Kila kitu ulichokuwa unafanyiwa wakati wa bf/gf relationship ndio unacho hamishia kwenye ndoa hakuna jipya. Kama mlikuwa mnatembea na watu wengine wakati wa uhusiano wenu wa bf/gf, basi msitegemee mabadiriko mtakapo oana.Manake kuna wengine wanasema labda nikimuoa huyu atatulia au labda nikimlazimisha anioe atatulia , hapana, tabia yake atakuja nayo kwenye ndoa hata kama si mwanzoni mwa ndoa baadae tabia itaendelea.
Kama wote waaminifu katika mahusiano yenu ya bf/gf basi uhaminifu utaendelea kwenye ndoa. Kwani hio tamaa haiwezi kuanza ghafla tu kisa ndoa, toka mwanzo itakuwa ilikuwepo labda uhuru kidogo utakuwa umepungua wa kutoka nje ya ndoa.
Kuhusu watoto, kama wote hamko tayari kuwa na watoto, basi bora msubiri mpaka mtakapo kuwa tayari. Hata kwenye uhusiano wa gf/bf kama mimba ikija mmoja hakuwa tayari lazima uhaminifu utapungua na ukorofi kuanza. Sio kwamba mtoto akija kwenye ndoa mtu anaanza kwenda nje, wako pia wale ambao hawajaolewa wana watoto wanakimbiwa pia. Kwahio swala sio kwenye ndoa tu tatizo watu wengi hawajiandai na mabadiriko ya kuja kwa mtoto kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida na kujumlisha kasumba yetu ya kwamba mwanamke akishazaa ndio kasha fuja. Kama mtu anawazo hayo ni vizuri akakaa mbali na swala mtoto/watoto na amtafute mwenzake ambaye wote watakubaliana kwamba hakuna mtoto/watoto kwenye uhusiano wao . Ni vizuri watu tukaelimishana zaidi kuliko kutumia watoto kama kisingizio cha kutembea nje ya ndoa. Vizuri ni kujiandaa kama wote hamko tayari haina haja ya kuwa na mtoto/watoto.Kama wote mko tayari ni rahisi kushirikiana kwa pamoja na kuweza kudumisha mapenzi yenu.
Kwa wanaolewa kwa kufata tamaa ya pesa haina haja kuwazungumzia kwani kila kibarua lazima ukitolee jasho.