Hivi ni kweli suala la Katiba Mpya ni suala la Rais kulikubali au kulikataa?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!
 
Vyama vya upinzani Tanzania shida yao wanataka majimbo na ruzuku basi ndio lengo lao kuu.

Juzi Mbowe baada ya kuitwa Ikulu kaaidiwa neema kedeke kuhusu maslahi yake leo kapiga gia angani.

Ukisema katiba mpya ipo mikononi mwa Rais maana yako ipo mikononi mwa CCM, kifupi Chadema wamepigishwa magoti na CCM baada ya kurushiwa fupa la nyama.
 
Vyama vya upinzani Tanzania shida yao wanataka majimbo na ruzuku basi ndio lengo lao kuu...

Inaonekana ww ni afisa wa ikulu? Mazungumzo na rais yalikuwaje na aliahidiwa nn?
 
Kuna nchi ambayo inaweza kufanya mchakato wa katiba mpya bila maamuzi ya serikali?.Maana katiba mpya ni mchakato wa serikali na serikali iko chini ya Rais sasa hebu niambie nikwajinsi gani rais atakua hatoi kibali cha serikali yake kufanya huo mchakato.Tofauti na rais ambaye ni kiongozi wa serikali kuamua kuendesha huo mchakato sisi wengine kama wananchi kazi yetu inaishia kuipush serikali kwa hoja ili ione umuhimu wakufanya huo mchakato nasio zaidi ya hapo.Kwahiyo rais ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kwenye hili.
 
Vyama vya upinzani Tanzania shida yao wanataka majimbo na ruzuku basi ndio lengo lao kuu...

Juzi Mbowe baada ya kuitwa Ikulu kaaidiwa neema kedeke kuhusu maslahi yake leo kapiga gia angani.

Ukisema katiba mpya ipo mikononi mwa Rais maana yako ipo mikononi mwa CCM, kifupi Chadema wamepigishwa magoti na CCM baada ya kurushiwa fupa la nyama.
Swala la katiba ya nchi ni zaidi ya vyama vya siasa.Kwahiyo kama ulishindwa kujibu swali la mtoa mada bora ungekaa kimya ukasoma comments za wengine.
 
Hao wanasiasa wenyewe wanaodai katiba mpya hawajielewi.

Eti Mbowe, mtu anayedai katiba mpya, anaenda kufanya mkutano na rais, halafu anawaambia watu kuna maneno ya siri wamezungumza.

Halafu watu wanamshangilia!
Unaweza kufanya mkutano watu wawili faragha?.Yale ni mazungumzo ndo maana yakawa ya faragha.na ni tofauti kabisa na mkutano.Kwahiyo kama unashindwa kutofautisha mazungumzo na mkutano bila shaka wewe ndiye ambaye hujielewi bora ata hao unaowananga inawezekana wakawa wanajielewa kuliko wewe.
 
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people????

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!
Kawaulize mazuzu wenzako
 
Vyama vya upinzani Tanzania shida yao wanataka majimbo na ruzuku basi ndio lengo lao kuu...

Juzi Mbowe baada ya kuitwa Ikulu kaaidiwa neema kedeke kuhusu maslahi yake leo kapiga gia angani.

Ukisema katiba mpya ipo mikononi mwa Rais maana yako ipo mikononi mwa CCM, kifupi Chadema wamepigishwa magoti na CCM baada ya kurushiwa fupa la nyama.
Ccm haitaki hayo majimbo na ruzuku?
 
Hujasikia Mbowe amesema ni siri atakuwa anatoa kidogo kidogo, na amesema katiba mpya sio muhimu kwa sasa.

Nawaonea huruma wale vijana na tisheti zao #katibampya watavalia wapi tisheti zao.
Tatizo lako akili zako tangu uliopo zikabidhi kwa Jiwe bado hujarudishiwa
 
Kuna nchi ambayo inaweza kufanya mchakato wa katiba mpya bila maamuzi ya serikali?.Maana katiba mpya ni mchakato wa serikali na serikali iko chini ya Rais sasa hebu niambie nikwajinsi gani rais atakua hatoi kibali cha serikali yake kufanya huo mchakato.Tofauti na rais ambaye ni kiongozi wa serikali kuamua kuendesha huo mchakato sisi wengine kama wananchi kazi yetu inaishia kuipush serikali kwa hoja ili ione umuhimu wakufanya huo mchakato nasio zaidi ya hapo.Kwahiyo rais ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kwenye hili.
Point
 
Wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi!

Rais yupo chini ya wananchi. Hayupo juu ya wananchi.

Na ndo maana wananchi wanaweza kumtoa Rais madarakani.

Unabisha?
 
Back
Top Bottom