Wadau wa jukwa hili natumaini hamjambo na kwale waliopata na misukosuko ya mafuriko poleni sana.
Nina swali langu hili.
Baada ya kusoma yale yanayoendelea Mbagala Zakhem watu kufanya ngono mchana kweupe na kununua kwa tsh 3000 na watu kupanga foleni kusubiri zamu zao na wengine hufanya wakiwa 20 kwenye chumba kimoja.
Nikaendelea kutafakari madanguro na wadada wanaojiuza na kuweza kupata wateja wa kununua ngono, nikatafakari ubakaji, kungonoka na wanyama au mwanaume mwenzako nimebaki nimechanganyikiwa na kujiuliza hivi ngono ni hitaji la muhimu kama ilivyo chakula ambapo mtu akikosa anaweza kufa? Ni tendo la lazima ambalo mtu hasa huyu mwanaume akilikosa hupungukiwa na kitu mwilini? Ama ni starehe? Au tendo la UPENDO
Nimeshindwa kuelewa, nimepatwa na msongo wa mawazo ghafla.
Hivi nisipokutana na boyfriend ama mume wangu kwa mwezi ama miezi what should I think?
Hivi nyie wanaume hamuwezi kuvumilia mpka mkanunue ngono kwa wauzaji?