OHB11
JF-Expert Member
- Jul 16, 2017
- 525
- 1,155
Bila kuchelewa naomba kuingia kwenye mada husika bila kupoteza muda
Hawa mapolisi wa dar baadhi yao wanaroho mbaya na kichwani hamna kitu
Kunandugu yangu mmoja anafanya kazi ya kuendesha bodaboda kuna siku alitoka kwenda kazini kama ilivyo kawaida kama ujuavyo kazi hii huchukua hadi muda wa usiku so mara nyingi huwa wanachelewa kurudi
Kwa bahati mbaya usiku wahuni walivamia nyumbani kwake wakavunja mlango na kuiba assets zilizokuwemo ndani humo ikiwemo tv king’amuzi freezer na vinginevyo
Sasa kati ya vitu vilivyoibiwa kimoja wapo ambacho kilikua king’amuzi kiliuzwa jirani na hapo ila sehemu kilipouzwa walishindwa kuset ili kiweze kuwa hewani so walilazimika kumuita fundi
Kwa bahati nzuri au mbaya fundi aliyeitwa aje kutengeneza ndiyo huyo aliyetengeneza kikiwa kwa muhusika na kama tujuavyo king’amuzi huwa na data zote za mtumiaji halali
jamaa ambaye ndiye fundi alivyoona king’amuzi kile ni cha mshkaj ambaye alimtengenezea mara ya kwanza ikabidi ampigie simu na kumwambia kwamba sehemu flani nimeona king’amuzi chako
So baada ya jamaa kujua kati ya vitu vyake vilivyoibiwa kimeonekana na alikua tayari na rb alienda polisi kureport kwa mara ya pili ili mtuhumiwa akamatwe na kuhojiwa
Jamaa alivyofika polisi,,polisi ambaye ndiye mkuu wa kituo maeneo hayo akamuuliza nani ambaye anahiko king’amuzi jamaa akamtaja ni mama fulani anamiliki lodge na baa flani (jina kwenye mabano) pale mtaani polisi akamjibu mimi huyo mama siwezi kumkamata,,jamaa kwa mshangao na shauku akamuuliza kwanini asikamatwe wakati yeye ndiye nimemkuta na king’amuzi changu na labda naweza pata vitu vyangu kupitia yeye,,polisi akajibu huyo mama mimi ni ndugu yangu ungekua wewe ungemkamata ndugu yako ?
Jamaa akawa hana cha kujibu na kuacha tu vitu alivyotafuta kwa jasho lake vikienda bila msaada
Nawasilisha