Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Nipo hapa slim5, Dip (Edu) Thug life - Deathrow college of Education, Bsc How to make fare sexy - Apocalypto Univ, Msc Dating other Men's wives - Ghetto Univ!
Na wala sina pozi, sina swags, na still K'koo - Bunju napekua! Kazi kwenu!
 
humu wapo wanaojua kusoma na kuandika tu, waliishia pale walipojua kusoma na kuandika tu na kuwa na mahaba mazito ya chama cha majambazi wakaajiliwa kwa buk 7 kila siku,kazi yao ni kututoa kwenye mada za msingi kwa kutuletea hoja zao za uharo,
 
Hizi tafiti nyingine bana...hebu weka ushahidi wa posts kadhaa za watu wanaokiri elimu zao na iwe kutoka majukwaa tofauti tofauti!!
 
hahahahaaaa Capitalist M,nimekupenda buuureee
Ndugu yangu yaani ya
humu ndani ukiyafuatilia, utachoka. Yaani;
-Hakuna mwenye vitz, wote wana v8
-Humu JF wote wanapiga bao 5 na kuendelea, sasa haya mabango ya kuongeza
nguvu za kiume ni ya akina nani? Labda wana JF hawahusiki!
-Humu wote wapo dsm, wa Mkiu hayumo humu.
-Humu Jf kila mtu amewahi kupanda ndege au amepanda ndege muda huu.
-Mwenye KIBAMIA humu hayumo, humu kila mtu ana
Tangopori tu. Chezea JF weyee!
-Humu watu tunajua kila kitu, mpaka dawa ya ebola imo humu.

-halafu kinginee, hakuna mla mihogo hata mmoja humu wakati kila siku
tunapanga foleni kwa mama Cha Upepo.
JF iache kama ilivyo.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo nini, mtu akisingizia anacho kitu fulani wakati hana si anaidanganya nafsi
 
Mkuu Umenena Vyema Hebu Angalia Maisha Ya Maprofesa Yalivyo Unakuta MTU NA PROFESA WA UCHUMI HANA KITEGA UCHUMI AU PROFESA WA KILIMO HANA HATTA SHAMBA Ndio Maana Huwa Nasema Ukisoma Sana AKILI ZINARUDI ZINAKUWA KAMA ZA MTOTO

Angalia hata hao wanaofundisha Ujasiliamali, nao hawana kitu, waoga kweli. Ila naamini kuwa kama hujasoma hadi huko juu utajituma kukimbizana na hao
 
Darasa la Tano.., Drop Out... na ni member wa JF pia hivyo nadhani swali lako naweza kulijibu simply kwamba sio kila member humu ana degree
 
Yaani jf nlichogundua kimoja ni kua kuna unemployed na wenye uwezo wa kuwaeka pazuri tu. Ila...
Kuna majungu na ushauri kwa kibinafsi.
Kuna 'thirsty niggas' na waume za watu wanaoenda pm kama vichaa.
Mengine nakaa kimya.
 
Mbona fb member wengi wana ajira tena sekta nyeti na wamesoma udsm?wabongo watu wa kujilisha upepo sana

mkuu unaziamni sana profile za member wa fb?.mi mwenyewe kule nimejiandika nafanya kazi kitengo cha uwekezaji benki kuu ya tanzania,wakati ni mkulima tu wa mboga mboga hapa bonde la mto msimbazi.
 
Shalom wakuu!
Swali hili limekuwa likinitatiza sana tangu miaka 2 iliyopita tangu nilipojiunga na JF,

imekuwa ni kama fashion kwa wanaJF wengi kudeclare elimu zao katika post zao nyingi, ajabu kila mtu anasema sijui alipokuwa chuo mwaka wa pili, mwingine ooh nimejiajiri lakini nina degree yangu, hivi ni kweli wote tumesoma mpaka level hizo? Hakuna hata mwenye diploma au Form4 kabisa? Mbaya zaidi hadi vijana wa BRN wa humu JF naona wameanza taratibu kurithi haka karoho ka kipepo kanakotokana na kutojikubali.

Tubadilike jamani.

Itakuwa hujawahi kunisoma wewe maana mimi mara nyingi nimetaja wazi kiwango changu cha elimu ya kidato cha nne na jinsi nilivyopata zali la mentali kwenda majuu kupiga boksi, na jinsi nilivyopanda ngazi hadi kufikia kuwa rais wa wabeba maboksi.

Pamoja na elimu yangu hiyo ya kidato cha nne, bado wenye shahada zao za chuo kikuu nawakimbiza mbaya.

Kwa hiyo watu tunaowakilisha wasio na shahada tupo na mambo yetu swaaafi kabisa.
 
Shalom wakuu!
Swali hili limekuwa likinitatiza sana tangu miaka 2 iliyopita tangu nilipojiunga na JF,

imekuwa ni kama fashion kwa wanaJF wengi kudeclare elimu zao katika post zao nyingi, ajabu kila mtu anasema sijui alipokuwa chuo mwaka wa pili, mwingine ooh nimejiajiri lakini nina degree yangu, hivi ni kweli wote tumesoma mpaka level hizo? Hakuna hata mwenye diploma au Form4 kabisa? Mbaya zaidi hadi vijana wa BRN wa humu JF naona wameanza taratibu kurithi haka karoho ka kipepo kanakotokana na kutojikubali.

Tubadilike jamani.
Mkuu umesema kweli,ngoja mimi nitangulie kusema sina digirii kama wapo na wengine wafuatie
kujikubari ni muhimu sana bila hivyo binadamu utaishi maisha ya hofu mpaka kufa.
 
Mkuu umesema kweli,ngoja mimi nitangulie kusema sina digirii kama wapo na wengine wafuatie
kujikubari ni muhimu sana bila hivyo binadamu utaishi maisha ya hofu mpaka kufa.

Kwel Mkuu nami sijawahi kusoma hata chuo kwa kilimo,lakini life linaenda ni kujipanga tu
 
Back
Top Bottom