Down To Earth
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 21,940
- 16,643
fanya kweli na kapicha kakeHahahahaa haya bhn
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
fanya kweli na kapicha kakeHahahahaa haya bhn
Ulitumia muda gani kuiandaa hiyo heading au ni msemo ambao ulikua nao kichwani tu... Anyway, uko na usimuliaji mzuri and napenda unavyobend na kutwist maneno kwa namna isiyoruhusu kugeuza hata shingo pembeni pindi tu unapoianza kuisoma episode fulani.Ahsante Vien.. Naidodosha soon. Hii weekend ya moto sana.
Ahsante sana kwa kuvutiwa na namna ya uwasilishwaji wa simulizi yangu. Karibu sana.Ulitumia muda gani kuiandaa hiyo heading au ni msemo ambao ulikua nao kichwani tu... Anyway, uko na usimuliaji mzuri and napenda unavyobend na kutwist maneno kwa namna isiyoruhusu kugeuza hata shingo pembeni pindi tu unapoianza kuisoma episode fulani.
Hakika haikuja tu lakini baada ya kujua nini nahitaji kuwasilisha na aina ya hadhira nayo ikusudia hapo ndio heading hio ikapatikana. Karibu PM.Ulitumia muda gani kuiandaa hiyo heading au ni msemo ambao ulikua nao kichwani tu.
Okay... ShukraniAhsante sana kwa kuvutiwa na namna ya uwasilishwaji wa simulizi yangu. Karibu sana.
Hakika haikuja tu lakini baada ya kujua nini nahitaji kuwasilisha na aina ya hadhira nayo ikusudia hapo ndio heading hio ikapatikana. Karibu PM.
Hudaiwi kwa leo.Tuendelee EPISODE 10B
Lile penzi la jana likafufua hisia zilizokuwa zimeanza kupoteza uhai. Nikajikuta wazo la kubutua ya mwisho niondoke linakosa nafasi. Miezi mitatu ikakatika nikiwa nimekutana na Recho kwa wastana wa mara moja kila mwezi.
Mkeka wa tatu ukaitika, hii sasa ni ajira rasmi ya kudumu. Kituo cha kazi si tu ni mkoa mwingine bali ni kanda nyingine kabisa. Kabla ya kumjuza Recho nilijiuliza maswali machache ikiwemo. Mosi, Mimi nipo na Recho katika mahusiano, je malengo yetu ni nini. Pili, kama kaweza kumcheat mumewe kwa sababu ya umbali vipi kwangu 'mpango wa kando'. Majibu yangu yote yalionesha hapa sina tena changu.
Kama ilivoada, binadamu tumeumbwa kuzoea/ adapt mabadiliko fulani katika kipindi fulani. Ndivyo ilivokua kwangu. Nilizoea kutafutwa mara moja kwa wiki, au hata wiki kukatika bila kutafutwa na hii iliiandaa akili yangu kuwa tayari kupokea taarifa yoyote mathalani kuachana na Recho rasmi. Majira ya kuondoka kwajili ya kazi yalipo karibia nikamjulisha Recho kwa njia yetu ileile.
Mimi " Recho nina habari njema". "Habari gani?" Akajibu. Kwa kuchat hutanielewa, ukipata nafasi nipigie". Akanipigia na nikamwambia nimebahatika kupata kazi mkoa X na Nina week tu kureport. "Dah! jamani kweli Mungu anajibu maombi. Hongera!!". Mimi " Ahsante sana... umenisapoti sana". Akacheka kisha "So waenda lini, Fanya basi uje tuagane nikutakie na safari njema". Mimi " Unadhani naweza kuondoka bila kumuaga mama la mama".
Tulipanga tuonane na hii ilikua nje na kwake. Naweza sema hii ndio ilikua our first date. Sijui alidanganya nini kwa jamaa yake, aliomba nichukue na chumba ili tusiongee kwa kujibana badala yake tuwe 'free' tuagane vizuri.
Ndani ya chumba chenye hadhi ya wastani nipo na Recho. Nikamuonesha vithibiti vya uhalali wa kazi. Recho " Babaa sasa umepata kazi ambayo siku zote tumekua tunamuomba Mungu...nenda ukafanye kazi". Akaendelea " Mimi usiniwaze kabisaa et uko mbali tutaishije.... umepata nafasi usiichezee, Mungu atampa mtu mwingine". "Unanisikia babaa.." nikaulizwa mwanaume .
Mimi "Yep yep.. ila kukuacha hivi inanipa mawazo". Recho kwa sura ya upole na sauti ya kuombea hela ya sadaka akaendelea, " Z mimi sio binti mdogo kwamba nitaanzisha mahusiano mengine...we Nenda kapambanie ndoto yako". Hakuishia hapo akaendelea, "Ukipata likizo utakuja, mbona tumeonana zaidi ya mara tatu toka jamaa kaja!!... itawezekana tu!".
Hii siku nilipewa mawaidha ya kutosha na Recho. Kubwa alilosisitiza zaidi ni Mimi kujishikilia. Nitangulize kazi mbele mapenzi yafate. Alikuwa sahihi sana, nafikiri aliweza kuona udhaifu niliyokuwa nao juu yake.
Moyoni nilijisemea " walahi huyu mwanamke angekua ndio mke wangu, kwa umri wangu huu kimaisha ningekua mbali sana" . Tuliongea mengi na baada ya hapo tukaziruhusu sehemu zinazotofautisha jinsi zetu nazo zipeane mawaidha.
Recho aliondoka mishale ya saa nne usiku kurejea kwake. Nilala pale huku nikiwa natafakari maisha mapya mbali na mwanamke ninayempenda yatakuaje.
Msomaji wangu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Hakika pamoja na ukosefu wa uadilifu katika ndoa yake, Recho alinisaidia kupiga hatua kimaisha mchepuko wake.
Pamoja na kwamba ni kweli nimeonekana kumkatia tamaa kimapenzi lakini bado yeye alionesha yupo ndani ya maisha yangu. Aliniuliza kila hatua niliopitia kwanzia safari kuelekea mkoani mpaka mapokezi kazini. Kwakweli aliweza kuniteka. Nilikuwa najisikia huzuni pale wazo la lini nitamuona tena Recho likiniijia.
Wiki ya kwanza ikaisha, mwezi ukapindika ndani ya makao mapya. Mimi na Recho bado tunawasiliana japo ni kwa style yetu ambayo ni limited. Wiki ya kwanza ya mwezi uliofata Recho ghafla akaacha kujibu status zangu na alikua anaziona, nilipojaribu kupiga simu yake muda wote ilikua busy, Yani nimekua 'blocked.
Ikanistua sana kuna nini kinachoendelea. Nikavunga kwa hio wiki niki 'assume' huenda yupo mazingira magumu kuwasiliana na mchepuko wake. Wiki iliofata hakuna madiliko. Tayari red light kichwani, nikasajili namba mpya na kumpigia nijue changamoto nini.
Simu ikaita kwa muda na haikupokelewa. Nilijaribu tena bila mafanikio. Hofu sasa ikanijaa kwani Recho kapatwa na nini.
Mida ya saa Moja kasoro akanipigia kwa namba yangu mpya " Hello". Nikaitikia "Yes Hello!". Recho "nimekuta umenipigia, sorry nani?". Mimi "Hata sauti hujaijua....ok Z hapa". Baada ya kujitambulisha vile Recho akakaa kimya kwa sekunde kadhaa nikamstua.
"Hello Recho.... ni mimi Z naona umeniblock na hata WhatsApp sikupati, tatizo nini niambie tafadhali". Recho pasipo kuongea lolote alikata simu. Sikuamini kile kitendo na nikivojaribu kupiga tena tayari alikwisha block hio namba yangu.
Maadamu niliweka reserve wazo la siku moja nitaachwa, sio kuachana na Recho kutokana na umbali nikajisemea hii Ndio tayari byebye. Kumbe Haikua hivyo. . . . .
Naomba niishie hapa lakini kesho tutamaliza kisa hiki, niombe radhi kwa ufupi wa kipande cha Leo. Ni muda wangu kwa leo si rafiki
sana. Ahsante!
🤣🤣🤣na sauti ya kuombea hela ya sadaka
Sawa 😄Mkuu... hahaha! Nafikiri sio sahihi.
Ndugu msimuliaji nataka nikwambie siku utakayopakwa mafuta utusimulie pia kwa madoido hivi hivi😂😂Tuendelee EPISODE 10B