Hivi ndivyo Rais Samia anavyozungumziwa kimataifa, "Hassan bans all political rallies"

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Hivi ndivyo Samia anavyozungumziwa kimataifa.

Kwa kweli watu wanaomuunga mkono huyu muuaji siwaelewi kabisa.

==============
Serikali imepiga marufuku mikutano yote ya kisiasa, jambo ambalo limepingwa na wanaharakati na upinzani (Chadema) kama "ukandamizaji unaoongezeka" na jambo ambalo ni "kinyume cha katiba".

Sababu za Serikali: Serikali imetoa sababu za usalama, ikidai kupata watu wenye silaha na petroli waliohusika kupanga matendo ya uhalifu kuelekea maandamano ya Julai 7.

Vifo na Kupotea kwa Watu: Ripoti ya tume iliyoteuliwa na serikali ilieleza kuwa watu 518 walikufa kutokana na vurugu za uchaguzi uliopita, huku watu 558 wakiwa bado hawajulikani walipo (missing). Hata hivyo, wapinzani na wanadiplomasia wa Magharibi wanakadiria idadi ya vifo kuwa kati ya 1,000 na 2,000.

Mabadiliko ya Rais Samia:kuwa hatua hii ni "kurudi nyuma kwa mageuzi" (reversal of reforms) kwa sababu Rais Samia awali alikuwa ameziondoa kizuizi hicho kilichowekwa na mtangulizi wake, John Magufuli.
  • Maonyesho ya Biashara (Sabasaba): Serikali pia ilihofia kuwa maandamano yangeingiliana na Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, jambo ambalo lingevuruga jitihada za kukuza biashara na wawekezaji wa kimataifa


View: https://youtu.be/dNkjvVADoKw?is=JNvNImuu9c_kIIzU
 
Kichwa cha habari kabla hakijahaririwa na mods hakikusema β€˜Rais’.

Samia siyo Rais kwa sababu hakuna uchaguzi halali uliofanyika na yeye kuchaguliwa kuwa Rais.

Huo ndo ukweli wenyewe.
 
athari za maamuzi ya hovyo ya kususia uchaguzi zitautafuna moyo wako vizuri mno gentleman,

na ndio kwanza hata mwaka moja haujaisha. Chuki binafsi nonsense zitakuzeesha haraka sana.

ni mwendo wa kila kitu kibaya, kila mtu mwenye maoni tofauti na yako ni mbaya mpaka 2030🀣
 
Ipo siku watanzania watamkumbuka rais hassan
Hasa vijana
Uko sahihi kabisa mkuu, vijana wanywa gongo,au vijana waliopoteza marafiki zao kutokana na mauaji ya Samia,pengine labda vijana waliopoteza wazazi wao kutokana na utekaji wa Samia hawa lazima wamkumbuke huyu mtesi wetu watanganyika
 
Fvck CCM
 
Kuna clip nilisikia akihutubia leo, nikajisemea moyoni "Her excellence is addressing the nation"! Nilisikitoka sana, kwa sababu alichoongea Mungu atusamehe tu watanzania kwa kuwa mbumbumbu.
 

Ujinga tu huo. Sasa ambao hawakusudia mbona nao walienguliwa....!!?
 
Nyie wote wapumbavu tu na hao mabwana zenu wanaotuzungumza vibaya huko nje,Sijui ndiyo nyumani Kwenu huko !. Tanzania hairudi nyuma.Na jaribuni tena muone na hayo mataahira yenu mawili yatwapeleka pabaya.
Wananchi wata deal na nyinyi moja kwa moja this time. Polisi kazi yao itakuwa ndogo sana.
 
Ujinga tu huo. Sasa ambao hawakusudia mbona nao walienguliwa....!!?
Gentleman,
Tanzania haina uhaba wa wanasiasa, viongozi wala wapiga kura.

ukisusa kwa hiyari yako,
wengine wanaendelea mbele kwa mujibu wa Katiba bila mbambamba yoyote. Na huna haja ya kuweweseka na kuendekeza chuki kwa ambao wanasonga mbele πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…