Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Mimi sina hiyo degree.Nadhani ni afadhali sina
kuliko kuwa nayo nikaishia kuvuliwa kofia bungeni
nikaanza kuomba mwongozo wa naibu spika.
 
Mimi fundi simu,ila najua kutumia computer! niliishia darasa la 6 huko kijijini kwetu...Ila naipenda j.f balaa..
 
Sio kweli lakini wengi wamesoma, sio rahisi kumkuta mtu amefika lasaba anaendelea kuifurahia jamii forum, bila ya kua na elimu utaikimbia mwenyewe hii forum

Mbona mimi sijakimbia mkuu? Elimu muda mwingine ni ujinga tu, Mchukue Prof ambae yupo Dar, mchukue na kijana toka Mtwara au sehemu yoyote njee ya Dar. Kisha wafungie na Prof kaliakoo weka wigo wanyang'anye mawasiliano, tena kijana wa miaka saba. Wape miaka mitatu kama Prof hamjasafirisha kwenda kuzika sijui. Kama kisukari ndio kitaanza hapo, kama presha itaanzia hapo, muangalie kijana yupo safi na kaishakuwa msaada mkubwa katika familia.. Nina hakika asilimia kubwa wengi wanasomea kuwa wajinga, ndio maana wasomi wote huwa watwana kwa wasio wasomi, na mifano ipo mingi, mmoja ni mwenye team ya Chelsia, bongo sitawataja kwa sababu maalum, hivyo wafikirie wewe mwenyewe ambao hawajasoma na wanaperekewa mpaka vyeti fake..na wasomi wa aina zote..

NB: hakuna Elimu nzuri kama ya kujitambua, Mtu kakaa darasani kwa time table miaka kibao cha ajabu na cha kusikitisha, hajui kwenda na muda hapo kuna Elimu kweli? Tusitaniane jamani!!
 
Kwani kufikiri kunahitaji degree ?, je inteligence mtu ili awe nayo mpaka awe ma digrii ? , halafu nn maana ya digrii .. hivi mzee masumbuko akikupa fact za ukweli na zenye uthibitisho japo hakwenda chuo utasema naye ana degree ?, degree unazaliwA nayo ila ukienda shule unaenda kuishtua tu , every body was born with a certain knowledge and ability hivyo hakuna sababu ya kuzungumzia degreeee
 
Just because you have a degree does not make you more smart than anybody else people won't believe in your degree UNLESS you make money from it and it really doesn't matter wether you have degree or not........ Watu kama Professor Mgaya unajiuliza walikuaje Maprof ni bora niwe hivo hivi kuliko kua na hizo degree zenu as long as am making money nothing matters!
 
Wasio na digrii utaona wanavyoandika, mfano "Alusha-Arusha" , '

Laisi -Raisi

Dalesalama-Dar es salaam

Tupog0- Tupo
 
sawa, una degree?????

Kwa kizungu tunaita "Colleges" not universities, Kwahiyo hizo elimu Veta,NVTC,ni Semi-skilled labour ambao darasani walikuwa wa mwisho mwisho ama wanashika mkia lakini wanajua kuandika.

Usijifariji eti umesoma IFM,CBe,,Ustawi Jamii,VETA ukasema umesoma university!

Hizo ni college tu,Semi skilled,ambapo wakoloni walianzisha kwa watu wanaovhelewa kuelewaa
 
Mbona mimi sijakimbia mkuu? Elimu muda mwingine ni ujinga tu, Mchukue Prof ambae yupo Dar, mchukue na kijana toka Mtwara au sehemu yoyote njee ya Dar. Kisha wafungie na Prof kaliakoo weka wigo wanyang'anye mawasiliano, tena kijana wa miaka saba. Wape miaka mitatu kama Prof hamjasafirisha kwenda kuzika sijui. Kama kisukari ndio kitaanza hapo, kama presha itaanzia hapo, muangalie kijana yupo safi na kaishakuwa msaada mkubwa katika familia.. Nina hakika asilimia kubwa wengi wanasomea kuwa wajinga, ndio maana wasomi wote huwa watwana kwa wasio wasomi, na mifano ipo mingi, mmoja ni mwenye team ya Chelsia, bongo sitawataja kwa sababu maalum, hivyo wafikirie wewe mwenyewe ambao hawajasoma na wanaperekewa mpaka vyeti fake..na wasomi wa aina zote..
sijakuelewa mantiki yako, yaani unamaanisha bora kua huna elimu kuliko kua nayo?

NB: hakuna Elimu nzuri kama ya kujitambua, Mtu kakaa darasani kwa time table miaka kibao cha ajabu na cha kusikitisha, hajui kwenda na muda hapo kuna Elimu kweli? Tusitaniane jamani!!
 
Mmmh! Kuumbe! hadi huyu babu kijana Asprin naye anakadegree yeleuwii! Wacha nami niende shulee...
 
hata mimi nna degree ya humu humu jf na nimejiajiri humuhumu jf...since 2011 si mchezo...
 
Back
Top Bottom