Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Ukifa hujui Kama unekufa una-transform na kuingia katika ulimwengu mwingine.

Uhakika ni kuwa Maisha baada ya kifo yapo Ila yapoje hakuna ajuaye.

Ni ishu ya ku-transformation

Ukifa unajua kama umekufa, mengine sijui
 
Acha kula wala kunywa kwa mwezi mmoja maximum uone kama utaishi. Hapo kwenye swali lako la ni chakula unachokula ama ?Unabaki yule yule tokea siku ulipokuwa conceived. Ina unakua na kuna kipindi kama kafanikiwa kufika uzeeni kunakuwa hakuna cell regeneration ya kasi ukilinganisha na ulipokuwa mtoto.
 
Wanaayansi wote walioleta mageuzi duniani waliamini katika miujiza...
Iwe Newton na alchemy, pythagoras na unajimu hata Einstein in short esoteric knowlegde haikwepeki.
Infact ni kwamba wanasayansi kuamini miujiza haini sababishii na mimi niamini hivyo hivyo.

Kupitia historia tunajua kuna idadi kubwa ya wanasayansi walioamini vitu vingi vya uwongo.

Wapo wanasayansi waliowahi kuamini kwamba yale matuta ya kichwani huashiria tabia ya mtu na kwamba wapo walio amini kua harufu mbaya inasababisha ugonjwa wa kipindupindu.

Hizo ni statistics ambazo zimeonesha wanasayansi waliokua wanaamini vitu ambavyo kwa wakati huo walijua ni ukweli.

Kwa hiyo utagundua mtu kuwa mwana sayansi haimfanyi awe karibu na ukweli katika kila kitu.

Kila kitu kinafanywika kwa mipaka, hiyo ikimaanisha kwamba kwa namna einsten alivyokua mtaalamu kwenye physics haina maana mawazo yake kuhusiana na dini au siasa yakubalike eti kwakua yeye ni bingwa wa relative kwenye physics.

Gwajima anaweza kuwa bora kwenye mahubiri ya kanisani na mimi nikapenda, lakini haina maana nikubaliane naye kwenye mtazamo wake wa kuhusiana na corona
 
Mwezi mmoja kote huko?
 
Umesema wewe ni mwili, mwili ni chakula unachokula protein, vitamin, carbohydrate wewe
ni hivyo vyakula?
Ni kipi kinakufanya uwe na uhakika ni yule yule huku umezaliwa na kilo moja sasa unakilo 60?
Nikipi kinakufanya uamiani mwili wako ndio wewe licha ya mabadiliko ya kila siku ndani ya mwili wako?
 
Tuwekane sawa kwanza..
Ukweli kwako wewe nini?
Na sayansi mawanda yake ni yapi(scope).
 
Sema mbinguni kutakuwa na sehemu kubwa sana ya kuhifadhi vitu vyote vinavyokufa huku duniani mf, watu, miti, ng'ombe, sisimizi, nyoka, mwewe nk.
Hakuna wote tunageuka mbolea hapahapa duniani ili tutumike na vile viumbe tunavyoviacha nyuma vikiendelea na maisha wakati tukifa.
 
Yapo tena ya umilele ndugu. Ila ukitaka kuipenda dunia na mambo yake utaishia sema hayapo. Believe me tengeneza na Mungu kabla hujafa.
Jiulize.
1. Je Mungu yupo?
2. Uchawi upo?
3. Kama haupo basi huviamini vitabu vya dini.
 
Bro utapoteza muda wako, Dunia nzima hakuna mwanadamu ata mmoja anayejua, sio mpagani, sio shekh, sio padre wala mchungaji, wao pia hakuna wanalojua bro, ajuaye ni yule aliyetuleta tu sawa sijui ni Mungu au ni nani katuumba mim pia sijui.

Wengi wanayajua yale yaliyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu na pia hawajui ni nani aliviandika ivyo vitabu.. ni imani tu
 
Umesema wanasayansi waliamini baadhi ya mambo kuwa ni kweli na ikaja baanika sio kweli..
Ni kipimo kipi kinatumika kupima ukweli na uongo?
Kama ni sayansi ni nin mawanda(scope) ya sayansi?
Kwangu mimi naona njia bora ya kujua ukweli ni kupatiwa uthibitisho wa ku-support hayo madai na kujua ni kivipi uthibitisho wa hicho kitu umepatikana.

Hata kwenye sayansi Idea haikubaliwi eti kwasababu imetoka kwa smart people, wanasayansi hawakumuamini darwin kwasababu alikua smart guy na ndio maana hawasemi evolution ni kweli kwasababu darwin kasema ni kweli.

Wanakubali kua evolution ni ya kweli kwasababu uthibitisho uliowekwa mezani una support hoja zake
 
Huo unaosema waliamini wanasayansi kuwa ukweli kumbe ni uongo,
Ni kipimo gani kilithibitisha uongo na ukweli?
Personal experience ndiyo chanzo cha majibu potofu, watu wa zamani asubuhi walivyokua wanaliona jua likichomoza mashariki na jioni kuzamia magharibi hawakuhitaji kufanya research wala kujisumbua na ndio maana wakaamini jua linatembea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…