SI KWELI Hivi ni kweli kuwa Kinyonga huwa anajibadili rangi kufanana na kila mazingira?

SI KWELI Hivi ni kweli kuwa Kinyonga huwa anajibadili rangi kufanana na kila mazingira?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu

Uhalisia wa Kinyong kuwa na uwezo wa kujibadili kuendana na kila mazigira upo?

Maana kuna muda kuna watu wanaambiana kabisa "oya wewe unauwezo wa kubadilika na mazingira kama kinyonga''
1783493301035.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na dhana ya muda mrefu kuwa kinyonga hujibadilisha rangi kulingana na mazingira anayokuwepo.

Je, Kinyonga hujibadili rangi na kufanana na kila mazingira anayokuwepo?

Lakini watafiti wa masuala ya wanyama wanabainisha kuwa si kweli kuwa Kinyonga anaweza kujibadilisha na kuwa kila rangi kulingana na mazingira husika.

Utafiti wa mwaka 2025 uliochapishwa na Royal society publishing wenye jina Flap-necked chameleons change colour to match their background wa Tom Major na wenzake unabainisha kuwa;

Jambo la Kinyonga kujibadilisha rangi yake ili kufanana na mazingira yake halijathibitishwa kikamilifu katika majaribio mengi ya kisayansi yaliyofanyika. Utafiti huo unaendelea kubainisha kuwa tafiti zilizopo zinaeleza kuwa kinyonga hujibadilisha rangi kwa ajili ya wasaliano ya kijamii, kudhibiti hali ya joto.

Mtaalamu wa vinasaba vya mageuzi katika Chuo Kikuu che Geneva na mtaalamu wa mabadiliko ya rangi ya ngozi za wanyama Michael Milinkovitch anaeleza kuwa;

Watu huamini kuwa ukimuweka kinyonga kinyonga juu ya ubao wa mchezo wa chess atajificha kwa kuchukua muundo au rangi hiyo, lakini bila shaka hilo si kweli.

Je, kwanini kinyonga hujibadili rangi?

Makala ya National Geographic inaeleza kuwa kinyonga hubadili rangi si kwa ajili ya kuendana na mazingira aliyopo bali ina kazi nyingine nyingi zaidi ya hiyo. Mathalani Kinyonga hufanya hivyo kwa lengo la

Kujificha

Anapokuwa katika hatari

Kuvutia na kukataa wenza

Vinyonga pia hutumia rangi zao kama njia ya kuwasiliana dhidi ya wapenzi wao na kuelezea hisia zao kwa wakati huo za kimapenzi. Madume hutumia mabadiliko ya rangi kama njia ya kutongoza au kuvutia, huku majike wakitumia rangi hizo kutoa majibu ya wazi na kujilinda:

  • Kukubali: Majike hubaki na rangi tulivu ya Kijani-kawia kuashiria utayari.
  • Kukataa: Majike hubadilika kuwa mweusi na kuonesha ukali kama njia ya kuwafukuza madume endapo tayari wameshapandana, jambo ambalo huwasaidia kuepuka shari na usumbufu.
Kudhibiti joto la mwili wake

Kwa mujibu wa mtafiti Devi Stuart-Fox, uwezo wa vinyonga na mijusi wengine kubadilisha rangi hautumiki tu kwa kujificha, kuwasiliana, au kuvutia wenza, bali pia ni mbinu muhimu ya kudhibiti jolto la mwili.

Kwa kuwa wanyama hawa ni ectotherm (hawawezi kuzalisha joto lao wenyewe), wao hutegemea joto la mazingira; hivyo, nyakati za baridi huifanya ngozi yao kuwa nyeusi zaidi ili kufyonza joto la jua kwa haraka na ufanisi.

Uwezo huu ni wa kipekee kwa sababu unaweza kutimiza malengo mengi kwa wakati mmoja, kama vile kumwezesha kinyonga kupata joto huku akiendelea kujificha kwa usalama kwenye mazingira yenye rangi nyeusi ili asionekane na maadui.
Kwahiyo wewe hujawahi kumuona kinyonga? Makuzi yako kama Broiller?
 
Ni kweli, hiyo ni sifa mojawapo ya kinyonga kujilinda na adui
 
Back
Top Bottom