Sumbi Sanchez
Senior Member
- Apr 16, 2017
- 100
- 355
Sio kosa la jinai. Yaani hutashtakiwa kwa lengo la kupewa adhabu. Isipokuwa yule uliyemuahidi anaweza kufungua mashtaka ya kukudai fidia. Fidia anazoweza kupata ni zile ambazo anaweza kuthibitisha kuwa alipata hasara kutokana na kuamini ahadi yako. Kwa mfano alimlipa MC GaraB kwa ajili ya sendoff, alinunua suti ya gharama, alikulipia ada akiamini utakuwa mke wake n.k.