ya mwisho kulia ni Mama Sakina (Bi. Chiku bint Said Kisusa), Bi. Titi Mohamed, Julius Nyerere na kushoto wa kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee.

Wako Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO February, 1955.

1619726221225.png


1619726443923.png






 
Hivi weye Mzee weye!! Una maatizo gani huko up stairs???

Tulikusahau umerudi tena!! Na yale yaleee!! ya watu waliokufa zamani.eti wanamsindikiza julius!!

Aache kusindikizwa kwao Musoma mumsindikize nyie?? km nani kwanza?
Bibi yupo hapo karibu kweli?

Hapana wewe iko shida mahala unatakiwa upewe ushauri nasaha?? Au unalilia teuzi?? Hazipo....
 
Back
Top Bottom