Hivi ndivyo Simba na Yanga zinavyodumaza soka la Tanzania

Hivi ndivyo Simba na Yanga zinavyodumaza soka la Tanzania

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Hivi punde nimesikia kutoka radio moja kipindi cha michezo kuwa Simba imekuwa ikifanya vibaya katika michezo yake hasa ile ya kimataifa moja ya sababu eti ni vile hawana kocha msaidizi, sasa wamepanga na wameshamalizana na kocha wa KMC wanamchukua wao

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo hapa Mbeya City walikuja vizuri sana katika soka watu tukafurahi kwa timu hii ya mkoani kuzipa challenge kubwa timu kubwa, kilichofuatia Yanga wakamchukua kocha wao! Timu ikapotea hadi leo

Hivyo hivyo tumeshuhudia wachezaji wengi wazuri wanaoibukia timu changa na kuzisaidia wanarubuniwa kuja kuzichezea hizi timu za Simba na Yanga na mwisho wengi wao wanapotea. Tushukuru tu akina Samatta na Ulimwengu hawakua na muda sana ndani ya timu hizi vinginevyo ndio ingekua basi

Kiukweli timu hizi hazina jipya na kuendelea kwake ni ndoto, kwanza hazina weledi wa kutafuta wachezaji wenye viwango ndio maana wana ng'ang'ania wachezaji wazee walio expire miaka mingi. Vipi unategemea wachezaji kama Okwi, Ngasa, Boban?

Kikubwa serikali izifute klabu hizi mbili zipo hapo kwa manufaa ya baadhi ya watu kujaza matumbo na kuua kiwango cha soka nchini timu hazina vision ya kwenda mbali kimataifa,serikali tuondoleni timu hizi kabisa zifutwe,iwekwe mikakati ya kutengeneza kizazi kipya tutafika mbali hakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpira pesa...kocha wa KMC akienda Mikiani atalipwa zaidi ya 10 m
 
Mpira pesa...kocha wa KMC akienda Mikiani atalipwa zaidi ya 10 m
Sasa hivyo njaa ndiyo itatutesa sana na hata simba na Yanga zipo ki uchumaji zaidi kuliko taaluma ya soka
Tutabakia kucheza ligi ya ndani tu na ushabiki mwiiiiingi njaa mbaya sana wakenya waganda wote washatuacha na watatuacha mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaonaje uanzishe timu yako hayo yote ili iwe mfano bora wa kurekebisha makosa ya Simba na Yanga
 
Back
Top Bottom