Hivi ni akili au matope!


Tausi Mzalendo naomba nishukuru kwa kunijulisha waniheshimu... I am humbled. In blue... bado nasimamia kauli yangu kua; kua house gal haina maana kua feeligs zinakua na utumwa.... Kupenda kuko pale pale bahati mbaya ama nzuri kampenda kijana wa hapo nyumbani kwa huyo kijana. Naweza kubali kua huyo kijana kamvuruga binti sababu tu! Ni mdogo na sidhani kama ana uwezo wa kum support wala kumuoa (kama nilivogusia last para in the first post); kwamba anapomuambia kua aondoke asiwe house gal yeye anampango wa kumsaidia vipi? other wise angekua kijana ana uwezo wa kumlea na kumuoa binti sioni tatizo bado...


I do agree with the principle... Ila naomba unijibu maswali haya:-

  1. Kijana angekua na uwezo kabisa wa kumuoa binti (HG) would it have been still wrong kuingia katika dimbwi la Mapenzi sababu anaishi hapo nyumbani?
  2. Nilijibu kwa vigezo ambavo Wali Mweusi alizungumzia... tone, maneno na maelezo yake ni kana kwamba kosa ni kupendana na huyo binti hali anfadhiliwa na kakake ambae ni Boss wa HG - Hivo basi for instance angempenda binti amtongoze kua atamuoa (kwa nia thabiti kabisa) je bado angekua in the wrong?
  3. In red I do support you na reading btn the lines twapishana badogo sababu ya hapo.... But Hio in beige color je utaifafanua vipi kwa wale wanakutana na kutongozana makazini hadi kuonana.... Will it still be called kuvunja maadili?



I am glad we do agree on the above Tausie.....
 


Shine nakubaliana na wewe kabisa.... Na ndio nilivosema katika my last para of my first post katika hili.... Kwamba yupo faster saaana. Na kakurupuka hajafikiria nini hasa hatma ya hayo maamuzi.
 
Housegirl na kijana mdogo mtu wanapaswa kufunzwa kuhusu kujitambua. Hawaelewi maisha bado, wafundishwe kwamba kufanya ngono kabla ya muda muafaka kuna madhara yake, na wafundishwe kufanya ngono salama, housegirl afundishwe kutambua kuwa wakati wa kazi ni kazi na wakati wa mapenzi ni mapenzi, kijana wa shule aelimishwe kutambua kuwa anatakiwa kujiandaa kwanza kimaisha na kujitegemea sio kupenda vya bure (HG) kwa kaka yake. Hakuna mtu anayeweza kuwazuia watu kufanya mapenzi ila anatakiwa kuwapa elimu ya ngono na kujitambua. Nakumbuka nyumbani HG akija tu Mama alikuwa anamwambia waziwazi tukisikia, ukipata mimba tu unakwenda kwenu sio hapa na hatutajuana tena.
 



Simplicity... hapo ni blue hata mimi nimekataa na kusema kijana anakurupuka.....

Nakubaliana na wewe kabisa in red.
 



Nakubaliana na wewe Cheusie.... Umeongea kweli kabisa.....
 
[/QUOTE]
I am glad we do agree on the above Tausie.....[/QUOTE]
asante


Huu ni utovu wa adabu kabisa na ukosefu wa shukrani.Hivi, huyo HG akiondoka, yeye ndio ataangalia nyumba na watoto?
 
Dogo hana akili, alitakiwa afanye heshima kwenye nyumba ya kaka yake.

Msimfukuze mpeni lecture, asikimbilie kucheza na kitabu cha house maid, wakati cha form four kimemshinda.
 
Inaelekea mkuu unaumizwa na nduguyo kuwa na dada wa kazi, kwani wewe una hisia/uhusiano na huyo dada???! mimi sioni tatizo kwamba anakula dada msaidizi,!! angekuwa anatafuna mkeo hapo tungesema toto halina shukrani ya kulipiwa ada!! Kisha wewe jiulize kama unaheshima kwa huyo dada kwa kumpa majina mengine zaidi ya cheo alichonacho cha kumsaidia mkeo!!! Tunawaita Mabeki sawa! lakini unafikiri wao wangependa kudharauliwa kwa namna hiyo?!?! Kwa jinsi unavyoandika hapa ni kwamba huyo dada hana future! usijidanganye na kumdharau kwani aliyekupa wewe ndiye anaye mpatia riziki yeye. Mimi nina heshima sana kwa dada/kaka zetu wanaofanya shughuli hizo kuliko hao wanaoamua kuuza sura na miili yao kwa sababu maisha magumu. Ulichotakiwa kufanya ni kuongea nao na kuwaambia kuwa jinsi gani ungependa nyumba yako mambo yaende na sio kuwaleta humu na kumwaga chumvi baharini. Hapa bado hatujasikiza their side of the story! inawezekana wewe ndiye usiye mstaarabu!! Inama mkuu ufikiri. Jamaa kachagua dada wa kazi na sio mkeo
 
NB: Kichwa cha habari kimenileta humu nilifikiri pacha wangu Matope kaonekana ;-)
 
Kuwa house girl ni jina tu. Lakini ubinadamu uko pale pale yeye ni mtu na ni mwanamke kama wanawake wengine ana haki yakupendwa na kupenda maana mapenzi ni kitu cha muhimu na cha msingi kwa mtu mzima, mleta maada usichanganye status na basic needs. Love and seX ni basic need ya kila kiumbe kilicho hai , haijalisha mnafanyia kwa kaka au nani tulieni msiwe vipingamizi kwenye mahitaji ya msingi ya kila mtu
 
Naona wengi wanachangia hii mada kwa jazba.Hakuna aliyekataa kuwa huo ni ubinadamu.
Mwanzisha mada anachosema ni ile hali ya kijana ambaye hajajitegemea, anayetegemea wengine, kujiingiza kuharibu taratibu za nyumba ya mfadhili wake. Angeendelea na mapenzi yake kimya kimya bila kuharibu utaratibu isingekuwa ishu.Hivi ungekuwa na mtoto/watoto wadogo halafu siku moja ukute mlezi wao katoroka na kuwatelekeza halafu ugundue nduguyo uneyemfadhili ndiye kafanya hivyo bado ungesema "love na sex ni basic needs"?

Tukiendekeza sana huu ubinadamu katika mjadala huu, tukaacha kuona ishu pana tutajipotosha.
 

Akimtundika mimba anaweza kumtunza au utafurahi kuona kichanga kimetupwa??
 
Nijuavyo hakuna sehemu permanent ya kumpata mwenzi hata we kumbuka wapi ulikutana na huyo mme/mkeo so dogo si ndo kampenda huyo binti no matter ni house girl kwa dogo ndo kafika cha msingi wape semina wote kwa pamoja juu ya madhara yanayoweza kutokea kwa sababu ya kufanya ngono zembe then wache wale mema ya dunia.
 
Niutoto tuu wakikia wataacha tabia hiyo wala usijali....

mtu keshabalehe yuko form four ni mtoto? Ni waharibifu sana hawa! Inatakiwa ukishagundua nyendo zake za kunyatia hosegirl mtimue hapo nyumbani! Rafiki yangu alishafanya hivyo ingawa alikutana na vpingamizi kwa wazazi wake lakini alijieleza kwa undani sana wakamwelewa.Kijana mharibifu aliomba kuishi mahali pengine kwa marafiki, akapata kibarua maisha yakaendelea. Ila kwa kweli vijana aina hii wanaong'ata mikono inayowalisha wapo wengi
 

Sikatai kuwa house girl anazo hisia za kimapenzi, ila kwa nini wanafanya mambo yao hadharani kabisa!Mbona hata sie tulipokuwa kwa wazazi wetu tulikuwa na girlfriends na kwa kweli hayakuwa mambo ya kuwaonesha wazazi, kwa nini ye anioneshe live?Haitoshi wawe na mahusiano, anamshawishi house girl aondoke then what will happen at home?Tunaenda job me na wife, mtoto atabaki na nani?
In short mi naamini kama upo kwa ndugu yako tafuta chako, I mean soma upate kujitegemea, upange gheto lako hapo utakuwa huru kuingiza umtakaye. Ukiwa kwa ndugu yako kuwa na adabu.
After all nshamtimua.
 


Hapo kwenye bold,mimi sina any interest with that girl najiheshimu sana isipokuwa sipendezwi na matendo wanayoyafanya. Can you imagine usiku tumelala wanatoka sitting room kufanya sex?Wapo pia ndugu wengine, sometimes wazazi wantutembelea, do you think its pleasant kweli?

Mkuu, nawaheshimu sana wasaidizi wa nyumbani, kwa sababu kubwa moja!WANAWATUNZA WATOTO WETU TUWAPO MAKAZINI! Hilo jina la Beki tatu nilitoa tu mfano kuwa Comedy hupenda kuwaita hivyo, also to me its not good, ila mimi sikufurahishwa na hilo jambo coz dogo namjua tabia zake, yule dada anamchezea tu isitoshe anao wadem kibao. Mbaya zaidi huyu dada ni yatima, alikuwa anaishi na dadake huko Mkoani. Sijapenda hiyo tabia coz najua 100% anamdanganya mtoto wa watu, na ikitokea dada ana ujauzito we unadhani nani atabeba huo mzigo?

Wakati tukiwa home, alikuwepo house girl, you cant imagine tulikuwa wanaume watano and no one touched her. Tulimheshimu as our own sister na aliolewa na mtu mwingine tena kwa heshima kubwa. Kama we ni baba wa familia hutokivumilia hiki kitu, na kama si baba wa familia na wewe unaishi kwa kakako utaona kama nawaonea. Kiukweli HATA WATOTO WANGU SITOWARUHUSU KUFANYA HUU MCHEZO NDANI KWANGU!Nadhani huu ni mtazamo wangu mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…