Shy land
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 6,208
- 2,767
Ni wachache sana wanaoweza kutoa siri zao jinsi walivyoweza kupata mafanikio. Maisha ya siku hizi unatakiwa uwe kama mwanajeshi ambaye yuko vitani, kwa hiyo umakini, nidhamu, mikakati, uvumilivu, maamuzi na kujituma ndio siri pekee ya ushindi. Kwa kuzingatia hayo hapo juu, hizi ndio binu nilizozifanya mimi nakuweza kufanikiwa.
Kilimo ndio chanzo kikuu na kimechukua asilimia kama 60% juu ya mafanikio. Baada ya mwaka mmoja kulima mpunga na dengu na kufanikiwa kununua kiwanja maeneneo ya sokoni(gulioni) kijijini, kiwanja ambacho kilinishawishi nijenge fremu yenye vyumba vitano wakati sikuwa na hela ya kutosha kujenga (ilikuwepo ila ni chache).
Nikaamua kutoweka nyumbani na kuenda Dar es salaam kutafuta vibarua (ni jambo zuri sana unapotafuta hela ili ukakamilishe jambo fulani) kweli nilifanikiwa kiasi cha kujenga nyumba yote na kubakiza milango tu.
Masika yalipofika nikarundi nyumbani ili kuendelea na shughuli zangu za kilimo. Mwaka ule haukuwa mzuri sana kwenye upande wa mavuno, lakini hata hivyo nilifanikiwa kumalizia ujenzi wangu (lakini asikuambie mtu ujenzi uko kwenye milango nilipoteza hela nyingi sana kupita sehemu zote za ujenzi).
Baada ya kumaliza kujenga moyo wangu ndio ulitulia, na nikaamua kuuza ng'ombe zangu nne ambazo nazo nilizipata kupitia kilimo, na kuniwezesha kupata hela ya kununua cherehani vya ushonaji nguo saba, nikaaliri watu kwa maelewano ya kwamba kila cherehani itanipa kwa siku tsh 2000, kwa hiyo kwa ujumla katika mwezi nikawa napata tsh420,000 baada ya miezi mitatu nikaogeza cherehani saba tena, mwezi unaofuati nikanunua cherehani ya kudarizi.
Piga hesabu mwenyewe!
Nikaamua kuongeza wigo katika biashara zingine kwa mda wa mwaka mmoja kwa kuleta bidhaa katika vyumba vingine vya fremu. Kwa sasa biashara kila siku inaendelea.
Mwenye swali atauliza.