Hivi ni kosa kisheria kuchangia mada ya kichochezi?

Hivi ni kosa kisheria kuchangia mada ya kichochezi?

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
Nina imani humu Ndani kuna ma guru wa sheria mutanisaidia kUjibu swali husika.
Hivi ni kosa kisheria kuchangia mada kwenye thread ya kichochezi.

Nauliza tu kwasababu kuna kipindi habari zilismbaa watu wajisalimishe kitua cha polisi kati ambao walichangia kwenye moja ya mda ya mbunge mmoja ambayo ilisemekana ni ya kichochezi.

Nitashukuru kwa msaada wenu, Nina watoto wanaonitegemea sitaki kufia jela
 
Kanyaga twende sir usiogope kabisa kutumia uhuru wako wa mawazo utakonda bure

Swissme
 
Mkuu hicho ulichochangia ndio kinachoamua liwe kosa ama sio kosa.Isiwe ukaona watu wanazima moto wewe unabeba dumu la mafuta ya taa na kusaidia kuzima.Ngoja wanazuoni wa sheria waje.Ila kumbuka uchochezi ni ukoko wa ukoloni kwenye fikra za viongozi wa kiafrika.
 
Upo Mkuu? Longtime hujaonekana humu
 
Kuchangia siyo kosa, inategemea na unachochangia...

Kosa ni kuchochea zaidi kuni badala ya kutuliza...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom