mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Naomba nianze na baadhi ya vituko wanavyo tufanyia wakenya hawa tunaojiita ndugu zetu wa damu, damu gani?
Wakenya miaka ya 70 tena kupitia radio na televisheni ya taifa waliwai kumkashfu baba wa taifa Nyerere kwa kusema MCHONGA MENO AMESHINDWA KUONGOZA NCHI YAKE.
Wakati Nyerere anatukanwa sisi tulikuwa tunakenua meno eti ndugu zetu. Na siri iliyokuwepo nyuma ya pazia ni kuwa Nyerere alikuwa anakataa upuuzi wao wa kujipendele na ubinafsi kila kitu kiwe kwao.
Miaka ya 1980 ilikuwa kila maali yaani mashuleni, vipindi vya redio, vipindi vya televisheni na mikusanyiko yao yoyote ata wakiwa katika arambee walikuwa wanaanza kwa kusema kitendawili hiki NI NCHI GANI DUNIANI INAVAA VIATU VYA MATAIRI watu wanajibu TANZANIAAA. Najua vijana wa sasa hii kitu hamjui waulizeni baba zenu
Wamekuwa na ubinafsi uliopitiliza hata kusababisha Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki kufa kutokana na ubinafsi, ambapo ilikuwa na nchi 3 tu yaani Tanzania, Kenya na Uganda.
Utashanga yaani makao makuu ya shirika la ndege yalikuwa Kenya, makao makuu ya shirika la usafirishaji mizigo na abiria yalikuwa Kenya, uchumi na uwekezaji vyote viliwekwa Nairobi Kenya. Usimamizi wa fedha za Jumuiya ulikuwa Kenya, Sisi Tanzania tulipewa sehemu tu yakufanyia vikao vya kupitisha upumbavu pale Arusha yaani tulilidhika kusema makao makuu ya Jumuiya yapo Arusha lakini uchumi wote walipeana Kenya na Uganda. Eti ndugu, ndugu ni kufaana na si kufafanana.
Ata Jumuiya ilipovunjika wakenya walivizuia vitu vingi sana ikiwemo ndege ambayo Magufuli juzi alimpongeza yule mzalendo kwa kutorosha japo ndege moja yetu akiwaambia anaipaki vizuri sehemu waliyo mwonyesha aipaki hili waibadirishe rangi. Hawa ni majambazi au ndugu? Mimi sitaki kusema vyote nataka kukaana familia yangu home ila kama huu ujinga ukizidi ninazo data zote nitazitapika.
Hadi sasahivi naandika wakenya wote wamefundishana wawe ndani ya nchi au ugenini wanasema mlima Kilimanjaro upo Kenya, jamani hawa ni ndugu au wahuni? Bila hata ya aibu wanaendelea kusema kuwa Ngorongoro ipo Kenya na Serengeti ipo Kenya, nilipofika Kenya nilitaka kujua kwanini wanafanya huu ujinga nilipo chunguza nikagundua wageni wakija wanawaambia sisi na Tanzania ni ndugu hizi mbuga tunashea pamoja na cha kushangaza ukitoka serengeti kunabarabara unaingia Masai Mara hivyo mtalii anatembezwa kote anaamini.
Hapa Dar kuna kampuni inakusanya kodi kutoka Kenya, jamani inaumiza sana hii, kampuni inakusanya kodi za mabango? mabango ya biashara, ina maana hakuna wazalendo wanaoweza kufaya hii kazi? mara ya mwisho ofisi yao ilikuwa Kigogo kwenye mzunguko, mlenda ndani utawakuta wakenya wakali kama pilipili wanaongea kiswahili chao kibovu. Ndiyo maana makampuni mengi yamejaa kutoka Kenya yapo katika shamba la bibi.
Wakenya wanamakampuni zaidi ya 500 hapa Tanzania na sisi Tanzania tuna makampuni kenya zaidi ya 25. Hivi kweli hapa pana usawa kweli na hawa ni ndugu kweli. Mmemsikia wenyewe Rostam Azizi alivyokuwa analalamika kuwa kuingiza kampuni Kenya ni ngumu mno ila wanandugu hawa kuingiza kampuni bongo ize. Hii ni kama Yesu alivyosema ni rahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi uzima wa milele.
Juzi tu mlisikia wanasema mahindi yetu yanasumu, sasa sijui sasahivi wameyakubari naona tumeyatia maziwa, ndiyo maana wakati wa awamu ya 5 tulichoma vifaranga vyenye sumu kutoka kwa nduguzetu wanaotaka kutumaliza, hawa ni zaidi ya majasusi ni taifa hatari kwa Tanzania na vizazi vijavyo, kama unaipenda nchi yako fanya tafiti na ushee na wengine. Kikulacho ki nguoni mwako.
Nibora kusema Burundi ni ndugu kuliko kusema Kenya ni ndugu, kwa sasa sisi Tanzania tunaye ndugu mmoja tu naye Zimbabwe, Wazungu walisha tugawa tukagawika mpaka dini wametuletea zimetugawa hakuna kitu kimoja hivi ukasema sisi ni wamoja ni vipande vipande kila kitu.
Nawasilisha Mtoto wa mchugaji.