Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Elimu ya darasani na namna inavyombadilisha mhusika hi vitu viwili tofauti. Ni kweli kuwa elimu husaidia kwa asilimia kubwa sana kumfanya mtu awe na mabadiliko chanya na hasi kwa uchache.
Hoja ambayo sana inatawala ni mtu kuwa na elimu halafu anakuwa sawa na asiye na elimu kama hiyo ktk MAWAZO, MATENDO, MAFANIKIO, BUSARA, UPEMBUZI, UJUZI n.k na hata kufikia sisi kusema AMESOMA ILA ELIMU YAKE HAIJAMSAIDIA.
MFANO:
1. kijana aliyemaliza chuo kikuu kuandika C.V ama barua ya kuomha ajira ni kazi
2. Form six ama hata chuo kikuu kuongea lugha ya kikoloni kwa tabu (zama za wazee wetu lugha ilikuwa kigezo na sense of pride)
3. Kijana wa chuo kikuu atokaye familia maskini na apataye mkopo, huyu hasaidii nyumbani kwao ni kuishia Club, wanawake, mashugadadi, pombe na kununua vifaa vya ki elekroniki vya gharama ( smartphones, flat screens, sub woofers etc) wakati wazee wetu enzi wanasoma ilikuwa kukumbuka nyumbani ni first priority
4. Kijana aliyemaliza degree yake (uchumi, sheria, umakanika, umeme, udaktari,) pale apatapo kazi hajui chochote ktk kazi husika ama anajua kwa sehem ndogo sana ukilinganisha na walio chini yake kielimu, anaanza kuelekezwa na CERTIFICATE HOLDER ama DIPLOMA HOLDER..... ilhali huyu alokuja ana elimu kuwazidi waliopo.

Hiyo ni baadhi ya mifano inayoleta kubezwa kwa wenzetu WASOMI

Hapa inaonyesha hata wewe ni msomi!
 
Humu kuna wasio hata na astashahada yoyote ila wana busara, hekima na maarifa, pia kuna wenye astashahada, stashahada, shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, shahada ya uzamivu lakini hawana hekima, busara wala maarifa. Lakini kinyume chake pia ni sahihi.

Elimu ni nin?
 
Shalom wakuu!
Swali hili limekuwa likinitatiza sana tangu miaka 2 iliyopita tangu nilipojiunga na JF,

Imekuwa ni kama fashion kwa wanaJF wengi kudeclare elimu zao katika post zao nyingi, ajabu kila mtu anasema sijui alipokuwa chuo mwaka wa pili, mwingine ooh nimejiajiri lakini nina degree yangu, hivi ni kweli wote tumesoma mpaka level hizo?

Hakuna hata mwenye diploma au Form4 kabisa?

Mbaya zaidi hadi vijana wa BRN wa humu JF naona wameanza taratibu kurithi haka karoho ka kipepo kanakotokana na kutojikubali.

Tubadilike jamani.

wewe ulishawahi kutaja elimu yako humu? au ndiyo kujiskia mnyonge kila unapoona watu wanaccomment? usiogope kijana, humu kuna watu wa kila namna na kila ngazi ya elimu wapo humu kuanzia PhD mpaka sisi tulioishia darasa la saba tukafeli tupo pia tunajichanganya nanyi wasomi! USIJITIE UWOGA BURE!
 
Hapa inaonyesha hata wewe ni msomi!

Mimi si msomi, mimi napenda kujua na kujifunza kila siku ikiwezekana kutoka kwa wahusika..... inapotokea najifunza vitu vinavyopingana sipendi sana kupata kutoka kwa mtu wa tatu bali mhusika.
MFANO:
1. Unapotaka kujifunza yahusuyo CHADEMA, kisha ukaenda LUMUMBA hapo hutapata kujua
2. Unapotaka kujifunza ukristo kisha unaenda kwa IMAN PETRO/MAGEZI (mhadhiri wa kiislam ktk kulingania dini) yeye ndo akufundishe asili, mila, tamaduni, miiko, mbingu, n.k Sidhani kama utapata vionjo vya ukristo. Na upatapo kuujua uislam vyema kisha ukamfata MCH. MTIKILA wewe msaka taarifa ndo utakuwa na matatizo
3. Unapohitaji kujua kiundani na ukweli habari za Tanzania halafu unasoma magazeti, blog za Rwanda....(sina la kuchangia)
Pata taarifa kutoka kwa wahusika
 
Madegreee ya nn kuwa na pesa watakuita wakupe udoctor kama mengiii
 
nna wasiwasi kama ulifanya research ya kutosha kabla hujaingia mitamboni.
Nadhani kama ulikuwa unataka majibu tu basi ushayapata.
Now you know
 
Sio kweli lakini wengi wamesoma, sio rahisi kumkuta mtu amefika lasaba anaendelea kuifurahia jamii forum, bila ya kua na elimu utaikimbia mwenyewe hii forum
 
Ukijiunga jamii forums tu wewe una degree ya u-great thinker sasa kazi inabaki kwako tu kuutendea haki huo u- great thinker
 
Kama utawapima wabongo kwa degree bsi umepotea maana tumeona mpka Professors wanaongea pumba tupu!!!!
 
Back
Top Bottom