Hivi ni kweli baadhi ya tabia anazoonesha mjamzito huashiria jinsia ya mtoto

dobolo

Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
47
Reaction score
8
kumekuwapo na njia mbali mbali za kubashiri jinsia ya mtoto alieko ndani ya tumbo la mama mjamzito,baadhi wamekua wakisema eti mimba ikisumbua sana(mjamzito kupata shida mara kwa mara) ujue ni mtoto wa kike, Wengine mjamzito akimchukia mumewe ujue hiyo mimba ni ya mtoto wa kike na mengine mengi.

Tunaomba watalaam wa mambo watujuze.
 
Kuna kaukweli wengi nimewashuhudia ambao mimba zilikua zikiwasumbua wamejifungua watoto wa kike,ila hapo kwenye kumchukia muwewe ni vice versa.
 
Kuna mimba mama anavimba uso sura inaharibika kabisa. W anasema mtoto anaiba sura. Na akizaliwa anakuwa copy ya mama yake
 
Kunakaukweli aisee,,

Hivi hawa wasanii wa mbele mbona nawasikia wakisema anatarajia kuzaa mtoto wa kike,,kwani kunamashine zinaweza ona Jinsia ndani ya tumbo?
 
Ultrasound

Mama mtoto wangu alipoenda hospital kujaribu kuangalia kwenye hiyo Ultrasound dogo aligoma kujulikana.
Madaktari wakamuomba wife ajaribu kuongea na dogo, wife akabembelezaaaa wapi dogo aligoma, tumekuja kujua jinsia ya dogo baada ya kuzaliwa.
Lingine wife alikuwa anakula hatari kipindi cha ujauzito wake, alikuwa mtu wa Soda water sana, na mpenzi wa mboga za majani na dagaa wa Kigoma na Ugali, vyakula hivi ilikuwa karibu kila siku lazima ale, wakati kawaida yake yeye na vyakula hivyo tofauti.
Wamama kwenye suala la mimba tunatakiwa tuwape respect ya hali ya juu kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…