Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Mkuu Humble African kwanza asante kwa uzi huu maana utazidi kufungua watu akili kujua kuwa ni FOREX SIO UTAPELI, nami nasema FOREX SIO UTAPELI.
Labda nikusahihishe jambo moja au mawili ili kuondoa utata.
MOJA ni kuhusu IB(Introducing Broker), Brokers kama wafanyabiashara wengine wanahitaji watu watakaofanya nao biashara kwahiyo walitengeneza affiliate program ambayo itamuwezesha mtu kuweza kupata faida iwapo atamuongoza mtu afikie maamuzi ya kufanya trading na Broker huyo, yaani kumtambulisha Broker!!Sasa kuna sehemu umesema kuwa IB inampa faida mtu iwapo huyo trader atapoteza pesa tu. Hii sio kweli kabisa. Mtu mwenye link ya IB anapata faida kutoka kwa broker kwa zile SPREADS wanazokatwa traders wanapofanya trading(Hapa traders watanielewa). Broker anakugawia sehemu ya ile faida ya spread pekee na sio kwamba hadi mtu apate loss. Mfano mtu akifungua trading account kwa kutumia link hii: Templer FX Trader basi atamuwezesha mtu mwenye link kupata faida kutoa kwa broker, inamaana faida ya broker itapungua kwa sababu atamgawia na mwenye IB link au ukiamua kujiunga moja kwa moja basi broker atakuwa anachukua faida yote ya SPREADS. Sasa kwa trainers wanakuwa na wanafunzi wengi na akiishawafundisha waende wapi sasa, inabidi uwatafutie broker. Sasa hapo ndipo broker wanakupa link ya faida yaani IB.

PILI, Kuna aina kadhaa za brokers, Moja ni A Broker ambaye yeye anakuwa kama middle man tu anakuunganisha trades zako na liquidators na yeye anafaida na SPREADS tu mfano ni TemplerFX: Unaweza kuwaangalia hapa Templer FX Trader, au wanaweza kutoza Commission mfano ni Tickmill: Unaweza kuwaangalia hapa Tickmill: Trade Forex & CFDs with an FCA UK regulated Forex Broker.
Sasa kuna broker wanaitwa B Broker, hawa ni wabaya kwa sababu wanafanya trade against you, 'They Book traders' Yaani wewe ukifanya SELL wao wanafanya BUY kwa pair hiyohiyo kwahiyo kupoteza wewe yeye anapata na hao wanaweza kuwatumia mentors kuwahadaa traders ili wapoteze ili broker apate na hao wanafanya kwa makubaliano ya malipo haramu ambayo haya malipo sio ya IB bali uhuni, wizi, na utapeli.

Kwahiyo ni vyema kwa traders kuwa makini na kuchagua brokers wanaoaminika na ambao wana sifa nzuri kwa traders wengine na sio kuletewa tu.
Pili kampuni(Trainers) sasa zimeongezeka nashauri watu wawe makini sasa kujua wapi wanajifunzia mfano kwa sasa najua kampuni kadhaa ambazo wote wako vzr na wana broker ambao wana sifa nzuri za utendaji. Kampuni hizo ni kama DAR FOREX ACADEMY chini ya Carl, +255MillionairesFX(Sijui Mhusika), na Tanzania Forex Institute(TFI) chini ya bwana mmoja nadhani ni David (Naomba kurekebishwa kama nimekosea).

TAHADHARI
Kwa wale ambao wanadhani forex ni nafuu ndio hao wanaenda kuibiwa!!!!!Unafundishwa Forex kwa 100,000 kwa siku 5 halafu unaanza kufanya trading siku hiyohiyo ni wizi.
Forex ni gharama, kubalini kugharamika, wekezeni kwenye kupata elimu bora ili kujilinda na kupotea kwa fedha zako. Wengi wanapoteza hela kwa sababu wanaamini forex haizidi 100,000 na huko ndipo hao trainers wanaingia makubaliano na brokers wa kuwaibia!!!!!

Poleni sana mliokumbana na kadhia hii lakini FOREX IS REAL. Pata elimu sahihi tu na muongozo sahihi.
thanks forex nilijua hata kabla ya ontario kuleta uzi huu.
 
Mtu Aliyenunua Hata Lexus Au Kujenga Nyumba Au Kuestablish Stable Business Pesa Katoa Forex Embu Aseme Hapa Maana Comments Mnasema Mnapakua Mpesa Usd 50 Kwa Siku,ila Hamjasema Mafanikio Mwee,embu Tuvutieni Na Sisi Watanzania Wenzenu Tuingie Kama Ambavyo Ontario Alivyowavuta Na Story Ya Mansion Na Mercedes O Km,
 
SEMA LEO NI IJUMAA GBP/AUD SINA NENO

bisf.JPG
 
Mtu Aliyenunua Hata Lexus Au Kujenga Nyumba Au Kuestablish Stable Business Pesa Katoa Forex Embu Aseme Hapa Maana Comments Mnasema Mnapakua Mpesa Usd 50 Kwa Siku,ila Hamjasema Mafanikio Mwee,embu Tuvutieni Na Sisi Watanzania Wenzenu Tuingie Kama Ambavyo Ontario Alivyowavuta Na Story Ya Mansion Na Mercedes O Km,
Mkuu hiyo bznes watu wameanza mwishon mwa mwaka jana tu leo hii wajenge? Imekuwa ni kuchota hela et? Hakuna bznes ya hivyo ile bznes ukiitazama kwa haraka unawezafikiri ni nyepesi lkn ingia kuifanya ndo utajua ugumu wake hasa ukiwa na ka acc ka dola 100 ndo itakuwa unachoka tu
 
Nikipata time ntaanzisha uzi...... huyu Dogo Ontario arudishe PESA za watu..... FOREX is real sema ni kama sports betting tu... utofauti wake FOREX n kusoma soma ma vitabu.... but n same na betting.. huwez tajirika through FOREX....

Ukiachana na utapel watu kama akina Ontario.. behind FOREX kuna kitu kikubwa sana ambacho watu hawakijui thus why wanapoteza.... FOREX ingekuwa kama Ontario na watu wengine wanavyoaminisha hakuna mtu angekuwa masikini.. watu wote tungekuwa matajiri.....

Kuliko mtu afanye FOREX bora afanye sports betting TU....

Mkuu usiunyeshe ujimga wako mbele ya watu you know nothing
 
Mtu Aliyenunua Hata Lexus Au Kujenga Nyumba Au Kuestablish Stable Business Pesa Katoa Forex Embu Aseme Hapa Maana Comments Mnasema Mnapakua Mpesa Usd 50 Kwa Siku,ila Hamjasema Mafanikio Mwee,embu Tuvutieni Na Sisi Watanzania Wenzenu Tuingie Kama Ambavyo Ontario Alivyowavuta Na Story Ya Mansion Na Mercedes O Km,
Word..... unakula leo $50.. siku mbili baadaye unaunguza kila kitu then the cycle begin
 
Kuna watu kibao humu JF walituasa kwamba Forex ni utapeli hilo kwanza napingana nalo kwa nguvu zote sababu sio kweli kwamba forex ni utapeli kabla sijafunguka mengine niwathibitishie nimejiridhisha bila hata lepe la mashaka kwamba Forex is real and its my future lifestyle na binafsi sijioni nikikoma kufanya Forex licha ya haya magumu ninayopitia bali mawazo yao ninayachukuliaga kama catalyst ya kutaka kuzidi kuijua hii biashara kwa mapana zaidi kujua weakness na strength zake na kujua potential scammer, wezi na matapeli wakoje maana wametawala hii biashara kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na money liquidity kubwa kuliko soko lolote duniani..more than 6 trillion USD is traded daily on the Global financial market..hiki ni kiasi kikubwa sana hivyo matapeli huwa wanazengea zengea kwenye magap Kama haya yenye mkwanja mrefu..my economic cake pie is in Forex that's why I wont quit it easily.

But changamoto kubwa ya Forex ni hawa brokers na trainers..ninaposema trainers nazungumzia mtu kama Ontario hawa waliochungulia fursa mapema na kuintroduce kwa watu nchini kwa kigezo cha kuitoa elimu kwa bei sawa na bure tusijue wana agenda yao ya siri na Wasauzi ya kutaka kuwaliza watanzania wenzao.

Ontario ni mtunzi mzuri wa story na ana kipawa cha kusimulia na kushawishi kwa ufasha na ni mtu mwenye uelewa mpana wa mambo but anakosa kitu muhimu sana katika maisha uwezo wa kusocialize na watu in harmony..he is not a leader he is a boss na ukiangalia there is a thin line between a leader and a Boss..Ontario ana dharau, kiburi, na kejeli mbaya sana bila kujalisha umri wa anaeongea nae. Hana attentive listening ukiongea nae anakuangalia kama Choo na hajali lolote najua wengi waliokutana nae watakiri huu ukweli mchungu kwake ukiona mtu ana urafiki na Ontario ujue huyo mtu analazimika kujishusha sana kwa huyu dogo ili waende along. Huwa nashangaa ni rafiki sana na Bold. Pole sana Bold..I know what you going through.

Wahenga humu walituhasa kwamba ukiitwa kwenye fursa tafakari mara mbili yaweza kuwa wewe ndio fursa.anyways tulipoitwa kwenye fursa mwanzoni mambo yalienda vizuri na humu tulikuwa tunavurumusha screenshot za profit tu kwa maelekezo ya Ontario ili tuwakoge haters hadi haters wakafyata but kadri siku zilivyoenda mambo yakawa kimya ikawa ni loss daily tu watu wamechukua viinua mgongo vyote vikafyekwa sokoni. Hakyamungu!

Saga lilianza around mwezi wa kumi baada ya Ontario kula njama ya siri na broker awe anampa pips 2 kwa kila kichwa na zikiwa zinatoka calls kibao kombo kwa siku na zote zilikuwa sio accurate hivyo na watu kutengenezewa mazingira ya kutrade more often inamaanisha wakitrade watu 1000 wakafungua position 7 kila mmoja na idadi ya spreads pips anazopewa kutoka kwa broker kwa mtu mmoja ni 2..kimahesabu anapata 1000×7×2= 14,000 pips hizi ni dola kibao kwa siku ..wandugu wanojua mahesabu zaidi wanajua ni madola kiasi gani jamaa kavuta, hili suala alituficha but aliwahi kusema "Bob Marley you can fool some people for sometime but you can't fool all the people all the time"... Tukashtuka..tukamuuliza..akakubali ila akakiri alituficha na hayo mamilion yanayopatikana ni kwa ajili ya kuendeshea ofisi ya TMT co Ltd iliyoko pale Jangid plaza.. Watoto wa maskini tukakubali tu kwa shingo upande ila tukawa tumeghafilishwa na kusikitishwa sana na hizi njama zao..hili likapita na tukajilazimisha kukimeza maana ukipenda boga upende na ua lake.

Tamaa ni mbaya sana..licha ya kuchukua mamilion kutokana na hizo pips hawakuridhika..bado tena walikuwa wanachukua pesa kibao kwa siri kwa ajili ya IB link kwa affiliate program waliotuunga nayo siku tunamaliza mafunzo kutoka kwa broker kwa sisi tukipata loss sokoni wao wanapata chochote maana broker wao ni market marker. Hakyamungu! People are heartless.

Kama ilivyo asili ya watu wenye tamaa mbaya wakivurugana basi wao hukimbilia kutafuta sympathy ya Wateja..juzi wakavurugana broker na TMT kama ilivyo tabia ya wezi na matapeli kugeukana.. Majuzi wenyewe wanakuja na habari kwamba yule Broker ni market Maker na mwizi..kweli? Wakati wewe mentor umeishi South afrika na umekuwa Trader kwa miaka kibao bado hujui status ya broker unae trade nae? Na inakuwaje mrecomend broker mwenye walakini na competency na efficiency yake? Broker nae anajitetea kwa kutuma texts kwa Wateja privately akimtuhumu huyo mentor kuwa ni batili na mbabaishaji na kuwasihi watu wamuignore!? Blalifuli!

Tangu mwanzo mchakato uligubikwa na walakini mkubwa uliokuwa unaendelea..kwanza kumlazimisha mtu afungue real account baada ya siku tano tu za kumaliza mafunzo na aweke laki tano kuanza kutrade ilikuwa ni ishara ya wizi wa wazi sema tulikuwa na trust na maneno sukari ya Ontario, thus we were blind and fear of missing out easy Money.. Hatukujua!

Kutoa calls zaidi ya 7 kwa siku ni ishara mbaya ya kuwafanya clients waovetrade then wao wapige hela. Wizi huu.

Kuwaambia watu waongeze position ilhali wako in deep red ilikuwa ishara ya wizi, kuwataka watu waburn account zao wao wanufaike.

Kudiscourage matumizi ya stop loss ilhali ndio silaha ya kukinga mtaji wako kwenye Forex ilikuwa ishara ya wizi.

Watu wapoteze zaidi ili mpate zaidi maana kila ijumaa ilikuwa tunapunwa hela yote ya wiki nzima.

Mungu sio Sholo Mwamba, Yule broker market maker aliekuwa anatupiga sisi kwa tamaa kapitiliza kawafanyia mtimanyongo hadi kampuni ya TMT kaipuna zaidi ya nusu billion mapema mwezi wa kwanza. Imagine kampuni hii Changa ya huyu dogo imewazaje kupata nusu billion kwa muda mfupi hivi? Ni mikwanja aliyotuibia sisi misukule wake. But in life! "easy come..easy go"..ukikipata kiwepesi..kitaondoka kiwepesi pia. Nusu billion gone in a single month. Kweli JP Market broker ni hayawani!

Nitoe Rai kwa Ontario...sio kwamba namchukia hapana Bali naamini biashara inayohusisha watu moja kwa moja haiwezi kutokana na tabia yake mbaya ya asili..biashara na dharau, kebehi, utapeli na matusi havichangamani milele. Ni vyema akaendela na kilimo apate mil 19 zake kwa siku. Ameharibu kitu muhimu sana katika maisha yake ya biashara "Brand" and trust ya watu wengi aliowavuta kwa maandishi matamu humu JF..Trust ya watu pekee ni mtaji mkubwa kuliko hata mtaji wa fedha.

Namshukuru kwa kutuletea fursa hii adhimu lakini isiwe sababu ya kutuibia, kututapeli na kutunyanyasa economically and emotionally.

Rai kwa traders waliopigwa za uso na ndugu yao.."if you want to be strong learn how to fight alone" kwa kuwekeza Kwenye skills and self learning tunaweza kuwa self consistency profitable traders..let's ignore TMT they are scammer and predators and I don't recommend anyone to trust them.

Oooooopsiiii! Finally misukule wa Ontario tuko huru but tuko nyang'anyang'a kiuchumi. But it feels good kuwa huru.

Forex sio utapeli, matapeli ni mawakala wake.

Ni bora walimkavu...kuliko walimwengu!

Freedom!.
 
Warren buffet(the intelligent investor)
"mistakes comes from misunderstanding"
kwa iyo ndugu zangu nawashauri kutoingia kwenye biashara yoyote pasipo kuifahamu,jitahidi kwanza kuifahamu kupitia kujifunza(kusoma) business books,na vinavyohusu biashara yenyewe.ndipo huweze kuemploy pesa yako.
by malima ,the intelligent investor.
 
Chief chief nimesema tokea mwanzo kuna kitu behind FOREX... .. kikubwa tu ndo maana nasema FOREX is like Betting.
Usipende kufananisha fananisha vitu boss .

Na hii inaonyesha wewe forex huijui kabisa yaani empty kabisa .

Na ndio maana wapambe nuksi wengi humu .

Wanajidai walitoa maonyo wakati hio forex yenyewe hata kitabu kimoja hawajawahi shika .

Na hawajui kitu kabisa

Mimi namshukuru Ontario kunifumbua macho lakini namlaumu yeye na timu yake kufanya tunaofanya forex kweli kuonekana tumepotea njia .

Na nashauri tu moja afunge hio kampuni yake au awe trainer mambo ya kuwapa watu signal kkuwa chagulia beokers ndio hutuletea kelele watu wapuuzi kama kama hivi tunaovyoona hapa

Forex is real forex is not for everyone forex is very risk

Forex 50% is technique and remaining 50% is pyschology .

Kama hujui vitu hivi plizi stay out acha kumwaga sumu hapa
 
Mkuu Humble African kwanza asante kwa uzi huu maana utazidi kufungua watu akili kujua kuwa ni FOREX SIO UTAPELI, nami nasema FOREX SIO UTAPELI.
Labda nikusahihishe jambo moja au mawili ili kuondoa utata.
MOJA ni kuhusu IB(Introducing Broker), Brokers kama wafanyabiashara wengine wanahitaji watu watakaofanya nao biashara kwahiyo walitengeneza affiliate program ambayo itamuwezesha mtu kuweza kupata faida iwapo atamuongoza mtu afikie maamuzi ya kufanya trading na Broker huyo, yaani kumtambulisha Broker!!Sasa kuna sehemu umesema kuwa IB inampa faida mtu iwapo huyo trader atapoteza pesa tu. Hii sio kweli kabisa. Mtu mwenye link ya IB anapata faida kutoka kwa broker kwa zile SPREADS wanazokatwa traders wanapofanya trading(Hapa traders watanielewa). Broker anakugawia sehemu ya ile faida ya spread pekee na sio kwamba hadi mtu apate loss. Mfano mtu akifungua trading account kwa kutumia link hii: Templer FX Trader basi atamuwezesha mtu mwenye link kupata faida kutoa kwa broker, inamaana faida ya broker itapungua kwa sababu atamgawia na mwenye IB link au ukiamua kujiunga moja kwa moja basi broker atakuwa anachukua faida yote ya SPREADS. Sasa kwa trainers wanakuwa na wanafunzi wengi na akiishawafundisha waende wapi sasa, inabidi uwatafutie broker. Sasa hapo ndipo broker wanakupa link ya faida yaani IB.

PILI, Kuna aina kadhaa za brokers, Moja ni A Broker ambaye yeye anakuwa kama middle man tu anakuunganisha trades zako na liquidators na yeye anafaida na SPREADS tu mfano ni TemplerFX: Unaweza kuwaangalia hapa Templer FX Trader, au wanaweza kutoza Commission mfano ni Tickmill: Unaweza kuwaangalia hapa Tickmill: Trade Forex & CFDs with an FCA UK regulated Forex Broker.
Sasa kuna broker wanaitwa B Broker, hawa ni wabaya kwa sababu wanafanya trade against you, 'They Book traders' Yaani wewe ukifanya SELL wao wanafanya BUY kwa pair hiyohiyo kwahiyo kupoteza wewe yeye anapata na hao wanaweza kuwatumia mentors kuwahadaa traders ili wapoteze ili broker apate na hao wanafanya kwa makubaliano ya malipo haramu ambayo haya malipo sio ya IB bali uhuni, wizi, na utapeli.

Kwahiyo ni vyema kwa traders kuwa makini na kuchagua brokers wanaoaminika na ambao wana sifa nzuri kwa traders wengine na sio kuletewa tu.
Pili kampuni(Trainers) sasa zimeongezeka nashauri watu wawe makini sasa kujua wapi wanajifunzia mfano kwa sasa najua kampuni kadhaa ambazo wote wako vzr na wana broker ambao wana sifa nzuri za utendaji. Kampuni hizo ni kama DAR FOREX ACADEMY chini ya Carl, +255MillionairesFX(Sijui Mhusika), na Tanzania Forex Institute(TFI) chini ya bwana mmoja nadhani ni David (Naomba kurekebishwa kama nimekosea).

TAHADHARI
Kwa wale ambao wanadhani forex ni nafuu ndio hao wanaenda kuibiwa!!!!!Unafundishwa Forex kwa 100,000 kwa siku 5 halafu unaanza kufanya trading siku hiyohiyo ni wizi.
Forex ni gharama, kubalini kugharamika, wekezeni kwenye kupata elimu bora ili kujilinda na kupotea kwa fedha zako. Wengi wanapoteza hela kwa sababu wanaamini forex haizidi 100,000 na huko ndipo hao trainers wanaingia makubaliano na brokers wa kuwaibia!!!!!

Poleni sana mliokumbana na kadhia hii lakini FOREX IS REAL. Pata elimu sahihi tu na muongozo sahihi.
Kuna kitu sijakuelewa mkuu
yaan b broker uki sell ye ana buy?ina maana ukichukua mt4 mbili ya ECN broker kama pepperstone au tickmill nab broker like jp markerts afu uka place the same order kwa pair moja lets say EURUSD pote pote wth same sl na tp je graph zinakwenda in different direction au vip yaan hapa ndo huwa sielewagi broker anakuibiaje apart fromSPREAD kubwa
 
Huyu Dogo aliwahi kuniahid kunipa laki NNE km mtaj humu humu JF kila nikimchek text kwa namba yake ya wasap anafungua text anasoma then hajibu chochote , niliendelea kumchek km miez miwil hv anafungua text zen anakausha , daah kitendo kile kiliniuma sana maana ni dharau ,, ila namshukuru hakunisaidia ile laki NNE maana ningekuwa km kijakaz wake masuala ya kunyenyekea sio mazur, ,,Dogo sio sir dharau sana yan
Acha kupenda kitonga mtu mzima na ndefu zako yeye hata hakujui anaanza wapi kukupa hela kubwa kama laki 4 .

We jamaa hata hujui kujiongeza mtu wa ajabu sana

Yaani jibaba zima linasubiria laki 4 kwa dogo hahahah

Na angekupa ungeichoma ndani ya dakika kadhaa au ungeenda kuhonga na kunywea viroba huko uchochoroni

Bora alivyonyuti

Siku ingine akili yako ifanye kazi vizuri
 
Back
Top Bottom