Hivi ni kwanini unakubali kuvunja ndoa yako?

Imeandikwa: “ Mungu anachukia kuachana “

Sasa Je ni nani chanzo au aliyesababisha wanandoa kuachana?
 
Hujakutana na wanawake wenye jeuri dharau na viburi.....pesa anayo,elimu anayo...utavumilia kama hauna kitu lakini vinginevyo utaua au utakufa kwa stress
 
Upo sahihi 100%....mtoa mada hajakutana na corporate ladies bado
 
Upo sahihi 100%....mtoa mada hajakutana na corporate ladies bado

Corporate ladies ndio kitu gani. Ndoa ina misingi yake isiyojali elimu wala kipato cha mtu. Hiyo ikifuatwa ndoa inadumu na changamoto zinakuwa za kawaida ingawa kwa mtu mwingine anaweza kuona ni shida kubwa. Issue sio corporate!!! Ukishaiweka ndoa kwenye nguzo ya ucorporate au usomi au utajiri na mali maana yake hujui ndoa ni nini.

Jambo ambalo huenda mleta mada hakutaka kuligusia moja kwa moja ni kuwa ndoa inaweza kulindwa na IMANI ya mtu. Unaamini katika nini na kwa sababu gani unaamini hivyo?

Imani hapa inasimama zaidi katika kuamini MUNGU. Dini nyingi hasa hizi kuu zinaamini kuwa above all kuna Mungu muweza wa yote. Huyo ndio aliyeasisi utaratibu wa ndoa na akaweka kanuni au misingi juu yake. Wanandoa (angalau mmoja wao hata kama sio wote) akifuata utaratibu wa ndoa kama ulivyosisiwa na kuamriwa na Mungu basi ndoa hiyo itapita katika mawimbi lakini haitaanguka! Hili nina uhakika nalo.

Mfano kwa wanaoaminj katika Neno (Bible), limetoa mwongozo (amri) yenye formula hii;

Mume - MPENDE MKEO
Mke - MTII MUMEO

hiyo ni balanced equation. Kila mmoja akitimiza alichoambiwa hapo juu, mawimbi ndani ya ndoa hata yawe makubwa vipi, mnavuka PAMOJA.

Kumbuka, mume kumpenda mke ni AMRI. Ni wajibu. Hiyo ni ama unataka au hutaki. Mpende. Muhudumie. Mtunze. Ukimpenda huwezi kumfanyia uonevu au ukatili. Akikosea kwa sababu unampenda, hutamuadhibu, utamsamehe na kumuelekeza (except uasherati)

Mke ukimtii mume wako suala la kuwa wewe ni corporate au career woman mwenye kipato au mali haliwezi kupata nafasi ya juu kuliko mume wako. Ikitokea kinyume chake basi shida lazima iwepo.

Hiyo equation ina maneno machache lakini iki balance hakuna issue ndani ya ndoa itasumbua.

Overall, kila ndoa iko unique. Na hata Neno limeruhusu kutengana katika mazingira ya lazima sana (uasherati). Lakini Neno linasema Mungu anachukia kutengana. Kila kitu kwa kiasi. Haitaleta maana kuvumilia ikiwa kila jitihada imeshindikana hasa pale ndoa inapokuwa life threatening kwa mmoja wao. Habari za kuchomana moto au visu zinaepukika kwa kutengana.

Upendo haulazimishwi.
 
Kuna tabia zingine ngumu kuzivumilia kuna Wana tabia ngumu yaani hawezi kuishi na mtu
 

Kabla ya kutengana ni vyema wanandoa wameane nafasi yaani watengane kwa mda kila mmoja akae mbali na mwenza wake ikibidi hata mikoa tofauti hii inasaidia kujipanga upya watakapo rudiana na KILA mmoja uona makosa yake.
Ndoa ni kanuni na ukikiuka kanuni ni lzm msuguano utokee
 
Mtoa mada;
ULISHAWAHI KUTOMBEW*? Tena juu kitanda ulichonunua mwenyewe?

#YNWA
 
Mfano umeoa poison women. Mwanamke mwenye mdomo mchafu asiye na aibu, aibu utaiona wewe mbwatukaji, mtukanaji, mwenye roho chafu. Labda uwe Yesu au malaika Ili umudu kuvumilia.
 
Kama umeoa mwanamke mpumbavu utafanyaje
 
MWANAMKE MPUMBAVU HUPIGA KELELE.

Kabla hatujatafuta mchawi wa mahusiano yetu, tunapaswa kujichunguza sisi wenyewe kwanza tupo sawa au tuna shida mahali ila hatujui kama hilo ndilo linatufanya tushindwe kuwa na amani kwenye mahusiano yetu.

Ukiwa kama binti, unaweza usiwe na tabia zingine mbovu unazojua wewe kama vile zinaa ila ukawa na kitu hichi, "kelele/makelele" unashangaa kila baada ya muda fulani mahusiano yako ya urafiki/uchumba yakikaa huwa yanavunjika.

Unaweza ukapata bahati ya kuambiwa shida yako na aliyekuacha, baada ya kukuonya mara nyingi huko nyuma, ama unaweza kuachwa kimya kimya bila kuambiwa shida yako ni nini.

Ukiwa kama mke, unaweza kuharibu ndoa yako kwa sababu hii, "kelele/makelele" kwa mume wako. Hasa ukiwa umeolewa na mwanaume ambaye hajasimama vizuri kwenye imani, na ambaye hajaokoka.

Ni rahisi sana mwanaume kuchoshwa na mke mwenye makelele/kelele, na kutoka nje ya ndoa yake. Sio njia ya kumaliza tatizo ila kwa mwanaume ambaye hajaokoka kwake haiwezi kuwa tabu kufanya hivyo.

Tunaweza kulalamika sana kuhusu waume zetu wanaochelewa sana kurudi nyumbani ila ukweli ni kwamba, kelele zetu ndio zinawafanya waume zetu waone ni heri kuchelewa nyumbani, kuliko kuwahi nyumbani ukakutana na kelele zisizo na mwisho.

Japo kuchelewa nyumbani hakuwezi kuondoa tatizo, wanaume wengi huona njia hiyo inawasaidia wao kuepuka kelele za wake zao. Sasa huko nje huwezi kujua huyu mwanaume anashindia wapi.

Ndio maana wanawake wengi huanza kuhisi vibaya waume zao, kwa kuwaambia wana wanawake wengine nje. Si unajua kusingiziwa kila siku kitu ambacho hukifanyagi huwa inauma na mtu mwingine inaweza kumwathiri. Na kuamua kufanya kweli, hasa kwa yule asiye na hofu ya Mungu ndani yake.

Kelele zisizoisha ndani ya ndoa zinaweza kuharibu kabisa ndoa ile, wawili hawa wanaweza kuonekana kwa nje wapo pamoja ila ukweli humo ndani hawapo pamoja.

Hebu tuangalie maandiko matakatifu yanasemaje kuhusu hili, huenda umepata ukakasi wa hili fundisho kutokana na kichwa cha somo hapo juu.

Rejea: Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.MIT. 9:13 SUV.

Mwanamke yeyote anayepiga sana kelele ni mpumbavu, na ni Mjinga, yaani ana sifa zote mbili, ya upumbavu na ya ujinga. Tena andiko likaongeza mkazo zaidi, HAJUI KITU.

Kwa lugha nyingine mwanamke wa namna hii, huwa mjuaji sana, kila kitu yeye anajua, yupo juu kwa kila kitu, kujishusha kwake ni hakuna. Mume wake hakuna anachoweza kuzungumza akaeleweka, yeye ni anachojua sana ni kelele.

Wanawake wa namna hii, huwa wanakimbilia wapewe haki SAWA, yaani 50 kwa 50, si unakumbuka ni kwa sababu HAWAJUI KITU! Ni andiko limesema hivyo, wanaojua kitu hawezi kupigizana hizo kelele.

Rejea: Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.1 KOR. 11:3 SUV.

Kichwa cha mwanamke ni mwanaume, na sio kichwa cha mwanaume ni mwanamke... huu sio ukabila. Maana kuna watu hawachelewi kusema huo ni ukabila/utamaduni wa watu fulani, hili ni andiko ndani ya Biblia.

Wanawake mtaponya ndoa zenu wenyewe, acheni kelele ndani ya nyumba zenu, ndoa inajengwa kwa hekima ya kiMungu iliyo ndani yako. Si kwa kelele zako ndani ya nyumba.

Rejea: Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. MIT.14:1 SUV.

Wasiosikia, endeleeni kuzibomoa ndoa zenu wenyewe huku mkilalamikia wanaume, utasema wewe hujui tu ninayoyapata, kwani wakati unaolewa naye hukujua hayo. Si hadi kuna watu walikuja kukunasua ukaona wanakufuatilia maisha yako! Basi tulia, acha kelele.

Tena tabia yake mbaya ulikuwa unaiona kwake ukasema Mungu atambadilisha akiwa ndani ya ndoa, kwa hiyo Mungu ameshindwa hiyo kazi? Jibu ni kwamba, ujuaji wako, upumbavu wako, Ujinga wako, na kutokujua kwako ndio kulikuingiza kwenye mahusiano yasiyo yako. Acha kelele.

Turejee kwa Mungu.
Samson Ernest.
+255759808081.
 
Kelele zinaboa. Zinakera ..na ndo mwanzo wa kuchomana mioto na visu mwanamke asiye na staha hamwelkez mumewe kistaarabu anaona Kama wapo sawa hajui Kama yy no Mali ya mumewe. Wanwake achen keleleeer
 
Mi naonaga ndoa tamu tu siku zote, tena zile siku tukiwa na hela ndio utamu unazidi tunaenda live band, tunatoka tunaenda bar nyingine, tunamalizia bar ya tatu, tunarudi home tupo bwaxxx....tukizama ndani ni kufanya tuuuu yani tunashtuka adhana ya saa kumi ndio tunalala.

huo uchungu mnauonaga siku gani kwani
 
Kelele zinaboa. Zinakera ..na ndo mwanzo wa kuchomana mioto na visu mwanamke asiye na staha hamwelkez mumewe kistaarabu anaona Kama wapo sawa hajui Kama yy no Mali ya mumewe. Wanwake achen keleleeer
Wacopy kwenye tamthilia
 
Ila bana wanandoa kuachana siyo poa ingawa Kuna wakati inabidi iwe ivyo ili kulinda amani ya moyo .
 
Tatizo linaanzia kwenye KUOA...

Ukiacha hilo hayo yote utayaepuka,,,ni vijana tu wamekuwa na masikio ya kenge..

Note: kama hauna misimamo inayofanana na mleta uzi,,,Kijana mwenzangu NDOA kwako sio sehemu salama kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…