Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 345
- 307
Baba yake ni mjumbe Mkutano mkuu Wilaya, Dada yake Ulega ni katibu Malezi kata kupitia Jumuia ya wazazi na Mtoto wa dada yake ni Katibu wa UVCCM.
Mke wake anautaka Ubunge wa viti maalum Pwani akitokea Mkuranga na tayari ameshachukua fomu.
Yeye Mwenyewe Ulega anautakaa Ubunge wa Mkuranga na leo kachukua fomu.
Wakishinda Ubunge moja kwa moja wanaenda kuwa viongozi katika ngazi ya kamati ya kisiasa na wajumbe wa halmashauri kuu wilaya.
Watakuwa ni mume na mke kwenye baraza la madiwani na hata bungeni.
Kwa vyovyote, watakuwa na sauti pana kwenye ngazi ya jimbo hususan kwenye vikao vya chama na baraza la madiwani, watakuwa na uwezo wa kuinjinia jambo lao lolote hasa kama litakuwa na maslahi kwa familia yao.
Kama unabisha angalia hapa ukienda wilayani unamkuta baba keshajipanga kupitisha hoja za mwanae, ukirudi katani dada mtu yupo, akishindwa anampigia pasi mwanae, unadhani utatokea wapi?.
Mbaya zaidi familia nyingine zisizokuwa katika mfumo itabidi zisubiri sana kunufaika na siasa za Mkuranga maana nguvu watakazokuwa nazo kulinganisha na maisha yetu sisi wakulima ni nadra kushindana nao katika uwanja wa haki.
Ama kweli sisi wengine tuendelee kulima kwa mtindo huu wa kutumia nafasi kidogo kujiwekea mizizi wananchi tuna kaazi ngumu kushika uongozi