Hivi ndivyo milima ya Congo DRC inavyoonekana ukiwa hapa Kigoma Tanzania

Kigoma Region Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
230
Reaction score
611
Bado unayo nafasi ya kuitazama milima ya Congo DRC ukiwa hapa Kigoma, mlima tambalale uliyonyooka kwa mapana uliopakwa rangi ya blue ni nchi ya Zaire, utafika katika nchi hiyo kwa usafiri wa Boti, ni rahisi sana kutokea hapa kwetu Kigoma.



Hapa ni Kigoma Karibu na Station Milima ya Blue inayoonekana ni milima ya Congo DRC.



Muonekano wa milima ya Congo DRC kutokea fukwe za Hiltop Hotel Kigoma



Muonekano wa milima ya Congo DRC kutokea fukwe za Hiltop Hotel



Hali ya Kigoma inakuruhusu kuona milima ya Congo DRC vizuri kutokea Kigoma. Picha ya saa tano asubuhi kutokea Mlole Minzambarauni Kigoma. Mlima mrefu wa blue ndio Congo DRC



Hapa ni Kigoma-Town - Lake Tanganyika Hotel, kwa mbali kuna mlima umeambaa kukaribia usawa wa hili hema nyeupe. Mlima huo ni eneo linaitwa Kabanga, Kivu ya Kusini nchini DRC. Kutokea hapa hadi kivu ya kusini ni takriban KM 58. Sawa na kutokea Dar es salaam hadi Visiga (Mlandizi).



Picha hii ya mwisho imepigwa katika Mji wa bandari wa Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye Ziwa Tanganyika.

Kwa mbali.. ng'ambo ya maji ni Milima ya hifadhi ya Taifa ya Mahale mkoani Kigoma nchini Tanzania.

 
Haya upesi sana kalipe Tangazo JamiiForums la kuzitangaza Hoteli Mbili za Hilltop na Lake Tanganyika ambazo umetumia Mbinu ya Akili Kubwa Kuzitangaza.
 
Kongo yenyewe wamejaa wakata uno
Tu ndomana pk anawanyoosha

Ova
 
Mwalimu JK Nyerere alifanya kazi kubwa sana ukiangalia kuanzia Tunduma mpaka huko Kigoma tuna eneo kubwa sana lenye rasilimali za kutosha ni vile wazee wa Kazi macho yao yapo kwenye Viete hawafikirii kutengeneza ajira kwa vijana kupitia ardhi yetu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…