Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Matokeo ya boxing yamegawanyila katika makundi makuu matatu ,lakini makundi haya yamegawanyika katika vipengele vingi sana.
Sasa leo tunaenda kujifunza kipengele kimoja baada ya kingine.
1)Unanimous Decision(UD)
Hii ni aina ya ushindi ambapo majaji watatu wote wanampa ushindi bondia mmoja.
Mfano;Jaji A :115-113
Jaji B:114-113
Jaji C:116-113
Mfano pambano la mayweather ft pacquiao , Mayweather alishinda kwa U.D (majaji wote watatu waliamua mshindi ni Mayweather)
2)Majority Decision(MD).
Hii ni aina ya ushindi ambapo majaji wawili kati ya watatu wanampa ushindi bondia mmoja na jaji wa tatu anatoa maamuzi ya sare.
Mfano;Jaji A:115-113
Jaji B:116-112
Jaji C:113-113
Mfano pambano la Mayweather ft Maidana 1 ,Mayweather alishinda kwa M.D pambano lapili akashinda kwa U.D
3)Split Decision (SD).
Hii ni aina ya ushindi ambapo majaji wawili wanampa ushindi bondia mmoja na jaji wa tatu anatoa ushindi kwa bondia aliyebakia.
Mfano;Jaji A :115-113
Jaji B:116-112
Jaji C:113-115
Mfano Timothy Bradley vs Pacquiao June 2012 Bradley alishinda kwa S.D
4)Knockout(K.O).
Hii hutokea pale bondia anapopigwa na kudondoka chini na refaree anamuhesabia mpaka kumi Ili anyanyuke na kuendelea na pambano ,kama atashindwa kunyanyuka katika huo muda hiyo itahesabika kuwa amepigwa kwa K.O
Lakini muda mwingine bondia anaweza kujitahidi kusimama lakini kama ataonekana bado ana mawenge na hajielewi elewi pia itahesabika ni knockout.
Mfano A.j vs Klitshko , A.j alishinda kwa K.O
5)Technical Knockout (T.K.O).
Hii hutokea pale bondia anapopokea kipigo kwa muda mrefu na hawezi kujitetea na dalili zote zikiwa zinaonesha hawezi kuendelea na pambano kwa kuzidiwa kupita kiasi basi refaree atasimamisha pambano muda huo huo bila kuhesabu na huyo bondia atahesabika amepoteza pambano kwa Knockout.
Mfano Mayweather ft Conor Mcgregor
6)Retired Technical Decision (R.T.D).
Hii hutokea mara raundi kumalizika kabla ya kuingia raundi inayofuata ,refaree akiona dalili zote za bondia kutoweza kuendelea na raundi inayofuata basi refaree atamaliza pambano muda huo huo na hii pia itakuwa kama TKO na itajumuishwa kwenye idadi za K.O's za bondia aliyeshinda.
Vilevile R.T.D inaweza kuamuliwa na uamuzi wa daktari kama ataona bondia hana hali nzuri ya kuendelea na pambano.
Pia R.T.D inaweza kutokana na bondia mwenyewe kama atagoma kuendelea na pambano kutokana na kutojiskia vizuri basi refaree atasimamisha pambano na huyo
bondia atakuwa amepigwa kwa K.O.
Mfano Lomachenko vs Rigondeux
7)Disqualification (D.Q).
Hii hutokea pale bondia anapocheza rafu mara kwa mara na kuonywa lakini bado akaendeleza makosa yake yale yale.
Mfano wa makosa ni kama vile kupiga kisogoni,kupiga kwa kutumia kiwiko ,kupiga kwa kutumia kichwa ,miguu nk.
Vilevile bondia huyu atapunguziwa points zake na majaji na atakuwa amepoteza pambano kwa Disqualification (D.Q)
Kama itatokea bondia yupo chini na bondia mwingine anamshambulia hapo hapo chini refaree atasimamisha pambano muda huo huo na huyo bondia atahesabika amepoteza pambano kwa DQ hata kama kwenye Scorecards inaonesha alikuwa anaongoza kwa points.
8)Draw.
Hii hutokea pale majaji watatu wakatoa maamuzi ya sare .
Mfano;Jaji A:113-113
Jaji B:113-113
Jaji C:113-113
Mfano Canelo Alvarez vs GGG
10)Majority Draw.
Hii hutokea pale majaji wawili wanapoamua sare na jaji watatu anampa ushindi bondia mmoja wapo .Hii kwa kawaida huhesabika ni sare.
Mfano;Jaji A:113-113
Jaji B:113-113
Jaji C:114-113
11)No contest (N.C).
Hii hutokea pale bondia anapopata tatizo la ghafla katikati ya mchezo kama vile mkono kuteguka nk.
Hapa kama raundi zitakuwa hazijazidi nne hili pambano litafutwa na hakutakuwa na mshindi hivyo itaitwa (No contest) ila wengine wanaita Technical Draw.
Kama raundi zitakuwa zimezidi nne ,matokeo ya majaji yataamua nani mshindi.