The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!
Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.
Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?
Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?
Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?
Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?
Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!
Mkuu Nyani, hiyo ndiyo hali halisi ilivyo Tanzania whether ni katiba au mabavu.
Tumeona ni jinsi gani JPM alivyo ni jinsi gani alivyoitopisha katiba pale alipoingia madarakani na hakuna hata aliyetia neno. Maza kaingia kasema katiba baadaye ... kasema hivyo kwa sababu anayo hayo mamlaka ya kuaamua nini kifanyike na nini kisifanyike na kwa wakati gani.