Hivi ni kweli hawa mawaziri wanakuwa wameagizwa na Rais au wanatudanganya!

Wanatenda Kwa niaba ya Rais na pia ni namna ya kuonesha utii.

.Bashungwa ndio amezidi.
Uko sawa mkuu!

Tusisahau pia hii kauli ilianza wakati wa utawala wa mwendazake...mwendazake alihakikisha kila mtu anajua kwamba yupo hapo kwa utashi wa Raisi na anaweza kutumbuliwa anytime na kwa hivyo ni wajibu wao ule utii uonekane kwa macho(kupitia matamshi) na vitendo(utekelezaji).

Na ile kauli ya Raisi ametoa fedha....nayo ni humo humo!

It's all about praising the highest office...udhaifu wa katiba na uchawa wa watawala!
 
Mfumo ni uleule mkuu, tengenezea tatizo Kisha tatua then utapata sifa za kisiasa kwamba unajali watu na msikivu wa tabaka la chini,kumbe ni ujinga tu.
 
Kiukweli kuna uongo sana mara tunalipa madeni ya watumishi mara tunafanya hiki uongo mtupu
 
Mwisho wa siku Bashe anasema maamuzi ya mwenzie Lukuvi yalikuwa ya kisiasa hii Nchi ngumu sana
Yaani hapo umepiga la penyewe! Kwa sababu hapo ndipo penye kiini Cha KERO ya utendaji usioeleweka wa wateule wa Rais. Wakifanikiwa katika hili serikali yetu itakuwa yenye kuaminika na kutumainika. Ni ajabu nchi yetu inafika mahali hata mkuu wa mkoa anakwenda kinyume na maagizo ya waziri mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…