Hivi ni kweli ofisi ya DPP wamekuwa blacklisted uteuzi wa Ujaji?

Kama wanasheria hawawezi kulinda haki zao, wataweza kutetea vipi haki za wengine? Kwa jinsi jaji mkuu wa sasa alivyokuwa anajinyenyekeza kwa dhalimu magu, hapo ndio nilijua mahakama ni utopolo mtupu. Si bure Hadi muhalifu Makonda anasema huwezi kupata haki mahakamani.
 
Wakili na jaji tofauti ndogo Sana

Wote wanatakiwa kuwa na uwezo mkubwa Sana kujenga hoja kwenye case

Sasa kama huyo WA DPP uwezo wake mdogo kuliko mawakili wengine wa mitaani au sekta binafsi au taasisi za umma huyo WA DPP ateuliwe kuwa jaji Kwa lipi?

Hao wa DPP hawajali kuwa unapokuwa na kesi kakamaa present seriously na uwe fit unalegea legea kama Mlenda na kuendekeza Rushwa halafu unategemea uwe jaji utasubiri Sana Tu

Nafasi za ujaji ukiona MTU kapewa hata kama hajawahi kanyaga mahakamani aweza kuwa aliombwa legal opinion kwenye very serious case akaitoa na serikali ikashinda baada ya kusikiliza legal opinion Yake kwenye kesi husika wakati hao wa ndani WA DPP walishindwa.kutoa huo ushauri

Kuwa ofisi ya DPP au mahakamani sio Tiketi ya kuwa jaji Ujaji Una hadhi na vigezo sio Tu muda umekalia benchi la uhakimu au kiti ofisi ya DPP

Ujaji haugawiwi kama kondomu za bure
 
Samatta si alikuwa High court Zimbabwe??
Bregedia si Mahakama ya Jeshi na Tume ya Vyama Vingi . Ni Prof Tu ndio hajakulia kwenye mahakama
 
Hivi yule ex- DPP Biswalo mganga si aliteuliwa kuwa jaji.

Huwa kuna vitu nikivifikiria naona ili nchi ipige hatua ni LAZIMA ipate katibs mpya.

Mtu kama Biswalo panapomfaa kwa sasa ni gerezani tu.
 
Samatta si alikuwa High court Zimbabwe??
Bregedia si Mahakama ya Jeshi na Tume ya Vyama Vingi . Ni Prof Tu ndio hajakulia kwenye mahakama
Samatta alikuwa DPP kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji. Ila aliteuliwa kuwa Jaji akiwa mdogo sana hivyo akakaa sana kwenye mhimili wa Mahakama.

Jaji Ramadhani aliteuliwa kutoka Jeshini. Ila at least hawa walijali sana mhimili wa Mahakama hasa kulinda misingi yake na kujali watumishi wakiwa Majaji Wakuu
 
nadhani kwa kawaida, huwa wana balance, wanatoa mahakimu wengi kuwa majaji, wanafuatia prictising lawyers kama mawakili wa kujitegemea, then kuna wengine mawakili toka ofisi ya DPP, Solicitor general na AG kwa ujumla, then wanaanza kuchukua mawakili ambao ni waalimu wa vyuo toka vyuo mbalimbali.

of all those above, waalimu wa vyuo ndio wanatusumbua sana mahakamani, wanakuwa wabovu kuliko chochote kwasababu majority wanajua tu theory, ile wanayofundishia wanafunzi, practice kwao ni kitu kigumu sana. ila ni haki yao, wawe wanawapa ili kubalance. kwa trend iliyopo, mama ameteua zaidi toka chama chetu cha TLS na mahakamani, na wengine toka mashirika ya kiserikali. ila warning, mashirika ya kiserikali huko ni wabovu hawajawahi hata kwenda mahakamani, wanatusumbua mahakamani hawaelewi.
 
Hao jamaa makauzu kweli,ila wanaongeka vizuri sana.
 
Justice resides not only in the courts but also in us, for justice begins with each of us striving to do the right thing.
 
Justice resides not only in the courts but also in us, for justice begins with each of us striving to do the right thing.
of course, haki ni ya Mungu, na kwa Mungu wetu haki yakaa ndani yake. akiwa mbinguni huangalia haki ipo wapi, na wapi haki inavunjwa ili ashuke kutetea anayeonewa. na mwanadamu yeyote anayemwogopa Mungu, lazima awe mtu wa kufuata haki bila kupindisha.
 
Tuache majungu,simjui huyo mahtmaa ila naamin ana qualification, kama ana connection why not, mana nowdays bila connection chukulia mfano utumish kule wanatumia miez mpaka 8 kukujib barua
 
Mengine hatukuyajua, kumbe ndivyo inavyokuwa? Sababu ni nini hasa?

Ndiyo maana siku hizi DPP hana kesi, DPP kamfutia kesi na mengine kama haya yanasikika.

Ni kwa kuwa watendaji hamna ukute na waliobaki ni wale I dont care.
 
Biswalo Maganga
Huyu walimtoa kumpa kinga ya dhambi alizowatendea watu akiwa DPP. Kuna watu wanamtafuta Biswalo wakimkamata wanamla akiwa mbichi. Amewatendea watu unyama mkubwa ashukuru cheo cha ujaji kinampa kinga na ana ulinzi.
 
ila kuna wakati watendaji wa ofisi za umma huwa wanapigwa dislike hadi wanakoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…