Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Salaam wadau,


Maisha yanatupa zoefu nyingi sana, zenye matokeo chanya na wakati mwingine zinaweza kukuachia alama ya uchungu isiyosahaulika. Mara nyingi sio kwa kupenda au kuridhia maisha automatically yanakupa darasa. Hiki ni kisa Cha ukweli.

Nitajaribu kuweka wazi mambo magumu ili upate picha japo kwa kusoma. Nikusihi tu soma na chukua machache kwajili ya kuboresha mahusiano Yako. Wala usinijaji kwa yaliotokea maana huko nilishatoka 6 years back na sijutii. Toba ilishamaliza kila kitu. Twende kazi.

Miezi miwili tu baada ya kumaliza elimu ya juu nipo home mark timing ndio nakutana na aliyefanya niandike huu Uzi. Tulikutana dukani mtaa Mmoja, wakati Mimi nafika yeye alikua akisubiri chenji/chenchi yake. Muuzaji alitoka kidogo ikabidi nimuulize yeye sasa. "Habari Yako, huyu yupo wapi ?". Akanijibu. " ametoka kidogo kufata chenchi anarudi sasahivi". Hili duka lilikua ndani ya mji wa mtu, unaelewa sikuhizi unajenga nyumba Yako na frame kadhaa mbele yake. Ndivo ilivokua.

Mimi sikuona Haya kuanzisha stori nae ili kubuy time. Mimi " sorry wewe ni mwenyeji huu mtaa ?" Huyu dada naomba tumuite Recho. Akanijibu "Ndio mi nikaa hapo tu jirani, na wewe ?". Mimi "Me pia nyumba ya tatu kutoka hapa". Recho " ooh! Kumbe tupo jirani... sasa mbona Mimi sijawahi kukuona na kwangu we ni mgeni kabisa". Nikamjibu Hilo swali kuwa na Mimi nilitaka nimuulize nivile tu kaniwai. Huku ukweli nikwamba ni kweli sio mkaaji sababu ya shule. Basi muuzaji alirudi na akampa chenchi yule dada akarudia nyuma kunipa nafasi nihudumiwe lakini hakuondoka nikama alikua akisoma sms kwenye simu yake.


Wadau mwanamke udhaifu wake upo masikioni. Maana yake ni unaweza athiri namna yake ya kufikiri kwa kupenyeza maneno matamu kwenye sikio lake. Lakini kwetu wanaume Macho ndio weakpoint. Kutaamani kunaanzia kwenye kuona. Binafsi nilimtamani yule dada. Why ? alikua amevaa tight ndefu ya grey, t-shirt ambayo kwake ni oversize chini kabisa kaua na kikuku Cha chain mguu mmoja. Shape na muonekano mzima of course alinivutia japo sijamuelezea kwa 100% maana sio dhima yangu ya msingi ingawa kama ungeiona picha yake insta naamini ungegusa kwenye kuview profile.

Bila kujua au kujali sikumpa tena attention kwani niliamini anaondoka lakini nilishangazwa na kitu. Nilisikia... " jirani me naondoka", nikama 30sec zilikatika toka anipishe nipate hudumu. Nikageuka chap naona ni kweli anashuka ngazi. Nikamwambia " sawa jirani tutaonana tena". Nilichonotice ni kama Recho alitarajia ninge endeleza maongezi sorts of maswali na hatimaye tubadilishane namba. Ukweli ni alikua sahihi lakini nilikaza tu maksudi maana niliamini kama ni jirani kweli na anakaa pale aliponionesha kwa kidole basi tungekutana mara nyingi zaidi maana nipo home sasa.

Kimsingi nilikua nimefunga zipu yangu kwa miezi kama mitatu hivi au ziaid hivyo nilikua hyper flani hivi. Hapa niweke kitu clear. Notion iliojengeka kichwani mwangu ni, mwanamke ambaye Anableach...anavaa vikuku...anatattoo. Iwe ni ana kimoja kati ya hivyo au vyote kwa pamoja ni Wanawake ambao wapo beyond the limits. Yaani kama kaolewa au anamtu kucheat sio issue na mambo ya bata hasa sex ndio issue zinawapa fantasy sana. Na hio Haina uhusiano na elimu yake . Super woman chukua hioo itakuaaidia. So niliamini tu hapa nitapiga hata iweje. Niliweka nia lazima nitamtafuta tu.

Kesho yake mida ya saa 5 asubuhi nilipita jirani kabisa na Ile nyumba na ilikuwa na fence. Kichwani nikawaza nigonge geti au nikaushe naona shetani akawini. Nikagonga geti, baada ya muda kidogo likafunguliwa. Aisee ni yeye Recho kafungua. " Jamani jirani umepajuaje hapa. Heeh! Karibu kumbe kweli wewe ni mwenyeji". Mimi " Jana baada ya kunionesha tayari nikajua ni nyumba gani haswaa" mara kidogo nyuma yake akafata mtoto mdogo wa kiume kama miake 4+. Sikuuliza lakini alinambia "Oh! Mwanangu huyu jirani, haya karibu basi ndani."

Kaka mkubwa niliingia Ndani, Moja kati ya very high risks nimewahi kufanya ni hii. Kuingia ndani ya mji wa mtu pasina kujua kaolewa au lah na kama kaolewa mwenye mke yupo ndani, katoka au utarudi muda gani... Leo tuishie hapa then kesho tujue yalionikuta, inshallah tunaendelea.
Msipende kukatisha mastory matamu kama haya 😂😂
 
Tuendelee EPISODE 10B

Lile penzi la jana likafufua hisia zilizokuwa zimeanza kupoteza uhai. Nikajikuta wazo la kubutua ya mwisho niondoke linakosa nafasi. Miezi mitatu ikakatika nikiwa nimekutana na Recho kwa wastana wa mara moja kila mwezi.

Mkeka wa tatu ukaitika, hii sasa ni ajira rasmi ya kudumu. Kituo cha kazi si tu ni mkoa mwingine bali ni kanda nyingine kabisa. Kabla ya kumjuza Recho nilijiuliza maswali machache ikiwemo. Mosi, Mimi nipo na Recho katika mahusiano, je malengo yetu ni nini. Pili, kama kaweza kumcheat mumewe kwa sababu ya umbali vipi kwangu 'mpango wa kando'. Majibu yangu yote yalionesha hapa sina tena changu.

Kama ilivoada, binadamu tumeumbwa kuzoea/ adapt mabadiliko fulani katika kipindi fulani. Ndivyo ilivokua kwangu. Nilizoea kutafutwa mara moja kwa wiki, au hata wiki kukatika bila kutafutwa na hii iliiandaa akili yangu kuwa tayari kupokea taarifa yoyote mathalani kuachana na Recho rasmi. Majira ya kuondoka kwajili ya kazi yalipo karibia nikamjulisha Recho kwa njia yetu ileile.

Mimi " Recho nina habari njema". "Habari gani?" Akajibu. Kwa kuchat hutanielewa, ukipata nafasi nipigie". Akanipigia na nikamwambia nimebahatika kupata kazi mkoa X na Nina week tu kureport. "Dah! jamani kweli Mungu anajibu maombi. Hongera!!". Mimi " Ahsante sana... umenisapoti sana". Akacheka kisha "So waenda lini, Fanya basi uje tuagane nikutakie na safari njema". Mimi " Unadhani naweza kuondoka bila kumuaga mama la mama".

Tulipanga tuonane na hii ilikua nje na kwake. Naweza sema hii ndio ilikua our first date. Sijui alidanganya nini kwa jamaa yake, aliomba nichukue na chumba ili tusiongee kwa kujibana badala yake tuwe 'free' tuagane vizuri.

Ndani ya chumba chenye hadhi ya wastani nipo na Recho. Nikamuonesha vithibiti vya uhalali wa kazi. Recho " Babaa sasa umepata kazi ambayo siku zote tumekua tunamuomba Mungu...nenda ukafanye kazi". Akaendelea " Mimi usiniwaze kabisaa et uko mbali tutaishije.... umepata nafasi usiichezee, Mungu atampa mtu mwingine". "Unanisikia babaa.." nikaulizwa mwanaume .

Mimi "Yep yep.. ila kukuacha hivi inanipa mawazo". Recho kwa sura ya upole na sauti ya kuombea hela ya sadaka akaendelea, " Z mimi sio binti mdogo kwamba nitaanzisha mahusiano mengine...we Nenda kapambanie ndoto yako". Hakuishia hapo akaendelea, "Ukipata likizo utakuja, mbona tumeonana zaidi ya mara tatu toka jamaa kaja!!... itawezekana tu!".

Hii siku nilipewa mawaidha ya kutosha na Recho. Kubwa alilosisitiza zaidi ni Mimi kujishikilia. Nitangulize kazi mbele mapenzi yafate. Alikuwa sahihi sana, nafikiri aliweza kuona udhaifu niliyokuwa nao juu yake.

Moyoni nilijisemea " walahi huyu mwanamke angekua ndio mke wangu, kwa umri wangu huu kimaisha ningekua mbali sana" . Tuliongea mengi na baada ya hapo tukaziruhusu sehemu zinazotofautisha jinsi zetu nazo zipeane mawaidha.

Recho aliondoka mishale ya saa nne usiku kurejea kwake. Nilala pale huku nikiwa natafakari maisha mapya mbali na mwanamke ninayempenda yatakuaje.

Msomaji wangu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Hakika pamoja na ukosefu wa uadilifu katika ndoa yake, Recho alinisaidia kupiga hatua kimaisha mchepuko wake.

Pamoja na kwamba ni kweli nimeonekana kumkatia tamaa kimapenzi lakini bado yeye alionesha yupo ndani ya maisha yangu. Aliniuliza kila hatua niliopitia kwanzia safari kuelekea mkoani mpaka mapokezi kazini. Kwakweli aliweza kuniteka. Nilikuwa najisikia huzuni pale wazo la lini nitamuona tena Recho likiniijia.

Wiki ya kwanza ikaisha, mwezi ukapindika ndani ya makao mapya. Mimi na Recho bado tunawasiliana japo ni kwa style yetu ambayo ni limited. Wiki ya kwanza ya mwezi uliofata Recho ghafla akaacha kujibu status zangu na alikua anaziona, nilipojaribu kupiga simu yake muda wote ilikua busy, Yani nimekua 'blocked.

Ikanistua sana kuna nini kinachoendelea. Nikavunga kwa hio wiki niki 'assume' huenda yupo mazingira magumu kuwasiliana na mchepuko wake. Wiki iliofata hakuna madiliko. Tayari red light kichwani, nikasajili namba mpya na kumpigia nijue changamoto nini.

Simu ikaita kwa muda na haikupokelewa. Nilijaribu tena bila mafanikio. Hofu sasa ikanijaa kwani Recho kapatwa na nini.

Mida ya saa Moja kasoro akanipigia kwa namba yangu mpya " Hello". Nikaitikia "Yes Hello!". Recho "nimekuta umenipigia, sorry nani?". Mimi "Hata sauti hujaijua....ok Z hapa". Baada ya kujitambulisha vile Recho akakaa kimya kwa sekunde kadhaa nikamstua.

"Hello Recho.... ni mimi Z naona umeniblock na hata WhatsApp sikupati, tatizo nini niambie tafadhali". Recho pasipo kuongea lolote alikata simu. Sikuamini kile kitendo na nikivojaribu kupiga tena tayari alikwisha block hio namba yangu.

Maadamu niliweka reserve wazo la siku moja nitaachwa, sio kuachana na Recho kutokana na umbali nikajisemea hii Ndio tayari byebye. Kumbe Haikua hivyo. . . . .






Naomba niishie hapa lakini kesho tutamaliza kisa hiki, niombe radhi kwa ufupi wa kipande cha Leo. Ni muda wangu kwa leo si rafiki
sana. Ahsante!
Okay...!
 
Salaam wadau,

Tuendelee EP 04

Baada ya kuamka pasipo uwepo wa Recho, nikampigia simu. "Hello Good morning" alianza hivo kabla ya mimi kuongea. Nikajibu "morning... uko wapi..mbona hujaniamsha". Recho " Acha woga wewe, nimedamka mapema nikuandalie chai...hatahivo ipo tayari, njoo basi sitting room". Mimi "Poa am coming".

Hapo mapigo ya moyo yakarejea kwenye wastani wake wa kawaida. Nikaamka chap sitting room. Sasa bashasha lililokua usoni pa Recho hata mimi likanipa walakini, akanikaribisha chai. Niseme tu ilikua heavy breakfast, mpaka nikajisemea "kweli dawa imemuingia, sio kwa hospitality ile".


Kwa jinsi alivokua mchangamfu na bashasha nikaona kweli huyu sasa haisi ombwe la upweke tena. Hakika sikukosea ilikua hivo. Recho " Z tumelala wote Jana...nimekubali tuwe kwenye mahusiano lakini ujue kabisa, Nina mume wangu na ananipa kila kitu...najua namkose ila imeshatokea".

Akamalizia, " Ila Z unajua mapenzi wewe khah! Mwanamke gani huyo alikufundisha kut*mb*n*."
Nikabaki natabasam tu. Unajua vile unafeel pale mrejesho ukiwa chanya. Baada ya kifungua kinywa na story Chache nikasepa.


Nakumbuka Ile siku simu yangu haikukauka sms kutoka kwa Recho. Kama sio kila baada ya dakika moja basi ni tano ujumbe unaingia. Nilisifiwa sana na Mimi kurudisha salama vilevile. Sikumbuki takwimu vizuri lakini ndani ya Ile week tulikulana kana kwamba tupo honey moon Magoroto, Tanga.
Jina la Z likapoteza mvuto badala yake naitwa 'Daddy', 'Babaa' au 'my love'.


Ukisikia ndege kunasa tunduni hii sasa haukuishia kwake tu bali hata mimi nikajipata na hisia kalii sana juu yake. Ila hii haiku chagizwa na sex pekee, hapana kuna kitu cha ziada hapa alikifanya Recho. Nitasema baadae.


Mwezi wa pili sasa unaelekea kukatika toka tuanze rasmi wizi. Siku moja aliniambia hivi "unajua unanikula kiasi kwamba hata nikihesabu naona kabisa umezidi idadi ambazo Mimi na mume wangu tumefanya toka anioe." Akaendelea " Em tupunguze kidogo maana huyu akirudi atajua tu...ntashindwa kabisa kum 'act' tia!"

Mimi nikasalia kimya. Recho " unaonaje tuwe tunafanya mara mbili tu kwa week babaa...please kubali basi. Fanya hivo kunisaidia Mimi please".
Sikutaka uwe mjadala mkubwa nikamkubalia.


Ipo hivi, nilianza kwa kumtamani sana huyu dada, ukizingatia jinsi alivyojiweka na muonekano wake bila kusahau falsafa yangu dhidi ya wanawake type yake. Lakini kadri muda ulivosonga niliibua hisia kalii sana za mapenzi, nilihisi nimegraduate kutoka kumtamani na sasa nampenda.

Lile wazo lake likaanza kuniumiza kichwa tena (wivu). "Inakuaje anipangie e...au amepata mdau mwingine?" Hapa nikasahau kama mie mwenyewe ni mwizi, sasa naanza kuogopa kuibiwa mali ya wizi. Ila maadamu nilishakubali nikajisemea tutacheza na beat lakini twice a week Hapana.


Mambo hubadilika, sasa home familia ipo kwahiyo utokaji wangu sio huru sana kama hapo nyuma. Hata ratiba ya kumuona Recho ilibadilika japo sio kwa sehemu kubwa. Mara nyingi tulionana jioni. Wakati mwingine akiforce anione asubuhi basi nilifanya kwenda kwake.


Hii miezi mitatu ambayo nilikua clean bila sex nilikua kwenye mgogoro na kidemu changu cha chuo na Mimi nilikua tayari nimeridhia tuachane ukizingatia hatupo tena mkoa mmoja. Baada ya kufanikiwa kutengeneza mazingira ya kutolala home siku moja nikaenda kulala kwa Recho.

Kulivokucha saa 11 alfajiri sijui hii siku huyu dem tumuite Nailah wa chuo aliniota au vipi. Ilikua hivi:


Mimi na Recho ndani ya duvet, Boxer yangu chini, pichu ya Recho pembezoni mwa kitanda. Yaani tayari wazungu nimeshawahamisha makazi. Mlio wa sms ukasikika.
Kabla sijaendelea msomaji, mara zote tukiwa busy na ujinga wetu Mimi na Recho yule bwana mdogo kama hatakua amelala chumbani kwake basi hua anakua sitting room busy na cartoon.

Tulijitahidi kuficha uchafu wetu. Nakiri hapo tulifanikiwa. Ok tuendelee, mlio wa sms kuingia ukasikika na ni kwenye simu yangu. Kwa speed ya mwanga Recho aliiwahi simu yangu na kuniambia nitoe password. Mara nyingi nilikua nampa anakagua na hakuti kitu kwahiyo sikua na wasi. Simu yangu upande wa sms sikuset 'Hide Content'. Wakati ananipa nitoe nywila akaghairi kisha akaanza kusoma kwa Sauti. " UMEAMKAJE"?.

Nikauliza ni nani?. Akakaa kimyaa kisha akaendelea " Hii namba ninaijua, nimekalili namba za mwisho. Huyu ni demu wako".
Sasa kwa bahata mbaya au nzuri Mimi na Recho tulikua tunatumia simu aina Moja, Samsung alikua na uwezo wa kutafuta chochote kwenye simu yangu.

" Hii namba imekupigia sana japo si hivi karibuni lakini niliona ndio namba mnacheckiana sana... Haya nambie huyu ni nani na kwanini asubuhi hii anakutext."


Nikachukua simu mwenyewe nikaangalia namba, nikaona ni Nailah kweli. "Dah! Huyu Demu ananitakia Nini mimi... asubuhi yote hii sasa najiteteaje." Nikawaza kwa ukimya kisha nikamwambia. " mpenzi wangu, huyu ndio yule mwanamke nilikua nae chuo... nilishaachana nae ila hatakkubali matokeo".

Recho tena kwa Ngeli na jazba " I am the one who supposed to know umeamkaje kwasababu tumelala wote...huo ujasiri anautoa wapi kukutumia text asubuhi... Mimi sio mtoto Z !!!.
Noma sana!
 
Tuendelee EP 07

Nilipokea simu nikatega sikio kwa umakini. Recho " hello vipi". Mimi " Safi, Kuna usalama kweli..tulisha agana mpenzi wangu lakini!". Recho " kwakweli babaa hii dawa imeanza kunipa mawazo...sisikii chochote wakati nilitegemea mpaka saahivi mambo yawe tayari".
Mimi " ulimeza saa ngapi ?".

Alidai alimeza saa mbili usiku lakini sasa inaeelekea saa Saba hajahisi chochote kwa maana ya maumivu ya tumbo la chini au ishara za damu kumtoka. Nikamtuliza pale pamoja na kuwa Sina uzoefu na jambo la utokaji wa mimba na tukakubaliana alale tu tuone kesho itakuaje.

Kesho yake tukaendelea kuwasiliana huku Hali ikiwa vilevile. Toka tumeanza wizi Recho alipunguza kwa sehemu kubwa kunywa hasa Konyagi. Hakuacha kabisa lakini alipunguza, kuna kipindi alikua anaficha chupa kwenye viunga vya maua nje ili nikija nisione na anakula ndizi mbivu kuikata Ile harufu.

Bado niliweza kumgundua lakini kwasababu najua alikua akielekea kwenye uraibu sikumjia juu. Naelewa ingemchukua muda kuacha.

Hii siku ilipita pia pasipo dawa kufanya kazi na hapo tukaanza kushauriana atumie nyingine. Ila kabla ya kufanya hivo tuwasiliane na daktari tuone angeshauri nini. Asubuhi ile kimya, mchana kimya, usiku bado hakuna mabadiliko. Tukaagana saa 3 usiku kila mtu alale salama.

Binafsi ule usiku siku lala kabisa, nilikua kwenye hali ya kukosa amani na usingizi kabisa. Mungu saidia paka kucha. Nikapigia simu mwenyewe, "wewe upo sawa kweli, usiku sijalala kwa amani asee...na vipi bado tuu?!?". Recho " Z shukuru Mungu nimepokea simu yako...Mimi Leo nilikua nakufaaa". Akaendelea "Hivi kwenu huwa hamtoagi mimba eh?". Mimi nipo kimya namsikilizia kwa makini. " Hapa ndio nimemaliza kusafisha nyumba maana nilipakaza damu kila Kona".

Nikamdaka " So unamaanisha tayari!??". Recho " Sasa huelewi nini... ndio dawa imefanya kazi". Mimi " Dah! Anyway pole sana my love, kwahio damu imeacha kutoka au vipi". Recho " baby haiwezi kukata tu mara moja itaenda inapungua mwisho itaacha... ila mh! Ulizia vizuri kwenu, ukoo wenu itakua hamtoagi mimba!...kidogo nife".


Wiki ilikatika bado hajakoma kutoka damu, tukakubaliana aende kwa mtaalam/daktari acheki na asafishe masalia. Ikawa hivo na nafikiri ndani ya wiki mbili mambo yakawa shwari. Sasa likaibuka jambo hapa.

"Hivi mara yako ya mwisho kupima HIV ni lini?" Nikaulizwa swali. Mimi " Sikumbuki lakini jibu rahisi ni kesho twende wote hata maabara tu tukapime." Recho tena " unajua nimekuota vibaya sana leo... Yani Kuna mtu ananiambia huyo kijana unaetembea nae ni muathirika." Akaendelea " sasa na hivi baba ( .) anarudi nimejipata na hofu kweli".

Nikamuangalia kwa hasira kisha nikamwambia " Recho umefikia hatua ya kuniwazia mie nina umeme.... tumelala wote siku ngapi, na katika hizo siku tumetumia kinga mara ngapi?" Nikaendelea "Leo ni mwezi wa ngapi tupo kwenye mahusiano... kama na HIV ingekua hujaona dalili!?!?. Ok kesho mapema sana wote hospital ".

Kama ungeniona navoshout msomaji ungestaajabu. Recho ananizidi miaka 5, yaani ni mkubwa kwangu lakini nilikua kama Mzee wake katika kutoa kauli. Niliongea kiume na tena bila kupepesa macho pembeni wala kutafuna maneno.

Hapa chukua hii. Mwanamke ni mwanamke, hata awe ni Rais wa nchi ni mwanamke. Katika uumbaji mwanamke yupo kutii kile mwanaume utasema/amua juu yake. Ukitaka kuamini hilo mpe order mwanamke ya kufanya kitu kwa sauti ya kurembua huone reaction zake. Na baadae toa order hiohio kwa sauti ya mamlaka yani kiume uone tena reaction.

Hakika utekelezaji wa amri yenye mamlaka ndio utafanyiwa kazi chap pasina mapuuza.

Turudi kwa Recho. Baada ya kuongea vile nikaanza kuombwa samahani. "Basi naomba nisamehe mwanaume wangu. Jamani ndio unanikasikirikia hivo... alaf sijazoe unanikalipia hivi." Akaendelea " au hunipendi, usinigombeze bhana me nitaanza kukuogopa". Basi ili kutoa nyongo vizuri nikapelekwa chumbani. Kimoja tu nikasahau kwani nilikua nashoutia kitu gani.

Katika zile harakati za kuomba kazi maeneo tofauti tofauti kuna kazi moja mkeka ulitika japo ilikua ni nje kidogo ya mkoa na haikua ya kudumu, kama miezi sita tu. Sikua nimwemwambia Recho maana nilitakiwa kureport mwezi uliokua unafata na ndio kipindi hiko hiko mumewe Recho angerejea nchini.

Recho aliniomba kitu tena. Recho " kabla huyu hajaja naomba tujizoeshe mambo mawili." Mimi " enhee!". "Mosi, tupungeze kuwasiliana walau mara mbili tu kwa siku...pili, hii week nianche kabisa usiniguse tena". Kwangu Likija swala la kutomgusa Recho siwazi kingine zaidi ya kuhisia Recho ana mtu mwingine.

Nikamjibu "Kuhusu kuwasiliana nitajitahidi ingawa sina uhakika sana kama ntaweza... lakini kukula mama wangu utanisamehe. Wiki Hapana".

"Z lakini usisahau tunafanya hivi ili tusijestukiwa mapema...sio kwamba tutaachana my love". Akazidi kunisisitiza " tukiendelea kufanya sitaweza kumuigizia...ndio nitaweza siku ya kwanza lakini najua tu mbeleni atajua tu. Em nielewe basi jamani."

Kwasababu sipendi mijadala mirefu nikamwambia poa. Sasa hapa wivu ukaanza kunitesa. Mali sio yangu lakini ndio hivo nimepanda mtumbwi wa vibwengo tayari ntafanyaje. Kweli bhana siku hio pattern ya kuchat ilikua sio nzuri.

Rasmi sasa napiga simu zinaiita tu na hanirudii. Katika sms 10 Moja ndio inajibuwa tena zile 'K' au 'P'. Ajabu nikienda kwake mahaba kama yote ila kwa njia ya simu hapana. Hii ikanitesa kiasi na kufanya nizidi kupata hisia hasi dhidi ya Recho

Hayawi hayawi sasa sasa yamekua, wiki ijayo jamaa kathibitisha atatua katika Ardhi ya bongo. Toka nimeanza story huyu mwamba sijamzungumzia kabisa, ni kwasababu sio kiini cha ujumbe naohitaji uupate kupitia story hii lakini sio mbaya ukamfahamu kwa ufupi.

Jamaa ni mtumishi wa serikali na nafasi yake ni poa sana. Huyu mwamba alienda kujendeleza kielimu nafikiri, kwa bahati nzuri au mbaya nilikutana nae pasipo yeye kunijua na tukasalimiana kabisa. Hapa inahitaji moyo kidogo. Kipindi yupo nje mara kadhaa akiwa anavideo call na babe wake mimi nilikua nipo live. Hapo ndio tuwaogope wanawake.

Nikaoneshwa picha ya risiti ya ticket ya ndege, tarehe inasomeka ni siku tano mbele ndio siku ya safari. Na kweli sijamvua nguo Recho toka siku alioniomba nisifanye hivo.

Usichanganye, toka Recho agundue ana mimba, atoe na kupona ni mwezi sasa unakaribia kuisha. Kwahiyo mpaka jamaa anarudi unakua umetumia ule mwezi mmoja toka amjulishe mkewe kuwa angerudi Tz. Na nilimuweka mara Moja tu.

Sio kwamba nilishindwa kufosi penzi, Hapana. Najua udhaifu wa Recho upo wapi na ningeweza kutumia mwanya huohuo lakini niliona niheshimu tu kile alichoniomba kwani tayari nina jiona nimekua kirusi kuingilia familia ya mtu na bado niendeleze unyama. Hapa niliamua kuwa mpole kwanza.

Sasa silaha yangu kubwa ya mawasiliano iliobaki sio simu tena bali kwenda nyumbani kwa Recho. Mume wake anarudi, simu zangu hazipokelewi, ubwege wa mapenzi umenijaa. Je ntatoboa....
Noma sana!
 
Tuendelee EP 09


Jana nilimalizia kwa kushauri, katika mapenzi mwanamke jitahidi uwe na kitu cha ziada mbali na sex ili uweze kuwin moyo wa mwanaume. Hii ni dhahiri mimi nikiwa mfano hai.


Haikutosha tu kuchezea shanga moja katika kiuno cha Recho, au kusikia na kusoma maneno ya mahaba kutoka kwake kunifanya niwe bwege na ninase mtegoni bali Recho kuhusika moja kwa moja kwenye harakati zangu za kujinasua kimaisha. Tuendelee.


Baada ya kuambiwa pacha wangu yani jamaa angetoka muda wowote kutokea siku hio nikawa napost status kila siku kuulizia. Ndani ya siku tatu toka nianze kuulizia sikuwa najibiwa. Nikiangalia kama ameview status nakuta hajaview. Nikirejea kwenye 'last seen' yake naona alikua online. Kichwa kinazidi kuniuma.


Kwanini Recho ananifanyia maksudi. Nikasema sasa ni muda nijue hatima yangu kwake, maana naona hizi ni dharau zilizojificha kwenye kichaka cha 'tutastukiwa'. Kesho yake mchana nikampigia simu, ikaita kwa muda kidogo kisha ikapokelewa.

Recho " Haloo... nimeona namba Yako nakutumia pesa yako muda si mrefu". Mimi "Hello Recho..Hello!!". Recho akarudia maneno yake ya awali kisha akamalizia kwa ukali "Heh! wewe si nimekwambia nakutumia pesa yako... alaf acha kunipigia pigia simu." Akakata simu.


Wakati wote huo anaongea mimi kimya nikiwa najiuliza. Kwani imekuaje nimekusudia kumpigia Recho badala yake nakosea namba. Mh! Lakini hapana ni yeye. Mbona jina kwenye simu limetokea vile nilivyo msave.


Baada ya Recho kukata simu nikawasha data tena na kupost status kuuliza imekuaje ananiongelesha mambo ya pesa na hajanipa nafasi kunisikiliza. Vilevile haikuwa 'viewed'. Ndani ya dakika 10 akanipigia. " umefanya nini...tulikubaliana nini. Si tulikubaliana tuwasiliane kule WhatsApp?". Mimi "Hivi unajisikia wewe.. we una muda gani hu'view' status zangu". Nikaendelea "tangu juzi nakutafuta na hunirudii".


Recho " Yani umeshindwa hata kujiongeza, me nakwepesha mada badala ukate simu unaendelea kuongea... yani hata hujajiuliza kwanini nilikua nakukalipia...kwani niilishawai kuuongelesha hivo?". " Ndio ujue jamaa bado yupo tena yeye ndio aliniita nije nipokee simu". Mimi "Ok sasa imekuaje umeweza kunipigia kama yupo?. Recho "nimeaga tu naenda dukani ingawa nahisi yupo nyuma ananifatilia".


Mimi " poa, haya kwanini hu'view' status zangu". Recho aliniambia kuwa itakua ali 'mute' status zangu bila kujua na aliahidi angeweka mambo sawa. Tukaagana huku nikasisitiza kichupa kimejaa. "Vumilia tu hata mimi nimekumiss" ndio lilikua neno la kwaheri kutoka kwa Recho.


Ukisikia mapenzi uchizi, upofu, kikohozi, hata wewe msomaji wangu ukitaka ongezea lako mathalani mapenzi ni Lipuli Fc ni sawa tu. Ndio ilivokuwa baada ya maongezi yangu na Recho.


Kesho yake niliomba off kazini na wakanielewa. Nilirudi home pasipo kumjulisha Recho. Kituo changu cha kazi ilikua ni nje kidogo ya mkoa kwahivo niliomba siku mbili. Kinacho nirudisha home sio kuwamiss wazazi au family members hapana, ni Recho. Ndio maana mpenzi msomaji nimekwambia mapenzi yape jina lolote utakaloona linakufaa. Mimi nimechagua mapenzi ni upofu. Huoni unachokifanya mpaka uambiwe na wanao ona.


Baada ya kufika home jioni nikapost. " Nimerudi home one time, Fanya unitumie picha yako nikuone". Akaview chap na akanijibu. "Umerudi!? kwema?!?" ujumbe uliambatana na picha yake.
Mimi "tutaongea kesho kama utapata time".
Recho " Poa, na yeye ametoka ila sijui kama atarudi au atalala huko maana naye haelewekii".


Mimi "kwani kaenda wapi". Recho " Kaitwa makao makuu ghafla sasa sielewi kuna nini na sijui kama atarudi". Alivosema vile niikajua ni mkoa wa jirani tu maana ndio ofisi kuu za mkuu wa kaya zilipo.


Nikamwambia anipigie simu baadae tuongee vizuri. Alifanya hivo na kidogo lile gubu likapoa kiasi. Nikamchana nimerudi kwajili yake na nilikua tayari kufanya chochote ili Mradi nimtie machoni.


Hapo nafikiri unaendelea kunielewa ndugu msomaji kwanini nilisema mapenzi ni upofu. Naweka rehani usalama wangu kwajili ya mtu aliejipata kimaisha. Nasahau kabisa kuna wazazi, ndugu na marafiki wanatarajia kuuendelea kuniona na kufurahi pamoja nami.

Mimi namuona Recho tu. Siwazi kabisa kama kuna mafuta ya nazi, KY na smartphone zinazochukua, kutunza na kusambaza kumbukumbu ndani ya dakika moja.


Kulivopambazuka mapema sana nikamuuliza kama jamaa alirudi na kudai hapana.
Kwa ujinga wangu nikajiona nimepoteza nafasi Jana. What a clear chance. Lakini kuna kitu nilikua najiuliza kuhusu Recho. Nini kinaendelea kichwani/moyoni mwake. Nikajisemea 'anyways' wacha nifosi nibutue kwa mara ya mwisho then ni 'quit'.


Tukakubaliana sikuhio kama jamaa hatarudi basi usiku niende ikiwezekana tuwe na mkesha wa maombi. Kweli saa 12 jioni inafika report inasoma bado bwana mkubwa hajarudi. Saa mbili usiku bado clear. Nikamuuliza Recho "kwanini unsimuulize kama anarudi au lah!". Recho " Z naanzaje...atanichukuliaje... em imagine ni wewe mkewe anakuuliza hivo". Nikamwambia ok sawa itakavokua sawa.


Home nimeshawapanga kuwa nitaondoka saa tatu kuna workmates wangenipitia na usafiri kurejea kazini.
Mpaka saa tano bado nipo home nazuga na sababu kibao. Kwa Recho bado kimya na huku moja haikai mbili haikai.

Nikampigia simu, " Ei vipi mbona kimya hunipendi feedback". Recho "Nilikua naongea nae, anasema anatafuta gari ila akikosa atalala hatokuja". Mimi "sasa si nije tu mamaa.. kwanza sahivi inaenda saa sita gari gani atapata".

Mama wa watu akaona isiwe kesi. " Z njoo ila kwakweli Sina uhakika sana na usalama wetu"..........







Last but not Least.
Mpenzi msomaji wa Uzi wangu huu. Ninayo furaha kukutakia wakati mwema katika sikukuu hizi ( Christmas and Happy New year). Naamini lugha nayo tumia inakupa picha halisi ya Nini kinatokea baina yangu Recho. Sio ya matusi. Tutaendelea baada ya kesho yaani Christmas. Ahsante!
Step by step usiruke kwenye mafuta puliiizzzz 😹
 
Salaam wadau, EPISODE 10A

Imani yangu tumekua na wakati mwema na mzuri tangu tulipo achana juzi. Tumshukuru Mungu.
Basi karibu ufungue box na Episode Moja kuelekea mwisho wa kisa changu na Recho.

Tuendelee;

Nguvu ya dula chini ya shinikizo la ubwege wa mapenzi Z natoa miguu yangu mahali penye usalama zaidi kwangu yani home nakuelekea kwa Recho. Pamoja na kutothibishiwa usalama wangu ama niseme wetu nikawasili getini.

Baada ya kumtaarifu Recho kuwa nipo getini alifika na kunifungulia. "Z umeshindwa kabisa kuvumilia ?". Aliniuliza Recho, Mimi " Recho sielewi ni nini lakini inaniwia vigumu sana kukubali haya maisha". Nikaendelea " nimekumiss sana Mwanamke wangu". Recho " sasa unatakaje na unajua kabisa huyu haeleweki kama nilivokwambia". Mimi " kwanza nina hali mbaya sana hapa...dula haelewi kabisa".

Recho alishusha mkono wake usawa wa suruali yangu ya jinsi kisha akashika pindo la zipu kujiridhisha kama yasemwayo ni kweli.
Kwakweli nilikua na hali mbaya. Recho kwa sauti ya chini na taratibu kana kwamba amelewa " Jamani babaa, mbona amekasirika hivi, haya nisubiri hapa hapa... hatuingii ndani".

Katika hali ile ya uchu wa zinaa kama ndio ingekua arobaini zangu zimetimia hakika sikuwa na bahati. Tena ningenaswa kama kuku bandani. Recho alizima taa za nje na kutoka nje akiwa na kipande cha kikoi.

Aliponifikia sikuwa na sekunde za kupoteza haraka sana kamata kiuno na kuanza kumla mate. Hatua chache kidogo kutoka ngazi za kupanda kivaranda nilishaanza kumpunguza nguo. Recho " jamani jamani Z taratibu basi...hapa chini hapana, tupande kwenye kivaranda hapo". Sikuona sababu ya poteza nishati kujibu badala yake nikatekeleza ushairi wake.

Hapa sasa hakuna cha 'una condom' au lah' ni kukimbiza farasi tu. Usalama wetu ulikuwa chini ya egesho la lock ya komeo la geti pekee. Nilikua kama mnyama mwenye kiu ya maji na kuona chemchem. Sikujali mimi ni swala na nipo eneo la Simba Hapana. Nilijari kukata kiu pekee.

Nikiri ujinga hapa, kweli show za kupanga tukutane tarehe fulani saa fulan, mahali fulani zinakuwa na utofauti na hizi za ku 'ambush'. Huu ni ujinga nimekiri ipo hivo ila haimaanishi mkeo umpige ambush barazani.

Tuendelee, niliunga viwili palepale bila kupoa. Na baada ya hapo ndio tukakumbuka kuna mtu alikua anatafuta usafiri urejee nyumbani kupumzika na mkewe. Chap Recho akajistiri na kile kipande cha kikoi na kuwai ndani huku anakimbia "Mungu wangu simu nimeacha ndani".

Kwangu hali ilikua shwari, naendelea kufuta kijasho baada ya fatiki ndogo ila pevu.

Recho alirejea pale akiwa anaongea na simu, bila shaka ni mumewe. Alipokata simu nikamuuliza kwa shauku "Vipi anakuja?". Recho "Hapana, kasema kesho". Akaendelea "Ila Z utanisababishia matatizo...kumbe alipiga mara nne!!!". Mimi " Nilijua tu hawezi pata usafiri mida hii..achana na hayo, uzuri haji! ". Recho "Nmh! yani wewe kwahio umefurahiii! Haya nambie ume enjoy". Mimi huku uso wangu umechanua kwa tabasam " Hakika, tena hii ya leo nimependa".

Niseme tu arobaini zangu zilikua hazijatimia au tuseme mwenyeziMungu alipanga nivuke hio hatua nijifunze kitu na leo nisimulie hivi.

Usiku ule tulihamishia mchezo uwanja wa nyumbani baada ya simu kuthibitisha jamaa harudi.
Hapa nakukumbusha kitu.

Nilikwambia nyuma kwamba mwanamke akishakuvulia nguo kwa ridhaa au kuridhia automatic amekuweka moyoni. Basi nasisitiza amini tayari amekupa funguo ya chumba katika maisha yake, kazi inabaki kwako kutumia funguo yako kuforce mambo.

Recho alinithibitishia kuwa anapewa kila kitu na mumewe isipokuwa upweke ndio uliokua unamtesa. Sasa mumewe karudi, upweke hakuna tena lakini bado kwa mara nyingine na mlala.

Tuendelee.

Majira ya saa tisa usiku baada ya cc za uji kupungua kama sio kuisha ndio akili zangu Z zinanirudia. "Mungu wangu hivi ningekutwa mimi jana ingekuaje"..."Hapana saa kumi na moja hapa sipo". Nilijiwazia na kujionea huruma mwenyewe.

Sikupata usingizi kabisa na ilipofika saa 10 usiku nikamuamsha Recho. "Ei nataka niondoke". Recho " Heeh! Z usiku wote huu uende wapi, kwanza ni saa ngapi". Mimi "saa 10!". Recho " Hapana angalau saa 11... alaf hujanambia huko ulipo ni kazi gani unafanya".

Baada ya lile swali tukaanza maongeza yenye tija kidogo na muda ukasogea mpaka kumi na moja. Ilipofika nikajiandaa na kiondoka.

Katika harakati za kuondoka kwa Recho nilisahau kofia. Muda kidogo akanipigia. Recho huku alicheka "Babaa yani wewe ni mwizi unaye ogopa kifo...em ijia cap yako isinisababishie majanga mimi". Nikairudia na taratibu kufata njia za panya kuelekea stand nisije kutana na family members nikose cha kujitetea.

Unaweza ukawa unajiuliza ndugu msomaji ni kwanini nilikua bwege kiasi hiko mpaka kurisk maisha yangu vile . Jibu ni rahisi, sikua na mwanamke mwingine mbali na Recho. Tamaa ziligeuka hisia halali za mapenzi, upofu ukanijaa, nikasahau mali ni ya wizi na kujiona nina hisa 100%. Kitu ambacho si ukweli.

Nilirejea salama kazini nikiwa mcheshi na mchangamfu. Hapo umenielewa bila shaka. Mawasiliano na Recho yaliendelea kwa mtindo uleule. Baada ya mwezi kukatika toka jamaa arejee taratibu mambo yalianza kubadilika.
Umeanza kuchana page 😡
Hapo ulifumwa bwana weeh 😹😹
 
Back
Top Bottom