Hivi ndivyo nilivyopata mafanikio na kujikwamua kutoka kwenye umasikini

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,208
Reaction score
2,767
Ni wachache sana wanaoweza kutoa siri zao jinsi walivyoweza kupata mafanikio. Maisha ya siku hizi unatakiwa uwe kama mwanajeshi ambaye yuko vitani, kwa hiyo umakini, nidhamu, mikakati, uvumilivu, maamuzi na kujituma ndio siri pekee ya ushindi. Kwa kuzingatia hayo hapo juu, hizi ndio binu nilizozifanya mimi nakuweza kufanikiwa.

Kilimo ndio chanzo kikuu na kimechukua asilimia kama 60% juu ya mafanikio. Baada ya mwaka mmoja kulima mpunga na dengu na kufanikiwa kununua kiwanja maeneneo ya sokoni(gulioni) kijijini, kiwanja ambacho kilinishawishi nijenge fremu yenye vyumba vitano wakati sikuwa na hela ya kutosha kujenga (ilikuwepo ila ni chache).

Nikaamua kutoweka nyumbani na kuenda Dar es salaam kutafuta vibarua (ni jambo zuri sana unapotafuta hela ili ukakamilishe jambo fulani) kweli nilifanikiwa kiasi cha kujenga nyumba yote na kubakiza milango tu.

Masika yalipofika nikarundi nyumbani ili kuendelea na shughuli zangu za kilimo. Mwaka ule haukuwa mzuri sana kwenye upande wa mavuno, lakini hata hivyo nilifanikiwa kumalizia ujenzi wangu (lakini asikuambie mtu ujenzi uko kwenye milango nilipoteza hela nyingi sana kupita sehemu zote za ujenzi).

Baada ya kumaliza kujenga moyo wangu ndio ulitulia, na nikaamua kuuza ng'ombe zangu nne ambazo nazo nilizipata kupitia kilimo, na kuniwezesha kupata hela ya kununua cherehani vya ushonaji nguo saba, nikaaliri watu kwa maelewano ya kwamba kila cherehani itanipa kwa siku tsh 2000, kwa hiyo kwa ujumla katika mwezi nikawa napata tsh420,000 baada ya miezi mitatu nikaogeza cherehani saba tena, mwezi unaofuati nikanunua cherehani ya kudarizi.

Piga hesabu mwenyewe!

Nikaamua kuongeza wigo katika biashara zingine kwa mda wa mwaka mmoja kwa kuleta bidhaa katika vyumba vingine vya fremu. Kwa sasa biashara kila siku inaendelea.

Mwenye swali atauliza.
 
je kwa sasa kipato chako ni shilingi ngapi kwa mwezi?
 
Unaweza kunigawia mtaji na mimi nianze kama wewe??
 
je kwa sasa kipato chako ni shilingi ngapi kwa mwezi?

Kipato kwa sasa kusema ukweli ni kikubwa maana biashara ya ushonaji nguo imechukua vyumba viwili, kumbuka fremu ina ukubwa wa 36ft urefu na 8ft upana. kwenye vyumba hivi kwa sasa nafata vitambaa dar es salaam kwa ajili ya ushonaji. pamoja na malumbota za nguo za mitumba

(usafiri wangu ni treni)

chumba kingine, namiliki biashara ya mpesa, bidhaa vyu matumi ya nyumba nauza kwa ujumla na rejareja.

kwa maeneo yetu biashara ya tubaku na ugolo inauzika sana nimeajili babu moja anayefanya hiyo biashara kwa siku anaigiza faida ya tsh8000 hapo haipungui labda kuogezeka,

pia nauza vifaa vya baiskeli pamoja na vifaa ya jembe la kukokotwa na ngombe. na hapo nakula faida kwa siku haipugui 10000,

So unaweza ukapiga mahesabu mwenyew utapata jibu.
 
Shy land msaidie Khantwe hapo juu!!

Swali langu kwako ni, katika harakati za kulima ulikutana na changamoto gani kuanzia uandaaji wa shamba mpaka kuuza bidhaa??
 
Last edited by a moderator:
Cherehani zipo mjini au kijijini?

Mkuu siyo mjini ni kijijini lakn ni sehemu ya senta kubwa sana maeneo yale. kwa dar es salam naweza kuifananisha na kigamboni pale feri japo haiwezi kuligana kwa 100%
 

Safi kaka
 
Shy land msaidie Khantwe hapo juu!!

Swali langu kwako ni, katika harakati za kulima ulikutana na changamoto gani kuanzia uandaaji wa shamba mpaka kuuza bidhaa??

Changamoto kweli ni kubwa na nyigi pia maana hata hivyo sikutegemea sana kilimo kwa 100%, nishawahi kulimi mwaka mmoja ndegu nakumbuka zilikubwa na mafuriko,

lakn miaka ambayo nilipata mavuno nilijitahidi kuyahifadhi kwa kusubiri bei. ikubukwe sikuwa na majukumu ya kifamilia vile vile nilikuwanga na tabia kila nikamilaza kuvuna naenda dar es salaam kutafuta vibarua, nishawahi, kubeba zenge, kulima maeneo ya kimbiji, dege n.k pia nishawahi kusafiri na meli kwenda moroco tukipeleka ng'ombe yote hayo nikutafuta hela na kuacha kutegemea mavuno kwa 100%
 
Last edited by a moderator:

, kama uko dar es salaam naomba tukutane jumapili nitakuwa nimekuja huko kwa ajili ya kufuata mzingo pale kariakoo.

Najua wewe ndio utakuwa wa kwanza kuja kuwathibitishia wana jf, kama ni maigizo au nini??
 
Aisee sasa urefu wa kamba yangu si umefika hadi kwako??

ni kwa nini mme wako Ntuzu asiniambie hizo habari? lakn wewe ndio uniambie, inaonesha unakutesa sana hata hela ya matumizi hakupi ndio maana shemeji yako Shy land unamwagukia kwenye miguu ili ukupe chochote ili uweze kujikwamua.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…