Hivi ni kwanini nchi za wazungu kila wanapotupa misaada tunawaita wahisani wetu wa maendeleo lakini pale wanapotukosoa tunawaita mabeberu?

msaada huwa hauna masharti(mhisani).

pesa yenye masharti sio msaada(beberu).

hii ni sawa na unakwenda kituo cha watoto yatima,unawapa hela wasimamizi wake kisha uwaambie hutaki wanunulie mchele hizo pesa.kama wana uhitaji na mchele kwa wakati huo wataichukia pesa yako.
 
Hiyo kawaida sana mbona binadamu akiwa hai uitwa mtu na akifa anaitwa marehemu mifano iko mwizi kila jina lina sababu zake watu ubadilishwa majina kutokana na matendo yao.
 
Twawaita wahisani kwa sababu tangu uhuru wamekuwa wakishirikiana na sisi kwenye kutusaidia kwenye miradi ya maendeleo.

Ndo maana tunao NIDA, SIDA, DANIDA , WFP na wengine tunao miaka na miaka.

Hawa wahisani hutupatia fedha za miradi ya maendeleo na huwa si mikopo.

Halafu kuna IMF na World Bank, hawa wapo kutusaidia mikopo na ushauri wa namna ya kuendesha uchumi, ila kwa masharti fulanifulani, kama kupunguza matumizi ya serikali na mengine.

Mabeberu (imperialists) ni makampuni makubwa na taasisi za kimataifa ambayo yapo kwenye nchi hizo na yana uwezo wa kulobby kwenye hizi taasisi na kupenyeza ajenda zao.

Wakifanya hivyo, wote waunganishwa na kuitwa mabeberu.

Mfano ni chama cha CDU ambacho mbunge wake ni mmoja wa wale wanamakati watano walojadili kuhusu fedha za COVID-19.

CDU ni chama kinachorikiana na Chadema.

Hivyo mabeberu yapo kutaka rasilimali, malighafi na vyanzo vingine kutoka Afrika lakini si kwa nia njema bali kwa kupora na kutumia vibaraka wao ambao huziweka rasilimali hizo rehani.

Kwahiyo, Tanzania haina ugomvi na Denmark, wala Sweden, wala Norway, Ujerumani, Uingereza na Marekani.

Ila inaweza kuendeelea kujibu hoja kadha wa kadha zinazotoka kwa wawakilishi wa mabeberu.

Kumbuka nchi wahisani hazijijajibu wala kuongea chochote hadi sasa na hiyo ni kwasababu wote wameonekena mambo waloyafanya baada ya uchaguzi wa mwaka huu.

Hivyo kuna tofauti ya wahisani (mashirika ya maendeleo) na mabeberu (makampuni ya kibepari).
 
ULIONA WAPI HUYOMZUNGU ANATOA MSAADA WA BUREE?? MZUNGU HAJAWAHI TOA MSADAA NA HATO TOA MSAADA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…