Hivi ni kipi kilipaswa kujengwa kwanza, ni kuinua daraja la Jangwani au kujenga Daraja jipya la Salenda hadi Coco beach?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Baada ya kuona haya mateso makubwa wanayopata wanabchi kwa kufunga barabara inayounganisha jijini Dar na Magomeni ikijirudia Mara kwa Mara kutokana na mvua kunyesha, nimekuwa nikijiuliza hivi hawa watawala wetu walitumia busara kweli kuamua kujenga daraja la kuunganisha Coco beach na Salenda, badala ya kutoa kipaumbele cha kuliinua daraja la Jangwani?

Imekuwa ni kawaida sana kwa siku za karibuni kila mvua inaponyesha, hata kama ni ndogo, tunaambiwa kuwa barabara ya Morogoro, inayounganisha Magomeni na jijini Dar imefungwa

Hebu tujaribu ku-imagine ni madhara kiasi gani yanayopatikana kiuchumi kila barabara hiyo inapofungwa?

Hebu pia tujaribu ku-imagine ni wakazi wangapi wanapata usumbufu wa kutokwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Muhimbili au kwenda waona wapendwa wao waliolazwa katika hospitali hiyo kubwa hapa nchini kutokana na kadhia hiyo?

Lakini kwa kuwa nchi hii hivi sasa tunajua kuwa inaendeshwa kwa "misifa" ya ONE MAN SHOW, kila alitakalo bwana yule ni lazima litekelezwe, bila kwanza kuangalia ni kitu gani cha kutoa kipaumbele kwa muda tulionao

Nina hakika watu maelfu kwa maelfu wanaathirika sana na hii barabara ya Morogoro ya kipande cha daraja la Jangwani kinachounganisha Magomeni na jijini Dar

Pia soma:
1). Magufuli: Tutajenga flyover Salender Bridge
2). Yaliyojiri Uwekaji wa jiwe la msingi Daraja la Selander
3). Wabunge pingeni na kataeni kujengwa kwa Daraja la Juu ya Bahari kutoka Coco Beach to Agakhan

 
Lakini kwa kuwa nchi hii hivi sasa tunajua kuwa inaendeshwa kwa "misifa" kwa ONE MAN SHOW, kila alitakalo bwana yule ni lazima litekelezwe, bila kwanza kuangalia ni kitu gani cha kutoa kipaumbele kwa muda tulionao

Jr[emoji769]
 
Lakini kwa kuwa nchi hii hivi sasa tunajua kuwa inaendeshwa kwa "misifa" kwa ONE MAN SHOW, kila alitakalo bwana yule ni lazima litekelezwe, bila kwanza kuangalia ni kitu gani cha kutoa kipaumbele kwa muda tulionao

Jr[emoji769]
Meya wa Jiji hana mipango!
 
Ni kweli hupangiwi, lakini unaona mateso makubwa wanayopata wananchi wako kwa kuifunga barabara muhimu sana ya Morogoro, Mara kwa Mara?

Dala la kuunganisha Coco beach wanapita matajiri na ma Beberu wahisani wetu.
Jangwani wanapita machinga na wauza nyanya na njegere Kariakoo.

Hapo utapima mwenye we!

Mbona haujauliza Chato Airport uulize na jangwani kipi kilitakiwa kiwe kipaumbele?
 
Tuna miundo mbinu ya hovyo sana Dar tena miaka yote , yaani hapo Jangwani kumeshindikana mara utasikia feasibility study zinatumia bil 50, mara tunasubiri world bank.

Tatizo kubwa hatuna mipango ya maana ya maendeleo, tukangefanya tafiti ya maeneo korofi yote mfano jangwani ,sewage system modernization ya mji wote Dar, Barabara za mwendo kasi phase 2 & 3, tukazichukulia mkopo mara moja kwa pamoja zikajengwa.

Baada ya hapo kinachobaki inakuwa ni kulipa tu loan, shida iko pale mnakaa miaka mitano mkisubiri pesa mpate huku watu wanatabika, au mnakwenda kuchukua mkopo wa jangwani peke yake ,baada hapo mnakaa kusubiri tena tatizo litokee sehemu Fulani hao mnakimbia huku mara kule, very bad.

Chukueni mara moja mikopo jengeni mmalize yote then kaaeni kukusanya pesa mlipe, ndio maana Africa iko hivi, watu wanahamia sehemu fulani wanazaliana ,population inaongezeka, hawana maji au barabara ndio serikali inatoka usingizini kuanza kuplan wakati huo kumekuwa hakuna jinsi wanaishia kubomolea watu majumba yao.

wakati nchi za nje wanapeleka kwanza maji, barabara zinajengwa, umeme unakuwa huko, shule zinajengwa, hospital halafu wana encourage watu wahamie kule, sisi ni opposite kila kitu ni holela sijui tuna nini kichwani. Mnakumbuka Jangwani tumeimba miaka yote, mwendo kasi kelele nyingi tumeishia phase leo 2020, mitaro ndio hivyo tena mvua ikinyesha, 58 yrs ya uhuru hatujui tufanye nini, wapisheni na wengine wajaribu.
 
Naipenda Dar yangu nilipozaliwa na kukulia.

Aliyejenga au aliyechora barabara ya BRT na lile daraja ni HITMAN na hili la kufunga barabara baada kujaa maji pale litatusumbia daima hadi patakapofumuliwa pale na kujenga kwa usahihi bila kuathiri njia ya maji.

Zamani nyuma ya miaka 10 iliyopita tulikuwa tukipita pale mto upo chini ya daraja na kina unakiona. Baada ya BRT kukamilika mto unauona level moja na daraja. Depo ya kupaki UDART kimejengwa eneo siyo sahihi hii yote ni kutupatia hasara endelevu.

Wataalam wa uhandisi wapitie hiyo michoro na kubaini kama kuna kasoro za kiupangaji zirekebishwe haraka.

Mnapopita pale jangwani siku zote kuna kijiko kinatoa mchanga na taka ili kuongeza kina cha mto. Sishawishiki kuamini kwamba hapakuwepo mchanga na taka hapo zamani bali there is something done inapelekea hii hali ya kufungwa barabara kutokea kila mvua inaponyesha.

Vyombo vya uchunguzi vichunguze kwa undani hili jambo. Inawezekana kuna ushauri ulipuuzwa kwa makusudi. Ikumbukwe kuna siku Rais wa wakati huo alipita eneo hilo wakati depo ya UDART inajengwa akaamrisha ujenzi usimame lakini baadae aliruhusu baada ya kugundua utaratibu ulifuatwa. Najiuliza ni kina nani walipitisha hayo maamuzi na kama walishauriwa kinyume na kupuuzia...

Inavyoelekea tunaanza kuizoea hali hii na kuishi nayo kama hewala.

Copy & Paste Kutoka Whatsapp

Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanapenda sifa ndio maana wala hawana mpango na Jangwani. Miradi tunayopenda lazima iwe na hii sifa ......"Daraja la kwa Mtogole ndio Daraja Jembamba zaidi Kusini mwa Afrika"
 
Dala la kuunganisha Coco beach wanapita matajiri na ma Beberu wahisani wetu.
Jangwani wanapita machinga na wauza nyanya na njegere Kariakoo.
Hapo utapima mwenye we!
Mbona haujauliza Chato Airport uulize na jangwani kipi kilitakiwa kiwe kipaumbele?
Kumbe Mkuu impongo hao tunawaita mabeberu pale tunapowaponda, lakini tunapowanyenyekea na wanapotupa misaada, jina lao linabadilika na kuwa wahisani?
 
Wanapenda sifa ndio maana wala hawana mpango na Jangwani. Miradi tunayopenda lazima iwe na hii sifa ......"Daraja la kwa Mtogole ndio Daraja Jembamba zaidi Kusini mwa Afrika"
mkuu mengine yapo malawi kwenye barabara wanaita lake shore ya mzuzu salima,Nkhokhotha mpaka Baraka then Blantyre or Zomba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…