Hivi ni kweli nampenda au nataka kulipa kisasi?

niaje wana jf, mimi ni kijana wa miaka 28, mnamo mwaka 2002 nilikuwa na mpenzi wangu wa kike alikuwa kamaliza A level na mimi nilikuwa nimemaliza o level na nilikuwa nafanya kazi za vibarua(kazi zisizo na ujuzi).wakati anamaliza shule nilimuahidi nita mnunulia zawadi za sherehe. kwa bahati mbaya sikupata fedha na mawasiliano yalikuwa ni barua kwa wakati huo na sikuweza kumjulisha. matokeo yake ya A level yalipotoka alikuwa amefaulu kwa kupata division 1, baada ya hapo alianza visa na kusema mimi ni bahili na siwezi kupata mwanamke kama nikiendelea hivi. chakushangaza ni kuwa nilikuwa namsaidia hapo mwanzo na bado ninampenda hadi hii leo. kuna siku nilikutana nae(2008) akiwa kamaliza chuo, nilijaribu kumwambia bado nampenda lakini yeye akasema eti wakati ule alikuwa bado mdogo na hakuwa na maamuzi na mimi nataka kumlipizia kisasi, anasema nimpe muda wa kujifikiria. mimi najiuliza ni kweli alikuwa hana maamuzi wakati huo? je amekuwa na jeuri hiyo baada ya yeye kufaulu A level nakuwa na uhakika wa kwenda chuo? na mimi ni kibarua sina muelekeo? mimi sikuwa na nia ya kulipa kisasi
Hamna mapenzi hapo, we check ustaarabu mwingine. hayo ni matatizo tupu!
 
Kama amekataa na anakuambia mambo ya ajabu namna hiyo achana nae,usilazimishe mapenzi wala usiombe kupendwa!!
 
Pole
Mwenzie kasha kutema siku mingi..
Anakuzuga tuu hapo... fuata ushauri wa Gaga
Rudi shule na wewe...
 
Mshukuru Mungu amekwambia ukweli kuliko angekupanga foleni. Hapo inabidi ujue dada ameshampa moyo wake mtu mwingine. Maana kama mlishakuwa wapenzi did you need to approach her again??? Haya mambo ni ya kawaida ni wachache wanaokuwa na mpenzi mmoja maisha. Na ni obvious mapenzi uvunjwa na mmoja wa wapendanao. Kwa hiyo wewe kaka si wa kwanza wala wa mwisho kuachwa. Na alichofanya huyo dada wala si cha hajabu ni maisha tu wala si wa kulaumiwa. Akikubali ombia lako maanake ujue kuna jamaa mwingine anakuwa cheated let her move on with her life na wewe vivo hivyo.
 
niaje wana jf, mimi ni kijana wa miaka 28, mnamo mwaka 2002 nilikuwa na mpenzi wangu wa kike alikuwa kamaliza A level na mimi nilikuwa nimemaliza o level na nilikuwa nafanya kazi za vibarua(kazi zisizo na ujuzi).wakati anamaliza shule nilimuahidi nita mnunulia zawadi za sherehe. kwa bahati mbaya sikupata fedha na mawasiliano yalikuwa ni barua kwa wakati huo na sikuweza kumjulisha. matokeo yake ya A level yalipotoka alikuwa amefaulu kwa kupata division 1, baada ya hapo alianza visa na kusema mimi ni bahili na siwezi kupata mwanamke kama nikiendelea hivi. chakushangaza ni kuwa nilikuwa namsaidia hapo mwanzo na bado ninampenda hadi hii leo. kuna siku nilikutana nae(2008) akiwa kamaliza chuo, nilijaribu kumwambia bado nampenda lakini yeye akasema eti wakati ule alikuwa bado mdogo na hakuwa na maamuzi na mimi nataka kumlipizia kisasi, anasema nimpe muda wa kujifikiria. mimi najiuliza ni kweli alikuwa hana maamuzi wakati huo? je amekuwa na jeuri hiyo baada ya yeye kufaulu A level nakuwa na uhakika wa kwenda chuo? na mimi ni kibarua sina muelekeo? mimi sikuwa na nia ya kulipa kisasi

Mliachana 2002.
Mkatakuta 2008 ukamwambia unampenda akasema umpe muda.
Leo ni katikati ya 2011 na bado unasubiri jibu kwa zaidi ya miaka miwili?
Na wewe umejindeleza kielimu au uliishia form four tuu?
Una kazi?
 
Back
Top Bottom