Hivi ni Kwanini Marekani Hawaulizi Vyeti ?

poison

Member
Joined
Mar 5, 2008
Posts
79
Reaction score
32
Ajabu Marekani ukienda kwenye Interview hawaulizi vyeti kabisa wala copy za vyeti haziko kokote kazini.

Nilipokwenda kwenye interview yangu ya kwanza nilikwenda na vyeti vyangu vya Tanzania nikajua wataka kuangalia na kuhakiki wala hawakuvitaka na nikapata kazi na kila nilipokua naenda ni hivyo hivyo na nimeuliza marafiki zangu wengine waliosomea huku wakasema na wao hakuna mtu anaviangalia wala kuvihitaji

Maana hata ukidanganya kwenye resume/cv kuhusu education hawatajua na kuna wahindi wengi tuu nawafahamu wamepamba kidogo resume zao kwenye education lakini wanafanya kazi tuu kwa miaka kibao ?
 
Kwani vyeti si ni makaratasi tu?wenzetu wanaangalia ufanisi wa kazi!
 
hawakuuliza GPA mkuu... hehehehe!
 
CEO wa Yahoo kashurutishwa kujiuzulu kwa kudai ana degree ambayo hakuwa nayo.

Inategemea na kazi unayotaka kufanya. Ukitaka kwenda kufundisha chuo of course wataangalia na ku verify vyeti.Wenzangunamie wengi pencil pushers hatuna majukumu ya kutosha ku warrant thorough checks hizo.Watu wanaangalia zaidi employment history, criminal records, credit history na sehemu nyingine hata drug test kuliko vyeti.

Marekani work history ni muhimu kuliko vyeti kwa sababu watu wako result oriented. Kwa hiyo kama unasema umefanya kazi hapa na pale chances are watapiga simu ku verify (au employment agency iliyokuunganisha inatakiwa kufanya hivyo).

Habari za vyeti hizo unaweza hata kununua cheti online ukaweka namba za simu za mjomba wako.

Tunarudi kule kule kwenye umuhimu wa practical competence over paper qualification.
 
Well said Kiranga na huo wa Yahoo ni shauri tuu wapinzani waliokuwa hawamtaki walimfuatilia kwa karibu lakini ingeweza kuteleza, wale waliomchagua waliagalia performance yake kama sikosei Paypal

Na nimeuliza swali hili maana hoja za watu wengi Tanzania wanaunganisha ufanisi na vyeti nikawa najiuliza mbona watu huku hawavithamini kama sisi watanzania ? Maana enzi za zamani unaulizwa hata cha JKT utafikiria unaomba kua mgambo
 
hawakuuliza GPA mkuu... hehehehe!

Haha Mkuu Njiwa mimi hiyo GPA nimekuja kujua maana yake huku marekani mimi na elimu yangu ya kuunga si wangenitimua zamani, bongo wanauliza na GPA ? Kazi kweli kweli
 
Haha Mkuu Njiwa mimi hiyo GPA nimekuja kujua maana yake huku marekani mimi na elimu yangu ya kuunga si wangenitimua zamani, bongo wanauliza na GPA ? Kazi kweli kweli

ah! si unawajua wabongo man! wanadhani GPA ndio kila kitu... watu wanadesa vyuoni kwa ajili ya GPA
 


ah! si unawajua wabongo man! wanadhani GPA ndio kila kitu... watu wanadesa vyuoni kwa ajili ya GPA

na kuvua chupi kabisaaaaaaaaaa,,,,,,,degree za chup nazo ,,,,mmmmh
 
unakuta mhasibu ana GPA ya 4.0 bank reconcilliation haiwez!unajiuliza hv kweli vyeti ni vya kwake au kanunua?bongo bwana!
 
Western education is Haram a.k.a Boko Haram...
Wabongo wanathamini sana vyeti, hasa serikalini.
 
duh kwa hiyo ukiweka cv ya mimi mjumbe wa nec haikusaiidii?lol
 
Kwa hiyo kama unasema umefanya kazi hapa na pale chances are watapiga simu ku verify

Habari za vyeti hizo unaweza hata kununua cheti online ukaweka namba za simu za mjomba wako.
Kwenye historia ya ajira huwezi "kuweka namba za simu za mjomba wako"?
 
Kwenye historia ya ajira huwezi "kuweka namba za simu za mjomba wako"?

Unaweza
Lakini utachukua chances kwani wanaweza kupata employment history kwa kutumia sosh kuangalia umefanya kazi wapi na wapi wakitaka.

Kwenye vyeti hamna a central authoritative system.It is a mess. Ndiyo maana diploma mills zina flourish.

Not that they cannot track if determined, lakini mtu unakuja kuomba kazi ya ulinzi kwa nini wajihangaishe na vyeti ikiwa security/criminal records hazina red flags?

Ndiyo maana nikasema inategemea na kazi unayokwenda kufanya. Huwezi kusema unataka kwenda kufundisha Princeton watu hawatataka kuangalia vyeti, watataka mpaka na publication history yako.
 
Nimemkumbuka Rose Mwalusaka sijui, yule aligombea ubunge wa EALA. My proffession I'm politician, my daily bread I'm contractor! Kuna mtu unamuangalia unajiuliza std 7 alifauluje, achia mbali masters!
 
Nimemkumbuka Rose Mwalusaka sijui, yule aligombea ubunge wa EALA. My proffession I'm politician, my daily bread I'm contractor! Kuna mtu unamuangalia unajiuliza std 7 alifauluje, achia mbali masters!
Kwani Rose Mwalusaka alikua na Masters ?
 
kazi gani mkuu hebu funguka? Isijekuwa kubeba mabox, cheti cha nn hasa.
 
Degedege

Haha mkuu hawaulizi cheti chochote kwenye professional work, nilifika kuwa. DW and business Intelligence manager bila kuulizwa cheti , nilianza kama ETL Developer , mkuu hilo sio box na nina rafiki yangu , Chemical Engeener kamaliza bongo hapa ni forenstic expert hawajawahi kukiona
hicho cheti, sembuse GPA

Box hayo ni maneno tuu watu wanasema huko bongo wako watu wengi tuu huku hatujawahi piga boxi wala hatutapiga na hatuna hata hiyo degree ni madiploma tuu
 
Last edited by a moderator:
Naomba kueleweshwa.

Navyofahamu mimi kwa bongo kuna hatua zifuatazo


(1) Unaona kuna kazi imetangazwa
(2) Unaomba kazi hiyo kwa kuandika barua, resume na kuambatisha vivuli vya vyeti vyako
(3) Unaitwa interview

(4) Ukiwa kwenye interview room, kuna baadhi ya waajili wanataka uwaoneshe vyeti vyako original na kuna wengine hawahitaji vyeti vyako.

Kama nimeelewa vizuri maelezo yanayotolewa na wachangiaji wengi ni kwamba huko Marekani hawahitaji hata vile vyeti vivuli vya awali nilivyotaja kwenye hatua namba 2 na badala yake wanategemea zaidi kwenye historia ya kazi ulizofanya. Je uelewa wangu ni sawa?


Na kama ni sawa wanajuaje km mhusika ana au hana elimu inayotakiwa kufanya kazi husika?
 
Huulizwi vyeti au chochote kwa sababu wao wanajali "uungwana wako" na ni "watekelezaji wa sheria".
Unaweza usiulizwe vyeti na kazi ukapewa. Unaweza kusafiri kwenye usafiri wa umma usiulizwe tiketi.
Unaweza kudanganya chochote ukajiona wewe mjanja lakini....Siku wakikukamata, hakuna msalie mtume.

Mfano, ikiwa imeandikwa "Kupanda basi bila tiketi faini ni dola 10,000 au kifungo cha miaka 3, siku wakikukamata hakuna wa kumpa rushwa wala mjomba atakayekutetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…