Hivi ni kushuka kwa elimu ni uzembe wa watoto?

Mbangubangu

Senior Member
Joined
May 6, 2013
Posts
188
Reaction score
69
Wadau hii me naona inanichosha.Wazazi tunatumia hela nyingi kusomesha watoto tution na gharama kibao za vitabu na vifaa vingine,bado ukija nyumbani ukifanya homework na mtoto ni madudu matupu.Mwandiko na uelewa ni hovyo kabisa.

Naomba ushauri jamani au walimu wa siku hizi wako busy hata watoto kufundishwa kuandika vizuri hamna.
 
Shida siyo waalimu ni maslahi madogo wanayopata. Wanakopwa likizo, mishara duni, mazingira ya kazi duni, n.k. Iambie serikali yako iache mzaha na maisha ya baadae ya watoto wenu na iwathamini waalimu kama kada adimu vinginevyo inamwandaa mwanao kumtawala milele kwa ujinga iliyomlazimisha. Nawashangaa wazazi hamchui hatua zozote za kuitaka serikali yenu iache kufanya siasa kwenye maisha ya wanenu. Amkeni, vinginevyo ni majanga! Je, wajua posho ya mbunge mmoja kwa siku ni mishahara ya miezi mitatu ya mwalimu?
 

mtoto wako anasoma shule ipi? hizi za 'kayumba'? au?
 
Ooyooo wasipo angalia basi elimu kwa walimu basi tuwe na matigemeo ya elimu ya kizuzu na mandondocha kwa sisi vidagaa na wanene watoto wao ni shulie zao za kimataifa na penye miti hakuna wajenzi
 
Walimu wamechoka kunyanyaswa na serikal sasa na wao wameamua kuwa busy na mambo yao hakuna tena somo la hati mashuleni..vipi wabunge wale mishahara minono kwa kaz ya kupiga picha za ngono halafu walimu wanaofanya kaz ya kuelimisha jamii wapewe mishahara midogo?
 
mtoto wako anasoma shule ipi? hizi za 'kayumba'? au?

Ndibalema hata hizi za English Medium waajiri wanawanyanyasa waalimu. Mishahara kidogo allowance hakuna lugha chafu. Mtoto anasoma nussery miaka 4 hajui kusoma. Tena kuna nyingine mtoto la 7 akiandika huwezi kusoma. Serikali na wazazi wawatetee walimu
 

Serikali ikipandisha madaraja ya walimu kila wanapo stahili kupanda, ikilipa madeni ya walimu Elimu taboreshwa, lakini walimu wasipo rejeshewa ari ya kufundisha serikali itapandisha madaraja ya ufaulu kutoka division five mpaka division one hundred huku watoto wakidaiwa wamefaulu ilihali hawajui kusoma na kuandika,
 

Hebu jaribu kuembelea hapa (www.uwezo.net) uone hali halisi ya uwezo wa watoto wetu na kasha tuanze kujadili nini kifanyike
 
Wakuu vijana wapo shule nzuri tu english medium.jina naifadhi kidogo na ipo arusha maeneo ya sakina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…