Hivi ni kweli Form six wanaanza masomo bila wadogo zao

Hivi ni kweli Form six wanaanza masomo bila wadogo zao

Makiri Unguluma

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2011
Posts
987
Reaction score
335
Jamani kwa mjibu wa ratiba ya shule za sekondari Advanced level wiki hii shule zinafunguliwa. Kwa maana hiyo waliokuwa form five mwaka jana wataanza masomo kidato cha sita. Sijui wengine mnafahamu nini, maana tulizoea miaka mingi ya nyuma form five walikuwa wanatangulia shuleni kujisajili na kuzoea mazingira. Sijasikia form five wakitamkwa popote kwa sasa, je ni kwamba wamekuwa wachache waliofaulu kwa hivyo wizara imeamua kuacha ili ije ichanganye na wa mwaka ujao au walioenda private waliyajua haya mapema wakaamua kusoma wao ili wengine wabaki. Upi ni ukweli maana yakisemwa mtaani yatakuwa si mema maana watakuja watu na busara zao zilizo juu ya ufahamu wa watu wengine nao watasema "sisi tunachapa kazi ninyi mnaleta uchochezi wa kuligawa taifa".
 
selection tayari tembelea sanduku la posta shule zilishaanza kuwapositia .Nina uhakika ninacho kisema maana nimeshudia kwa macho yangu join instructions zikijazwa majina but this time wa mbeya unakuta kapangwa Tanga
 
Afadhali kama wameshatoa selection maana nilishaanza kuingiwa na hofu. Hiyo ya Tanga Mbeya haisumbui
 
je ni kwamba wamekuwa wachache waliofaulu kwa hivyo wizara imeamua kuacha ili ije ichanganye na wa mwaka ujao au walioenda private waliyajua haya mapema wakaamua kusoma wao ili wengine wabaki.".[/QUOTE].

Hii hapa umeongea pumba ndugu yangu
 
mungu awajalie wanaa hizo selection wafanye haraka maana miyo inaumia
 
je ni kwamba wamekuwa wachache waliofaulu kwa hivyo wizara imeamua kuacha ili ije ichanganye na wa mwaka ujao au walioenda private waliyajua haya mapema wakaamua kusoma wao ili wengine wabaki.".
.

Hii hapa umeongea pumba ndugu yangu[/QUOTE]

Watanzania wengi huwa wanafaulu vizuri masomo mengine lakini ufaulu kwenye somo la kiswahili huwa ni tatizo, je huwa inatumika kwenye swali. Kwa mila zetu swali huwa linataka jibu halijawahi kutoa msimamo wa mada. Usizoee kutukana utakuja tukana mkweo
 
Back
Top Bottom