Hivi ndivyo rais wa kwanza wa Zanzibar Mh. Abeid Karume alivyouawa

Hivi ndivyo rais wa kwanza wa Zanzibar Mh. Abeid Karume alivyouawa

Cc: Mohammed said

Njoo huku mwangalie nduguyo akidhalilisha fani ya uandishi.
 
Umejuaje kama aliwaona wanajeshi kwa mbaaaali..... hahahah dah!!
pengine kabla ya pyuu pyuu alisema hao wanajeshi wanaenda wapi wenzake wakajibu wako wapi, fumba na kufumbua risasi hizooo
 
Brother nahic ulikuwa na haraka ya kumaliza tu ila haiwezi kushibisha watu ambao tunasoma,, unaweza ukaijaza taarifa hata kwa vipengele,, unaweza niambia kuwa ilikuwaje akauliwa na wanajeshi aliowaona wanakuja,, je hakuwa na ulinzi alafu upepo alikuwa anapungia wapi,,nini kilifanya apigwe risasi umefupisha sana mkuu jikaze kuandika taarifa itufikie vyema wasomaji.

asutulishe tango pori kwa kusimamia sehemu moja tuu ili uwafurahishe waleee,andika uzi huu bila uoga
 
Ulikua na story nzuri ila umeiwakilisha kama tupo kwenye kijiwe cha kahawa! Mfano; unasema Karume aliona wanajeshi wanakuja du? We umejuaje kama aliona wakati karume ameshakufa? Je kabla ya kufa alihojiwa ndio akasema aliwaona wanakuja? Yan umeeleza kama vile Karume alikua mtu wa kawaida, tulitegemea utueleze kwa kirefu.
Siku nyingine ukiwa na story nzuri ujipange, sio nunaandika kama mtoto wa darasa la 2B
 
HISTORIA YA ABEID AMANI KARUME.

Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa
Rais wa kwanza wa Zanzibar . Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi .
Karume aliongoza nchi baada ya
mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964 .
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere . Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania , Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.




KUIPINDUA SERIKALI YA SULTANI MPAKA KUWA RAIS.


Usultani wa Zanzibar ulikuwa umepewa na Uingerezauhuru wake mwaka 1963 . Kabla ya hapo, Waarabu walikuwa wamefaulu kudumisha katika mfululizo wa chaguziutawala waliokuwa nao tangu zamani za Zanzibar kuwa chini ya Usultani wa Omani.
Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP), kilichowakilisha hasa Waafrika, kilipoona kwamba bungeni kina viti vichache ingawa kilipata 54% za kura katika uchaguzi wa Julai 1963 , kilipatana na chama cha mrengo wa kushoto Umma Party .
Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP John Okello (1937 - 1971 ?) kutoka Uganda aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa
kisiwa kikuu cha Unguja kushinda polisi wa nchi na kuteka silaha zao. Halafu walielekea Zanzibar Town walipompindua Sultani Jamshid bin Abdullah na serikali yake. Waliokufa katika mapigano wamekadiriwa kuwa 80 hivi tu.
Kumbe yalifuata kwa siku kadhaa (labda hadi tarehe 20 Januari )
maangamizi ya kimbari dhidi ya Waarabu (waliokuwa 50,000 hivi) na
Waasia wa Asia Kusini (waliokuwa 20,000 hivi); hakuna hakika kuhusu
idadi ya waliouawa: makadirio yanataja kuanzia mamia kadhaa hadi 20,000.
Kiongozi wa ASP Abeid Karume, asiyekuwa na msimamo mkali akawa
rais wa kwanza wa nchi, na wanachama wa Umma party walipewa nafasi serikalini. Kufikia Machi Okello alikuwa ameshawekwa pembeni na kufikia Aprili kikosi chake kimeshanyang'anywa silaha.
Mwelekeo wa Kikomunisti wa baadhi katika serikali mpya uliogopesha nchi za Magharibi . Kwa kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya athari ya Uingereza, serikali yake iliandaa mipango kadhaa. Hata hivyo, hofu ya kuundwa serikali ya Kikomunisti haikutimia kamwe, na kwa kuwa wananchi wa Uingereza na
Marekani waliweza kuhama bila shida, mipango hiyo haikutekelezwa.
Wakati huo nchi za Kikomunisti za
China , Ujerumani Mashariki na Umoja wa Kisovyeti zilianzisha mahusiano ya kirafiki na serikali mpya ya Zanzibar kwa kuitambua rasmi na kwa kutuma washauri.
Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa
Tanzania ; vyombo vya habari vilitafsiri muungano huo kuwa juhudi za kuzuia Ukomunisti kugeuza Zanzibar.
Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama
sikukuu ya taifa zima la Tanzania.

KUUAWA KWAKE.


Mnamo tarehe 7 April 1972 akiwa kibaraza cha ikulu akipunga upepo aliona wanajeshi kwa mbali wakija ikulu ambao walimpiga risasi kadhaa ambazo zilipelekea kifo chake.



Mungu Ibariki Tanzania.


Mungu Ibariki Africa.
Hakuna unachokijua kuhusu mapinduzi wala kifo cha karume you better shut up! instead of visualising the nudity of your brain!
 
Umenipotezea nyege zangu za kusoma "shwaini''
 
Brother nahic ulikuwa na haraka ya kumaliza tu ila haiwezi kushibisha watu ambao tunasoma,, unaweza ukaijaza taarifa hata kwa vipengele,, unaweza niambia kuwa ilikuwaje akauliwa na wanajeshi aliowaona wanakuja,, je hakuwa na ulinzi alafu upepo alikuwa anapungia wapi,,nini kilifanya apigwe risasi umefupisha sana mkuu jikaze kuandika taarifa itufikie vyema wasomaji.

Mtoa uzi amezingua...angesoma historia na kujiridhisha kwa utafiti....Hayati Karume hakuuawa akiwa ikulu. Aliuawa wakati akicheza bao na Sheikh Thabit Kombo akiwa makao makuu wa ASP Kisiwandui, na Sheikh Kombo kujeruhiwa vibaya na shambulio hilo la mwanajeshi.
 
Next time usome zaidi historia ya Zanzibar wakati wa Karume ni hayo tu.
 
Kiufupi yale ya 1964 yalikuwa ni mavamizi ya majeshi ya tanganyika kuivamia zanzibar, na kifo chake huyo karume kimetokana na kupinga ukoloni wa tanganyika zidi ya zanzibar na Mr X ndie mratibu wa mauaji ya rais karume.
 
Kiufupi yale ya 1964 yalikuwa ni mavamizi ya majeshi ya tanganyika kuivamia zanzibar, na kifo chake huyo karume kimetokana na kupinga ukoloni wa tanganyika zidi ya zanzibar na Mr X ndie mratibu wa mauaji ya rais karume.
 
Kuwa mwana historia sio Sawa na kuuza karanga ( njugumawe) Lakin si hilotuu, kupotoshahistoria ni kosakubwa, kubwa hata kuliko ubakaji. Mi nashauri huyu mtu aliyeandika hii Habari ya Karume atafutwe alambwe viboko hamsa matakoni.
 
Hivi ndivyo alijibu swali la darasa la saba lililouliza "Elezea unavyoyafahamu mapinduzi ya Zanzibar"
 
Back
Top Bottom