Hivi ni jambo gani raia anaweza kufanya akafukuzwa katika nchi yake?

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667
Hivi ni jambo gani kutokana na sheria za nchi raia anaweza kulifanya na akafukuzwa nchini kwake akaishi uhamishoni moja kwa moja au kwa muda wa miaka kadhaa?
Hebu wajuvi tiririkeni hapa...!!
 
Hakuna kitu kama hicho, option iliyobaki ni ile ya kizamani ya kina museven
 
Kufukuzwa haufukuzwi lakini cha moto utakiona. Kwa awamu ya utawala huu ni kuwa makini na kila unachokifanya.
Haijulikani rasmi ni kosa gani linaweza kukupeleka hatiani na adhabu unapimiwa tu kadri wanavyojisikia wao, no law applies.
 
Hivi ni jambo gani kutokana na sheria za nchi raia anaweza kulifanya na akafukuzwa nchini kwake akaishi uhamishoni moja kwa moja au kwa muda wa miaka kadhaa?
Hebu wajuvi tiririkeni hapa...!!
Kuukana uraia kwa kupata uraia was nchi nyingine
 
Chukua uraia wa nchi nyingine, halafu wajulishe watu wa uhamiaji. Dual citizenship hairuhusiwi Tanzania, so itakubidi kuukana uraia mmojawapo, ukane uTanzania.
 
Tofauti na hilo la dual citzenship hakuna jambo lingine?

Zipo case za miaka ya nyuma nimewahi zisikia wakati wa utawala wa JK Nyerere kuwa kuna watu waliwahi fukuzwa wakaishi uhamishoni kwa miaka mingi!
Hao case yao ulikuwaje..?
 
Freyzem - Hawakufukuzwa bali "walitoroka/walikimbia" nchi baada ya kutofautina na Nyerere - e.g. Oscar Kambona.
 
Tofauti na hilo la dual citzenship hakuna jambo lingine?

Zipo case za miaka ya nyuma nimewahi zisikia wakati wa utawala wa JK Nyerere kuwa kuna watu waliwahi fukuzwa wakaishi uhamishoni kwa miaka mingi!
Hao case yao ulikuwaje..?

Sifahamu kuhusu hilo la Nyerere, pengine alifanya kwa utashi wake na nafasi za hao waliofukuzwa.
 
Hivi ni jambo gani kutokana na sheria za nchi raia anaweza kulifanya na akafukuzwa nchini kwake akaishi uhamishoni moja kwa moja au kwa muda wa miaka kadhaa?
Hebu wajuvi tiririkeni hapa...!!
unataka ufukuzwe?
 
Back
Top Bottom