Hivi ni kwanini dini za sasa zinafanya watu wajisikie vizuri ila sio wawe wazuri?

Hivi ni kwanini dini za sasa zinafanya watu wajisikie vizuri ila sio wawe wazuri?

Joined
Jun 15, 2019
Posts
83
Reaction score
106
Unajua kwenye muda mchache nilioishi duniani, nimekuja kugundua kuwa madhehebu na dini nyingi za sasa zinafanya watu wajisikie vizuri na sio kuwa watu wema. Maana nikiangalia kwenye nyumba nyingi za ibada, waliojaa wengi si watu wema hata kidogo, wengi ni wale extremely dangerous people . Sisemi kuwa wazuri hawapo, no, wazuri wapo na wao ni wengi pia ila waliochukua nafasi kubwa ni wale wa kusema:

1. "mpende jirani yako kama nafsi yako" huku anatembea na mke wa jirani yako, ana mpango mbaya na jirani yake, hana utu, lugha chafu, tabia mbovu na kadhalika?

2. Atakuambia "tenda wema" ila akitoka hapo anakutafuta akuue.

3. Atakushawishi utoe fungu la kumi huku akikukosea vifungu kutoka kwenye vitabu vya dini mfano malaki ikisema tunamuibia MUNGU kwa kutokutoa fungu la kumi huku yeye anakudhulumu na kukuibia hata kidogo ulichonacho.

Ni kwamba wachuingaji wameshindwa kusema ukweli? ni kwamba watu wametekwa vizuri na shetani? au ni nini haswa?

Kuna kisa kimoja , siku moja nilikosea namba, kuna mtu nilikuwa namtafuta mtu fulani, kwenye kupewa namba, badala ya 06........, aliyenitumia akanitumia 07........, sasa baada ya muda nikatuma message, na mimi nikakosea, badala ya kuandia "wazima huko...." nikaandika "wazika huko....", kilichofuata ni matusi kwanza alafu baadaye nikaanza kuhubiriwa. Nikawa najiuliza maswali mengi sana, ni kwenye haya madhehebu yanafundisha hivi? watu wawe hivi? Niliishia kumuambia tu yule aliyekuwa ananihubiria kama kwenye yesu unayemsema ndiye aliyekufundisha haya unayoniambia, basi mimi simtaki. Maana YESU ninayemjua mimi anafundisha upendo, anafundisha heshima, utu na mengine mazuri, ila huyu wako wa matusi, hapana.

Ni kwamba wachungaji wameshindwa kazi kusema ukweli au ni kwamba shetani anazidi speed? naombeni leo tujadili na kung'amua hili
 
Unafki tu ndani ya jamii za dini, na ni ngumu mtu kufundisha matendo yake, hivyo inamlazimu kufundisha matendo yaliyoandikwa kwenye neo la Mungu!
 
Back
Top Bottom