Hivi ni kweli hawa mawaziri wanakuwa wameagizwa na Rais au wanatudanganya!

Hivi ni kweli hawa mawaziri wanakuwa wameagizwa na Rais au wanatudanganya!

Wanatenda Kwa niaba ya Rais na pia ni namna ya kuonesha utii.

.Bashungwa ndio amezidi.
Uko sawa mkuu!

Tusisahau pia hii kauli ilianza wakati wa utawala wa mwendazake...mwendazake alihakikisha kila mtu anajua kwamba yupo hapo kwa utashi wa Raisi na anaweza kutumbuliwa anytime na kwa hivyo ni wajibu wao ule utii uonekane kwa macho(kupitia matamshi) na vitendo(utekelezaji).

Na ile kauli ya Raisi ametoa fedha....nayo ni humo humo!

It's all about praising the highest office...udhaifu wa katiba na uchawa wa watawala!
 
Sasa mkuu hoja yangu kama kweli ni Kwa niaba ya Rais mbona kama wanapinga tena wao Kwa wao. Yaani Rais anamtuma waziri kufanya shughuli Fulani wakati huo huo waziri mwingine kibaya zaidi hata mkuu wa wilaya au mkoa kuleta agizo tofauti Kwa uongo kwamba naye ametumwa na Rais. Yaani hapo wanatudanganya sisi watawaliwa.
Mfumo ni uleule mkuu, tengenezea tatizo Kisha tatua then utapata sifa za kisiasa kwamba unajali watu na msikivu wa tabaka la chini,kumbe ni ujinga tu.
 
Mwajiri wa watumishi wote wa umma ni rais wa JMT, hivyo viongozi wote wa kuteuliwa na rais, kila wachofanya ni wanafanya kwa niaba ya rais, kwa utaratibu wa the end justify the means, hata fedha, wanaolipa kodi ni wananchi, hivyo fedha za kodi ya kuendesha serikali yetu ni fedha zetu, TRA inazikusanya, baada ya kufika TRA, zinageuka ni fedha za serikali ni fedha za Samia, wateule wa rais kila wakiongea utawasikia Samia kutoa fedha hizi na zile na zinaitwa fedha za Samia!.

Hivyo sii kweli ni fedha za Samia, ni fedha zetu, na hata tukikopa tunaolipa ni sisi!, hao viongozi hawajatumwa na rais ila chochote wanachofanya ni wanafanya kwa niaba ya rais wa JMT.
P
Kiukweli kuna uongo sana mara tunalipa madeni ya watumishi mara tunafanya hiki uongo mtupu
 
Mwisho wa siku Bashe anasema maamuzi ya mwenzie Lukuvi yalikuwa ya kisiasa hii Nchi ngumu sana
Yaani hapo umepiga la penyewe! Kwa sababu hapo ndipo penye kiini Cha KERO ya utendaji usioeleweka wa wateule wa Rais. Wakifanikiwa katika hili serikali yetu itakuwa yenye kuaminika na kutumainika. Ni ajabu nchi yetu inafika mahali hata mkuu wa mkoa anakwenda kinyume na maagizo ya waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom