Ukisoma system ya mwili wa binadamu inavyofanya kazi hakuna roho. System ya mwili ni inafanywa na organs zinazotegemeana .kwa hiyo organs ambazo ni vital zinapofeli au inapofeli ndo system ya mwili inacolapse na mtu anakufa. Vital organs ndo msingi wa maisha ya mwanadamu. Moyo ukifail ndo mwisho maana moyo unasukuma damu kwenda kwa mwili na kwenda kwenye mapafu ili damu isafishwe huko. Damu ndo inabeba nutrients na Oxygen kuufanya mwili uendelee kuishi.
Ndo unavyojiliwaza hivyo au siyo....Lakini unasahau kabisa kwamba kabla ya hapo wewe HUKUWEPO na HUKUJULIKANA KABISA KAMA UTAKUWEPO ghafla ulishtukia tu UPO na UKAWEPO BILA RIDHAA YAKO,hivi huyo aliyekufanya UWEPO akakutengenezea hizo system za kustaajabisha na zinazoshangaza kama hzo na tena kama ulivyosema zinafanya kazi kwa kushirikiana bila kukosea,na baadhi huwa zinafanya kazi bila ridhaa yako ikiwemo MOYO au MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA MWILINI,yan kazi yote hiyo kubwa aliyoifanya awe basi tu amekuleta tu duniani hapa kuja kucheza cheza tu kupoteza muda kisha ufe akuzime tu kama taa usiwake tena? Kwa thamani yote hiyo ya hzo syatems ulizozitaja ipitee kizembe zembe tu ufe tu kama mzoga iwe imeisha eti asikurudishe tena? Kirahisi rahisi tu....Umeishi muda flan hv kisha huyo Mtengenezaji hizo SYSTEMS akaamua kuzi SHOOT DOWN(kufa) bila wewe kupenda,Hivi HUYO kwa ujuzi mkubwa wa kushangaza kama hivyo ashindwe kweli KUKUWASHA (kuhuisha)ILI UWAKE TENA KWA MFUMO MWINGINE bila ridhaa yako?
Kipi kigumu,KUTENGENEZA KISICHOWAHI KUWEPO au kutengeneza KILICHOWAHI KUWEPO?
Kumbuka wewe ulikuwa HAUPO KABISA na hakuna mtu alikuwa anakutaja,umekuja Duniani kupitia STAREHE walioifanya watu wawili kitandani kati ya mwanamke na mwanaume ambapo wewe ndo unawaita baba mwingine unamwita mama.
Starehe hiyo waliifanya lakin pia walikuwa hawajapanga kabisa na hawajui ndo unakuja wewe...NA HUENDA HATA SIKU ILE MIMBA YAKO INATUNGWA KUNA MMOJA KATI YAO HAKUZIPOKEA VIZURI TAARIFA YA MIMBA YA WEWE KUTUNGWA LKN PIA HUENDA WALILAUMIANA KWANINI WEWE UMETUNGWA ILA KWA VILE NI MPANGO WA MUNGU NA SIO RIDHAA YAO NAO WAKAAMUA TU KUPOTEZEA MAANA HAKUNA JINSI, MAMA AKAKUBALI KULEA MIMBA YAKO KWA SHIDA AFU NDO UKAJA WEWE LEO AMBAYE SASA HV UPO hapa JF na simu yako UNASEMA HAKUNA KUFA NA HUYO MUNGU HAYUPO.
Hivi HUYO aliyefanya yote haya bila ridhaa ya wewe na wazazi hivi ukishakufa ashindwe kweli KUKUHUISHA tena wewe ambaye ulikuwa HAUPO KABISA?
Umekuja huku ukiwa dhaifu wa mwili na akili unajinyea,unakojoa popote tu unatoka udenda muda wote,lakini BILA RIDHAA YAKO tena unakuwa mtu mzima unafanya mabalaa ya kuyafanya,unaiba,unazini, unatukana watu,unadhurumu KWA RIDHAA YAKO mwisho YULE YULE alikuekuleta Anakuzima tena BILA RIDHAA YAKO (unakufa),Hivi huyu MUNGU ashindwe kabisa kukufanya uwe hai tena?
Kipi kigumu,KUUMBA KISICHOKUWEPO au KUUMBA KILICHOWAHI KUWEPO?
Unakufa bila ridhaa yako na kisha anakupeleka kulee wasiporudi lakini kufa kwako huko lengo ni wewe kubadili hali kutoka uhai wa Dunia kwenda uhai wa akhera,huko utaambiwa yote yote uliyowahi kuyafanya kwa sababu sasahv kila unachokifanya kipo RECORDED kuanzia unabalekhe/vunja ungo mpk siku ile UNAZIMWA na kisha akutie motoni kwa mabaya au akutie peponi kwa mazuri uliyofanya,Huyu ndo akuache tu ufe afu iwe ndyo basi?
Tuache kujitoa akili ndugu zangu,Hzo akili ulizopewa angepewa hata mbuzi lakini Muumbaji ameamua akupe wewe binadamu,lakini pia ukumbuke huyo aliyekuleta hajakuleta tu hivihivi amekuleta kwa mpango maalum na uje utii sheria zake na ufuate kile alichokuamuru ufanye kwa kutumia mfumo sahihi ambao ni dini SAHIHI,dini ya mitume wote walioletwa na Mungu muumbaji.
Duniani Hujaletwa kuja kupoteza muda na hapa duniani sio mahali pa kuishi alipopanga Mungu,na hata hzo organs hujapewa tu burbure,hzo organs running hours zipo limited na matendo unayoyafanya yote yapo in records.
Dunia ni sehemu ya kufanya Utii ili atakaefanya vzr huo utii basi kuna mahali Mungu ndo ameandaa maisha yasiyoisha.
Hebu jiulize kitu kimoja,kama hii dunia ni sehemu ya kuishi kwanini watu wanakufa,kwanini watu wanakufa katika umri wa uchanga,utoto,ujana na utu uzima?
Kama dunia ni kutafuta maisha kwanini wengine hawayapati,wanaishi kwa shida lakini mbona ukiyapatia hayo maisha pia unakufa?Kwanini ufe?mbona starehe zote duniani ni za kipindi flan tu hv,mbona majonzi.ndo mengi kuliko furaha?
Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni kwamba YUPO ALIYEKUANZISHA NA KUKULETA DUNIANI KWA MUDA bila ridhaa yako ILI UJE UFANYE MITIHANI (MAJARIBU)ufanye UTII kwa ridhaa yako mwenyewe huku kufanya utii Mungu ametoa maelekezo tafuta uysome na uyafuate ili uanze kutii,
Amekupa nyenzo za wewe kufaulu huo utii na kuishinda hiyo mitihani,amekupa Muongozo wa vitabu kwa zamani (Zaburi,Torati,Injili) na sasa ni QURAN,pia akakupa Akili,kusikia,kuona,kunusa,kuonja nk,anakupa muda flani,baada ya muda huo flan HUYO HUYO ATAKUFISHA bila ridhaa yako tena NA ATAKURUDISHA TENA KTK UHAI WA AINA NYINGINE bila ridhaa yako ....Ni vile vile kama kwenye chumba cha mtihani,unapewa kila kitu cha kufanyia mtihani ikiwemo na Muda,ukiskia msimamizi anasema "PENS DOWN" huko ndiyo KUFA kwamba muda umeisha,na muda unaisha bila ridhaa yako tena,kisha sasa ndo sote tutakutana huko kwenye SIKU YA HUKUMU,siku ambayo kila mtu atabeba alichokipanda kwenye uhai wa Duniani.
Wakati wewe unandelea kuuchezea muda lakini ipo siku na wewe kule mbinguni patasemwa kwa ajili yako "Pens down" .....hapo utapangiwa ratiba na watu kwamba wakakufukie wapi na lini tena wakati huo wewe upo kwingine kabisa unapambana na hali yako huko.
Hzi pumzi zisituhadae ndg zangu,hakuna watu wanaoendelea kujilaumu hivi sasa kama wale marehemu wetu tuliowazika,Mtu mwema kwa mazuri anayoyaona huko saizi anajilaumu kwanini amefanya mema machache,na mtu mbaya ndo analia na kusaga meno kumuomba Mungu awarudishe kidoogo warudi Duniani kuja kusawazisha yale yote waliyokosea jambo ambalo abadani haliwezekani.