Tupo bado tunajipongeza kwa ushindi wetu wa magoli ya kitaalam haswa.
Ile inaitwa total football perfomance.
Dilunga na Chama walikimbia na mpira huku wakipigiana Vibration Pass ambazo hata wapinzani hawakupata nafasi ya kuugusa mpira.
Yaani Chama alianza mpira kwa staili ya Fast Attack kwa kumchomekea harakaharaka Concentration Pass John Boko, naye bila kichelewa akapiga Direct Pass kwa Hassan Dilunga.
Dilunga naye kabla ya kuipokea alisha tazama jinsi Chota Chama anavyoonesha shauku ya kuupokea mpira huku akiwa amesha waangali mabeki na kipa wa Nkana fc walivyo Jiposition,
Kumbuka mbele ya Chama kulikuwa na John Boko naye akikimbia kwa kasi ya Splinting ikitegemea kama Chama atauruka ule mpira wa Dilunga basi yeye autumbukuze tu kirahisi kimiani.
Dulunga akakimbia Spidi kali huku akiibia Jicho kuona ni jinsi gani mabeki na kipa wanavyomlinda na pia ni kwa utayari gani Tim Mate wake walivyo jipanga tayari kuupokea mpira anaoukokota.
Hapo akapiga ile kitu inaitwa The Best Final Touch ambayo wachezaji wengi wanashindwa kuipiga na kuishia kupoteza mpira.
Kumbuka Dilunga alisha mpunguza Beki wa Mwisho lakini akaangalia mbele na kuona hayuko kwenye Right Angle Triangle ya Ku Score.
Hiyo ndio sifa ya mchezaji mzuri ambaye anauwezo wa Kudrive mpira kwa kasi na kuangalia njia kwa wakati mmoja.
Sifa hii anayo pia Cretus Chotta ambaye kabla ya Kureceive mpira anakuwa ameshajua pa kuupeleka.
Hivyo ni kwa Body Language yake, Cretus alimwambia Hassan kuwa ulete hapa mpira na Dilunga hakufanya ajizi zaidi ya kusema Ndio Chotta.
Chotta akauchota kwa Kisigino na kuwahadaa mabeki na kipa wa Adui zake na bila kuangalia kuwa mpira umeelekea wapi akaanza kushangilia maana alikuwa na uhakika wa 100% kuwa hakuna wa kuizuia ile The Deadlly Final Touch Yake ambayo ikaenda Strait Nyavuni mwa lango la Adui.
Huku akiwaacha wapinzani wake wameduwaa.
Kwako Mwalimu Kashasha