Siku hizi imekuwa ni kawaida kwa watu wanaoenda kuwapongeza akina mama waliojifungua kutoa SIFA ambazo mimi naona ni KASHFA. Kwa mfano kama ni mtoto wa kiume eti wanasema "umetuletea jambazi" na kama wa kike "umetuletea changudoa, house girl...nk" Hata kama ni utani huu umezidi, inaweza kutokea kweli mtoto akawa hivyo. Hii tabia mimi siipendi, mbona zamani ilikuwa safi maneno ya umetuletea "mchumba, mkwe, mama, bibi dada, nk" yalitawala na yalikuwa mazuri.
Aisee kuna watu wanakupongeza umeleta jambazi? haki nitapigana na mtu mm! na urafiki kwishnei simhitaji ndio nimesikia hapa leo
Halafu unashangaa after sometime mtoto anakuwa Jambazi kweli halafu unaanza ku refer kwa mtu aliyetoa hiyo comment
Unaweza ukaua mtu!!!Mimi nadhani inategemea na wewe ni mtu wa namna gani, labda unaendekeza utani wa kijinga, mimi nimezaa watoto wawili miaka hii mitano iliyopita na sijawahi kusikia mtu aniambie hivyo, na atakae jaribu atanijua vizuri.:A S angry::nono::nono:
Ni utani tu jamani!...Mbona kuna watu humu ndani wanaitana"KICHAA WANGU". are they serious?
Kuna wakati inabidi tuelewe kwamba wazazi wanataniana!
Maana hata mtu akimwita binti yangu MCHUMBA, atakuwa anamvuruga ati, kwanini amwanzishie mambo ya uchumba wakati anatakiwa akikua aanze shule!

Wengine nilisikia wakisema kaleta barmaid!! muhimu mtu unapotamkiwa unakanusha saa hiyo hiyo na kumpa onyo aliyetamka,vinginevyo kweli kinywa huumba.