Hivi ni kweli mamilioni ya wapenzi wa Yanga tunashindwa kuichangia timu yetu tuipendayo?

Chrizant Kibogoyo

Senior Member
Joined
Aug 12, 2016
Posts
159
Reaction score
81
Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano umeanza kutuonyesha Watanzania kuwa tunao uwezo wa kujitegemea Kwa kutumia raslimali zetu wenyewe.

Katika siku za karibuni Mfadhili wa Klabu yetu ya Yanga amekuwa akikubwa Na changamoto mbali mbali za kisheria, kiasi cha kushindwa kuendelea kutoa ufadhili Kwa klabu yetu ya Yanga.

Ni ukweli usiopunguka kuwa uongozi umejitahidi sana kutymia raslimali kidogo zilizopatikana kutoka Kwa wadhamini mbali mbali kufanya usajili was wachezaji makini wenye uwezo was kuendelea kutupatia Furaha ya ushindi.

Kukoseka kwa mapato kutoka kwa mfadhili kama ilivyokuwa siku za nyuma kumekuwa na mapungufu ya timu yetu kuanza Ligi Kwa kusuasua kutokana Na wachezaji kukosa ari. Hivi karibuni tumeshuhudia wachezaji waandamizi was Yanga wakionekana mahakama ya Kisutu wakiteta Na aliyekuwa mfadhili wa klabu ya Yanga.

Lakini Yanga ni timu kubwa yenye mamilioni ya wapenzi nchi nzima. Hivi ni kweli uongozi uliopo unashindwa vipi kutumia falsafa Mpya ya "Kujitegemea" inayopigiwa chapuo Na uongozi was Awamu ya Tano Kwa kuwashirikisha mamilioni ya wapenzi wake kuziba pengo LA mapato yaliyokuwa yakitoka Kwa Mfadhili!

Nichukue fursa hii kuuomba uongozi was Yanga kuwa wabunifu, wawazi Na wakweli ili kuweza kufanikiwa kutushirikisha wapenzi kuziba pengo LA mapato yaliyokuwa yakitoka Kwa Mfadhili, ili Furaha yetu mashabiki tuweze kuiendekeza.

Ni i Mani yangu kama uongozi watakuwa wabunifu wapenzi Na mashabiki tutaweza Kupunguza angalau bia,soda,sigara Na mengine kama hayo kwa siku I'll kuichangia timu yetu Kwa lengo LA kuendeleza Furaha yetu ya ushindi.

Ushauri wangu ni kuwa katika hill uongozi was klabu ni lazima uhusishe wataalamu wa fani za "Promotion and Advocacy" ili kuweza kuwafikia, kuwashawishi Na kuwamotisha wapenzi Na Mashabiki kuchangia timu yetu ya Yanga kwa lengo LA kuendeleza Furaha tuipatayo kutokana Na timu yetu kupata ushindi dhidi ya wapinzani.
 
Hili timu bora lishuke daraja tu... maana hamna namna tena.
 
Ushauri mzuri sana mkuu, hakika wakiuzingatia utafaa
 
Kuna shabiki mwenzenu mwingine ana matatizo huko mtwARA
Mkazi wa Mtwara afikishwa mahakamani kwa kumshawishi mwanaume mwenzie wafunge ndoa
fb_img_1505489682753-jpg.589087
 
Siyo kila anayevaa jezi ya Yanga ni shabiki wa Yanga.

Overall, tatizo la ushoga limeshakumba dunia yote hivyo hakuna sababu ya kuchekana bali ni kuombeana kwa Mwenyezi Mungu ili hii tabia chafu iondoke katika jamii yetu.

Kwa upande wa mada hii:
Yanga haipaswi kulia njaa, mashabiki waliopo ni mtaji tosha kabisa wa kuendesha Klabu bila kumtegemea mfadhili mmoja.

Chukua mfano mdogo tu:
Nchi hii ina watu karibu Milioni 50 sasa, endapo tutapata mashabiki wa ukweli kama Makoye Matale wapatao Milioni 5 tu ambao wanaweza kununua hisa za thamani ya Shilingi 10,000, Yanga itapata mtaji wa Shilingi Bilioni 50; Viz. 5,000,000 x 10,000 = 50,000,000,000.

Fedha hii ni zaidi ya mara mbili ya bei ambayo mikia fc wameuza Klabu yao. Aidha, mashabiki hawalazimiki kulipa fedha hiyo mara moja, wanaweza kulipa kidogo kidogo ndani ya mwaka mmoja wawe wamekamilisha hizo Shilingi 10,000 hivyo kila mmoja atakuwa anatoa si zaidi ya Shilingi 840 tu kwa mwezi.

Hesabu hizi hazinganyi, kikichobaki ni Viongozi na Wanachama wa Yanga kuiingiza Klabu katika mfumo wa Hisa haraka iwezekanavyo ili kuondoa kero zinazoikabili timu yetu kwa sasa.
 
imetolewa short code ya kuchangia watu wote mitini sisi wazuri wa kuongea lakini sio vitendo tushozea na kuzoweshwa kupata vitu vizuri bila ya kuingia gharama
 
Kwenye hiyo code tunachangia sana tena sana tu kama hisani.

Mfumo wa hisa unainufaisha Klabu pamoja na mwenye hisa mwenyewe. Uchangiaji kwa njia ya code iliyotolewa ni hisani kama ya Mhe. Manji. Tunahitaji formal ownership ya Yanga yetu.
 
Nimekupata mkuu kwa ilo ila najua ata huko upande wapili wanangojea kununuliwa hisa na tajiri sio kutoa pesa yao mfukoni ndio tatizo letu kuu.

Katika kipindi hiki kigumu nilitegemea hiyo short code ingeonyesha mresho mzuri huku tukiendelea kutafuta mchakato wa kuelekea katika mabadiliko.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma, Fred Minziro alimfanyia vitendo vya ki Juma Nyoso Husein Marsha,aisee Marsha fasta alimtandika kiwiko/ kipepsi Mr Katailya...meno 2 chini na mdomo kupata majeraha makubwa..ikabidi washabiki wajitolee pesa ya matibabu...mhhh ikapatikana kama elfu 4500 hivi ambayo haikufaa chochote...Yanga bhana.
 
imetolewa short code ya kuchangia watu wote mitini sisi wazuri wa kuongea lakini sio vitendo tushozea na kuzoweshwa kupata vitu vizuri bila ya kuingia gharama
Kilichofanyika ni watu wasio na utaalamu wa masuala ya uwekezaji kutoa Short Code kuwataka watu kuchangia kama harusi. Soka ni biashara. Ili kufanikiwa ktk biashara yeyote ni lazima maandalizi ya kutosha yafanyike ikihusisha wataalamu wa fani mbali mbali kama vile wachumi, wanasheria n.k
 
Nimekupata mkuu kwa ilo ila najua ata huko upande wapili wanangojea kununuliwa hisa na tajiri sio kutoa pesa yao mfukoni ndio tatizo letu kuu.

Katika kipindi hiki kigumu nilitegemea hiyo short code ingeonyesha mresho mzuri huku tukiendelea kutafuta mchakato wa kuelekea katika mabadiliko.
Kama hiyo mnayoita Short Code ilitolewa haikutolewa Na watu wenye utaalamu wa Mambo ya uwekezaji. Nahisi waliotoa hiyo Short Code hawakufanikiwa kwa sababu ya kutaka wanayanga wachangie timu kama wafanyavyo ktk harusi.

Kabla uongozi kutoa Short Code ulitakiwa kuandaa nyaraka kama vile mahesabu ya kipindi kilichopita, bajeti ya mipango inayotaka kutekelezwa na makisio ya faida itskayopatikana na kuziweka hadharani ili watu waweze kuelewa nini makusudio ya uongozi.

Soka sio sherehe ya harusi ambapo MTU huchangia kwa mategemeo kuwa naye atakula na kunywa. Soka ni biashara, hivyo knachotakiwa ni watu wawekeze ktk timu yao. Hivyo lazima wahusishwe wataalamu wa biashara wasndae mpango wa biashara utakaowashawishi wapenzi na masjabiki kuwekeza ktk timu yao
 
Siyo kila anayevaa jezi ya Yanga ni shabiki wa Yanga.

Overall, tatizo la ushoga limeshakumba dunia yote hivyo hakuna sababu ya kuchekana bali ni kuombeana kwa Mwenyezi Mungu ili hii tabia chafu iondoke katika jamii yetu.

Kwa upande wa mada hii:
Yanga haipaswi kulia njaa, mashabiki waliopo ni mtaji tosha kabisa wa kuendesha Klabu bila kumtegemea mfadhili mmoja.

Chukua mfano mdogo tu:
Nchi hii ina watu karibu Milioni 50 sasa, endapo tutapata mashabiki wa ukweli kama Makoye Matale wapatao Milioni 5 tu ambao wanaweza kununua hisa za thamani ya Shilingi 10,000, Yanga itapata mtaji wa Shilingi Bilioni 50; Viz. 5,000,000 x 10,000 = 50,000,000,000.

Fedha hii ni zaidi ya mara mbili ya bei ambayo mikia fc wameuza Klabu yao. Aidha, mashabiki hawalazimiki kulipa fedha hiyo mara moja, wanaweza kulipa kidogo kidogo ndani ya mwaka mmoja wawe wamekamilisha hizo Shilingi 10,000 hivyo kila mmoja atakuwa anatoa si zaidi ya Shilingi 840 tu kwa mwezi.

Hesabu hizi hazinganyi, kikichobaki ni Viongozi na Wanachama wa Yanga kuiingiza Klabu katika mfumo wa Hisa haraka iwezekanavyo ili kuondoa kero zinazoikabili timu yetu kwa sasa.

Mkuu, uongozi ukiamua sasa hivi natoa hiyo buku 10, Mimi,wife na wanangu wawili fasta.
 
Kama hiyo mnayoita Short Code ilitolewa haikutolewa Na watu wenye utaalamu wa Mambo ya uwekezaji. Nahisi waliotoa hiyo Short Code hawakufanikiwa kwa sababu ya kutaka wanayanga wachangie timu kama wafanyavyo ktk harusi.

Kabla uongozi kutoa Short Code ulitakiwa kuandaa nyaraka kama vile mahesabu ya kipindi kilichopita, bajeti ya mipango inayotaka kutekelezwa na makisio ya faida itskayopatikana na kuziweka hadharani ili watu waweze kuelewa nini makusudio ya uongozi.

Soka sio sherehe ya harusi ambapo MTU huchangia kwa mategemeo kuwa naye atakula na kunywa. Soka ni biashara, hivyo knachotakiwa ni watu wawekeze ktk timu yao. Hivyo lazima wahusishwe wataalamu wa biashara wasndae mpango wa biashara utakaowashawishi wapenzi na masjabiki kuwekeza ktk timu yao
Mkuu tuko pamoja sana. Sijui kama viongozi wetu hupita hapa JF angalau wasikie kilio cha wapenzi wa Yanga.

Mimi binafsi, kama Yanga wataamua kuingia kwenye mfumo wa hisa, niko tayari kununua hisa za Shilingi 10,000,000 (Milioni Kumi).
 
Hakuna misingi mizuri iliyo wekwa na hizi timu zetu jinsi ya kuchangia..
 
Back
Top Bottom