Makiri Unguluma
JF-Expert Member
- Jul 21, 2011
- 987
- 335
Jamani kwa mjibu wa ratiba ya shule za sekondari Advanced level wiki hii shule zinafunguliwa. Kwa maana hiyo waliokuwa form five mwaka jana wataanza masomo kidato cha sita. Sijui wengine mnafahamu nini, maana tulizoea miaka mingi ya nyuma form five walikuwa wanatangulia shuleni kujisajili na kuzoea mazingira. Sijasikia form five wakitamkwa popote kwa sasa, je ni kwamba wamekuwa wachache waliofaulu kwa hivyo wizara imeamua kuacha ili ije ichanganye na wa mwaka ujao au walioenda private waliyajua haya mapema wakaamua kusoma wao ili wengine wabaki. Upi ni ukweli maana yakisemwa mtaani yatakuwa si mema maana watakuja watu na busara zao zilizo juu ya ufahamu wa watu wengine nao watasema "sisi tunachapa kazi ninyi mnaleta uchochezi wa kuligawa taifa".