[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Ila tambua hii Ni Jamii.
wale watu wa mtaani kwako,ndugu,majirani, etc
nao wapo Humu.
Jamii Ina kila Aina ya watu,
SI vyema kuwa na chuki/hasira/kisasi na mtu,haya ni maisha.
hahaha utajisikiaje utakapojua/kugundua Genta ndiyo Yule mpenzi wako anayekunyimaga usingizi?
au itakuwaje utakapogunda Genta ni ndugu yako Yule unayempenda SANAA ambaye Ni toka Ni toke.
nikupe kisa kidogo.
Kabla sijaja na hii I'd.kuna I'd fulani nilikuwa naitumia,Nilikuwa mchokozi na mtu wa matusi Sana.
Kuna siku nilimtukana mtu matusi Makali Sanaa na yeye akawa ananitukana matusi Makali,
tukafika mbali zaidi, tukaanza kutukaniana wazazi wetu na viungo vyao+Mambo ya kishoga kwa wazazi wetu.
Bahati mbaya I'd zilikuwa zinatudanganya..nakumbuka Ugomvi ulihamia Hadi Pm.
Mara Paaap siku, Nikawa nahitaji simu ya mshua nitume Email na barua ya kazini kwa Kamishina coz simu Yangu haikuwa na Moto (chaji) (Nilienda home kuwatembelea).
Baada ya kumaliza kazi zangu,nikiwa na peruzi na ku, check Apps za kwenye simu, ghafla nikashtuka kuona,Apps ya Jamiiforums.!nikawa na maswali mengi,ila nikaona Ngoja niingie Aha Hamad!!!!! nikakuta ile I'd AMBAYO nilikuwa natukanana nayo na Mambo mengine Kumbe Ni mzee wangu wa kunizaa KABISA.!
Nilikosa Nguvu na Pozi,na ndani ya Moyo wangu nikapata Maumivu Makali Sanaa coz kumbe nilikuwa nawatukana wazazi (Coz ilifikia extent nikawa naita ile I'd kuwa Ni punga na huwa nampigia mke wake)
ukitazama Ni matusi na laana AMBAYO nilijitengenezea .
ikabidi nimuite mzee na kumuomba Sana radhi na haikuishia Hapo hadi kwa Mama Yangu an ndugu zangu.
na hapo nikaachana na I'd ya mwanzo.
ila nikajiapiza kuwa,
Sitokuja kutukana,kumchukua mtu au kumjibu vibaya yeyote Humu Jf
coz wale wa mtaani na ndugu wa Koo na damu ndiyo Hawa Hawa huwa tupo nao Jamiiforums.
so Haina haja au Maana ya kuwa na chuki kwa Mtu.
Jaribu ku, relax na kupotezea
Mkuu.
na c WEWE hata kwa members wengine Wote
AHSANTE.