Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
... kama mwanamke mjamzito pindi uchungu umjiapo. Akishazaa papo hapo anasahau na "kumpa tena mumewe" hivyo hivyo hadi anazeeka.Mvua zikiisha nyinyi nyote mnao lalama mtaungana na serikali kusahau daraja la jangwani! Mtaanza tena kipindi cha masika. Mtasahau tena baada ya masika kwisha. Hivyo hivyo mpaka mnazeeka. Au mnahamia chama tawala na kufumbuka macho.
Nashukuru lakini usisahau uchafu unaotupwa mto wa msimbazi na uchimbaji michanga ambapo kunakuwa na mmomonyoko wa mchanga unaoziba.Ni kweli hili daraja ni la miaka mingi sana na halikuwahi kuleta kero kama hizi hapo kabla.
Vipi hizi kero zije baada ya kujenga mwendo kasi na ofisi zake pale?
Kilichofanyika, walipoongeza barabara ya mwendo kasi na kujenga ofisi kuna mkondo umefinywa pale, matokeo yake kutapika kule na si swala la mazingira Boss!
Nijadili nini na mtu unayeandika haya?Vichwa gani wa maana haooo
Au Hao wenye matumbo makubwa wanakaa ofisini
Shida yenu nyiee hamna long term plan
Nyie ni wazee Jenga Leo kesho mnabomoa
Ova
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukitaka kutatua tatizo lazima ujue tatizo. Nawe una tatizo la kutojua tatizo ni nini! Unamlaumu rais na kumuita misifa kwani hapo Jangwani matatizo yameanza leo? yalianza zamani, je, wakati rais Kikwete anabariki mradi wa daraja la Selader hakujua tatizo la jangwani? Kwa nini unamuita rais wa sasa misifa? Kuna wakati mtu una tatizo, jingine lakini unaamua kulilia sababu nyengine.
Halafu sasa, wewe umegeuka kuwa injinia kwa kuomba daraja liinuliwe. Nani amekuonesha kwamba likiinuliwa ndo ufumbuzi. Toa kilio chako uwaachie wataalamu watatue. Siyo kuomba liinuliwe, kwenda wapi? Msimbazi haihitaji ufumbuzi rahisi kiasi hicho. Lazima vichwa vya maana vikae na kuamua. Daraja lilishainuliwa tangu mwaka 1982 mbona leo limefunikwa.
Meya hana nywila za kuingia ofisini. Utamlaumuje?Meya wa Jiji hana mipango!
Tuache ubinafsi, barabara ya nyakanazi to kigoma ndio muhimu zaidi,,jangwani ni makosa ya kujenga namna ile wakati mto mkubwa unapita paleBaada ya kuona haya mateso makubwa wanayopata wanabchi kwa kufunga barabara inayounganisha jijini Dar na Magomeni ikijirudia Mara kwa Mara kutokana na mvua kunyesha, nimekuwa nikijiuliza hivi hawa watawala wetu walitumia busara kweli kuamua kujenga daraja la kuunganisha coco beach na selander, badala ya kutoa kipaumbele cha kuliinua daraja la Jangwani?
Imekuwa ni kawaida sana kwa siku za karibuni kila mvua inaponyesha, hata kama ni ndogo, tunaambiwa kuwa barabara ya Morogoro, inayounganisha Magomeni na jijini Dar imefungwa
Hebu tujaribu ku-imagine ni madhara kiasi gani yanayopatikana kiuchumi kila barabara hiyo inapofungwa?
Hebu pia tujaribu ku-imagine ni wakazi wangapi wanapata usumbufu wa kutokwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Muhimbili au kwenda waona wapendwa wao waliolazwa katika hospitali hiyo kubwa hapa nchini kutokana na kadhia hiyo?
Lakini kwa kuwa nchi hii hivi sasa tunajua kuwa inaendeshwa kwa "misifa" ya ONE MAN SHOW, kila alitakalo bwana yule ni lazima litekelezwe, bila kwanza kuangalia ni kitu gani cha kutoa kipaumbele kwa muda tulionao
Nina hakika watu maelfu kwa maelfu, wanaathirika sana na hii barabara ya Morogoro ya kipande cha daraja la Jangwani kinachounganisha Magomeni na jijini Dar