Hivi ni kweli ofisi ya DPP wamekuwa blacklisted uteuzi wa Ujaji?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Kuna malalamiko yamekuwa yakisambaa kitambo sasa, binafsi kuna siku nilitoka mahakamani nikawa kwenye lunch na mawakili kadhaa, miongoni mwao walikuwepo wa DPP. Nikachomeka, ati mbona kila mkeka wa majaji hatuoni mawakili wa DPP,(niliongea kwa kebehi tu nione mawakili wa serikali tulikua nao pale watasemaje) jamaa waliongea kwa uchungu sana, wanaamini Samia amewablacklist. Tuliwacheka kwelikweli. Nakumbuka kuna mwaka Tundu Lisu aliwahi kuambiwa na magufuli kuwa hatateuliwa ujaji, TL lisema, hata akiteuliwa hatakubali kwasababu ni kazi ya utumwa, ila hawa jamaa wana uchungu kabisa na wanaamini wamekuwa blacklisted.

binafsi, siwaonei huruma, kama ni kweli, wacha tu wasote pengine kuna siku akili zao zitafunguka, wakajua uthamani wao na namna Mungu anavyotaka wafanye kazi. naongea hivi kwasababu zifuatazo:

1. Hii ni ofisi ambayo ccm wameitumia miaka mingi sana kama silaha ya kushindia uchaguzi. kamata kamata na shitakishitaki hawa jamaa wanatumiwa sana kinyume na haki.

2. Tulimwambia yule wakili kwamba, akubali tu kwamba mawakili wa DPP siku zote hutumiwa kama instrument kwa ajili ya wengine kupanda, ila wao wanaachwa palepale hadi uchaguzi mwingine. hivi, mtakuwa ngazi za wengine kufanikiwa hadi lini? na wakifanikiwa hawawakumbuki. .

3. Jifunzeni, SAMIA tangu aingie, ameteua majaji wangapo toka ofisi ya DPP? zero. wala hakuna ukurugenzi, urasi au uchochote, ila tukikutana mahakamani mnavyotukamia utafikiri mnapata chochote. juzi tumetoka mahakamani tunapata lunch sehemu na mmoja wenu, hadi anazuga tumlipie bill, mara zote analalamika ati Samia amewadis hawateui ujaji, awateue ujaji halafu nani awe anatumiwa kama fimbo kuchapia wengine, ninyi si ndio mmeamua kuwa hivyo? mnataka ujaji wa nini wakati matumizi yenu ninyi ni kipigio cha wengine? heshima yenu ndio hiyo.

4. Mwakani ni uchaguzi, fungukeni akili, ifuateni haki, mwogopeni Mungu, msitumiwe, narudia tena msitumiweeee. mjue kuwa, ccm wakiwatumia kama bablish kunyanyasa wapinzani, wakishashinda, watawaweka kwenye dustbin hadi uchaguzi wa 2030 ndio mtakumbukwa tena. mishahara yenu itabaki vilevile, na mtaendelea kudharaulika hivyo hivyo. mnataka hadi malaika ashuke toka mbinguni aje awaambie kuwa ninyi huwa mnatumika tu na hawaoni kama mna faida yeyote zaidi ya hiyo?

Ni hayo tu.
 
Huyo Wakili msomi kutoka Ofisi ya DPP anayetaka alipiwe bill ya Chakula hata akiteuliwa kuwa Jaji ataendekeza rushwa.

Haiwezekani Wakili mzima ushindwe kujilipia chakula cha 15,000 hapo mgahawani/hotelini
 
Profesa Juma ni mbaguzi kuteua majaji kutoka taasisi nyingine wakati yeye mwenyewe asili yake sio Mahakama, asili yake ni madarasani huko, akaokotwa, akaletwa. Leo ndio champion wa ubaguzi pale Mahakama.

Kimsingi, vigezo vya kuwa Jaji ni vya kikatiba, bila kujali mtu katoka wapi. Kuna siku niliwahi kuonya kwamba, kama Rais asipokuwa makini, Mahakama inaweza kugeuka "cult" , yaani kama kijiwe cha wachawi, kama hujuani na mtu akuingize, huingii.

Ilifikia muda Mahakama ikawa kama Jeshi letu zamani, kila Jaji anaandaa mtu wake ampandishe, ukifuatilia majina mengi ni yale ya nani kamjua nani.

Mahakama inahitaji watu wa kada zote, kwa kuwa inaamua mambo ya watu wote. Hivyo itoe wanasheria wanaofanya kazi sekta ya bima, kodi, hifadhi ya jamii, ardhi, na kadhalika, wenye uelewa wa ndani na wa vitendo zaidi ya ule wa Prof. Kanywanyi wa darasani.

Rais asilazimiahwe kutoa watu ndani ya Mahakama, iwe sharti kwamba asilimia kadhaa ya pendekezo la majaji litakaloletwa mbele ya Rais na Tume ya Utumishi wa Mahakama litoke nje ya mahakama. Vinginevyo Mahakama Kuu itajaa mahawara za watu, na marafiki
 
prof tena?
 
prof tena?
Yes......yeye ndiye kingpin wa Judicial Service Commission ambayo ndio inapeleka majina ya wateule wa ujqji kwa Rais. Kuna kipindi JPM aliichana orodha waliyompelekea akateua upya. Majina waliyomjazia yalikuwa ya wajomba, shangazi, rafiki, ndugu, wa watu wa Mahakama, ila mmoja alipenya, Jaji Matma, ndugu wa karibu wa Jaji Mkuu.
 
Tanzania hakuna mahakama bali Majengo yenye jina la Mahakama.
Jaji Mkuu amekuwa bize kujenga majengo, amesahau kujenga mahakama ndani ya majengo hayo anayojenga. Ndiye Jaji Mkuu pekee ambaye hajaandika maamuzi yoyote ya kimapinduzi katika sekta ya sheria.

Anachowazidi majaji wakuu waliopita, ni kuhudhuria hafla za pilau ikulu, kuhudhuria sherehe za kuapishwa hata wakuu wa mikoa ikulu
 
Yes......yeye ndiye kingpin wa Judicial Service Commission ambayo ndio inapeleka majina ya wateule wa ujqji kwa Rais. Kuna kipindi JPM aliichana orodha waliyompelekea akateua upya. Majina waliyomjazia yalikuwa ya wajomba, shangazi, rafiki, ndugu, wa watu wa Mahakama, ila mmoja alipenya, Jaji Matma, ndugu wa karibu wa Jaji Mkuu.
Wacha bana..😳
 
Prof Juma ameiua Mahakama. Saivi Mahakama Mahakimu wanataka kuondoka kila siku.

Yeye amekalia Tehama na Majengo tu hajali kabisa kuhusu misingi ya Mahakama kikatiba na maslahi ya watumishi wa Mhimili huu.

Saivi Mahakama inachezewa tu na wanasiasa.
Shida nyingine Wanasiasa wamejaza watu wengi ambao wametoka nje ya mfumo wa Mahakama ambao hawajui misingi ya kikatiba kubusu Mahakama.

Kwenye nchi zilizoendelea Mahakama ndo Mhimili unaowafunga speed governor wanasiasa na watawala. Na Wanasiasa na Watawala wanauogopa kweli Mhimili wa Mahakama maana wanajua huo ndo mhimili unaowawekea mipaka na kuweza kuwapeleka jela pale watakapokosea.

Kuhusu Mawakili wa DPP kutoteuliwa kuws Majaji sioni kama ni tatizo kubwa. Moja ya Mambo yaliyosababisha hadi morali ya ka,I kupungua kwa watumishi wa Mahakama ni kupata viongozi waliotoka nje ya mfumo wa Mahakama ambao hawajui shida zao.

Kwa kipindi kirefu sana Majaji Wakuu wamekuwa wakitoka nje ya mfumo wa Mahakama hivyo hawajali shida za Mahakamu na watumishi wa chini. Majaji Wakuu ambao walitoka nje ya mfumo wa Mahakama na wakajali maslahi ya watumishi wa chini ni Samata na Ramadhani tu. Wengine hawa wamekuwa puppets wa Serikali ambao wame frustrate sana watumishi wa Mahakama.
 
sasa pamoja na mahasira yenu uko ndani mwenu msije zimalizia kwa raia na vikesi vyao huko Mahakamani, pamoja na changamoto zenu huko ndani tunawaomba endeleeni kusimamia haki za watu bila hila!!
 
Kuna malalamiko yamekuwa yakisambaa kitambo sasa, binafsi kuna siku nilitoka mahakamani nikawa kwenye lunch na mawakili kadhaa, miongoni mwao walikuwepo wa DPP. Nikachomeka, ati mbona kila mkeka wa majaji hatuoni mawakili wa DPP,(niliongea kwa kebehi tu nione mawakili wa serikali tulikua nao pale watasemaje) jamaa waliongea kwa uchungu sana, wanaamini Samia amewablacklist. Tuliwacheka kwelikweli. Nakumbuka kuna mwaka Tundu Lisu aliwahi kuambiwa na magufuli kuwa hatateuliwa ujaji, TL lisema, hata akiteuliwa hatakubali kwasababu ni kazi ya utumwa, ila hawa jamaa wana uchungu kabisa na wanaamini wamekuwa blacklisted.

binafsi, siwaonei huruma, kama ni kweli, wacha tu wasote pengine kuna siku akili zao zitafunguka, wakajua uthamani wao na namna Mungu anavyotaka wafanye kazi. naongea hivi kwasababu zifuatazo:

1. Hii ni ofisi ambayo ccm wameitumia miaka mingi sana kama silaha ya kushindia uchaguzi. kamata kamata na shitakishitaki hawa jamaa wanatumiwa sana kinyume na haki.

2. Tulimwambia yule wakili kwamba, akubali tu kwamba mawakili wa DPP siku zote hutumiwa kama instrument kwa ajili ya wengine kupanda, ila wao wanaachwa palepale hadi uchaguzi mwingine. hivi, mtakuwa ngazi za wengine kufanikiwa hadi lini? na wakifanikiwa hawawakumbuki. .

3. Jifunzeni, SAMIA tangu aingie, ameteua majaji wangapo toka ofisi ya DPP? zero. wala hakuna ukurugenzi, urasi au uchochote, ila tukikutana mahakamani mnavyotukamia utafikiri mnapata chochote. juzi tumetoka mahakamani tunapata lunch sehemu na mmoja wenu, hadi anazuga tumlipie bill, mara zote analalamika ati Samia amewadis hawateui ujaji, awateue ujaji halafu nani awe anatumiwa kama fimbo kuchapia wengine, ninyi si ndio mmeamua kuwa hivyo? mnataka ujaji wa nini wakati matumizi yenu ninyi ni kipigio cha wengine? heshima yenu ndio hiyo.

4. Mwakani ni uchaguzi, fungukeni akili, ifuateni haki, mwogopeni Mungu, msitumiwe, narudia tena msitumiweeee. mjue kuwa, ccm wakiwatumia kama bablish kunyanyasa wapinzani, wakishashinda, watawaweka kwenye dustbin hadi uchaguzi wa 2030 ndio mtakumbukwa tena. mishahara yenu itabaki vilevile, na mtaendelea kudharaulika hivyo hivyo. mnataka hadi malaika ashuke toka mbinguni aje awaambie kuwa ninyi huwa mnatumika tu na hawaoni kama mna faida yeyote zaidi ya hiyo?

Ni hayo tu.
Biswalo Maganga
 
  • Nzuri
Reactions: UCD
Back
Top Bottom