Hivi ni kweli suala la Katiba Mpya ni suala la Rais kulikubali au kulikataa?

Hivi ni kweli suala la Katiba Mpya ni suala la Rais kulikubali au kulikataa?

Wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi!

Rais yupo chini ya wananchi. Hayupo juu ya wananchi.

Na ndo maana wananchi wanaweza kumtoa Rais madarakani.

Unabisha?
Nakubaliana na wewe kwa kutumia maandishi, lakini hao wananchi mpaka waje wapewe hiyo nguvu ya uamuzi wa mwisho, watakuwa wamechakazwa balaa. Swali kwako, uko tayari kuchakaa mpaka pale vikwazo vitakapo izidi serikali ndipo wananchi wapewe mamlaka yao?
 
Mnaongeleaje katiba mpya ya JMT bila ya kutatua kero za huo muungano kwanza? Wabara mnataka serikali 3, Wazanzibari wanataka sovereignity. Katiba mpya ya muungano wa kero siyo katiba. Ni kupotezeana muda tuu maana hiyo katiba mpya itapigiwa kelele na kubadilishwa badilishwa kila kukicha.
 
Ktk nchi hii Rais ndyo kila kitu,kumbuka ngosha mwenzio aliposema muhimili wake umejichimbia chini zaid
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!
 
Leo umeongea ngosha sio kutupia lawama upinzani wananchi ndio mafala
 
Wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi!

Rais yupo chini ya wananchi. Hayupo juu ya wananchi.

Na ndo maana wananchi wanaweza kumtoa Rais madarakani.

Unabisha?
Uko Sahihi. Huwa uamuzi wa Wananchi katika mazingira ya Nchi yetu inawezekana. I think the move must start somewhere. Mbowe akizungumzia Katiba mnamdhihaki. Bunge letu ndio hilo rubber stamp ya Serikali kwa Kila jambo Bila Political will ya Rais katika Mazingira ya Tanzania Katiba ni Ndoto
 
Read ....inawezekana??
 
Mfumo gani? Mfumo rasmi au mfumo wa kienyeji?

Uwezo wa Rais kuamua tuwe na katiba mpya unatoka wapi?
Muulize Mange Kimambi anawajua vizuri sanaa watanzania, hasa pale kunapohitajika mass mobilization ili kudai na Kupata haki zao... Aliachwa solemba na mabango yake [emoji23][emoji23][emoji23] Hata Leo walivyomzingua kuhusu kuvujisha Ile clip ya ndugu yetu anayepigana na uvuli wa mauti, kakumbushia kwamba nyie wabongo hataki hata kuwasikia kwenye mambo ya kudai haki...
 
Kwa katiba tuliyo nayo.

Rais wa Tanzania is very powerful.

Kwanza ni;

1. Mwenyekiti wa Chama Dola.

2. Amiri Jeshi Mkuu.

3. Kiongozi mkuu wa Serikali kuu.

4. Mkuu wa Nchi.
 
Vyama vya upinzani Tanzania shida yao wanataka majimbo na ruzuku basi ndio lengo lao kuu.

Juzi Mbowe baada ya kuitwa Ikulu kaaidiwa neema kedeke kuhusu maslahi yake leo kapiga gia angani.

Ukisema katiba mpya ipo mikononi mwa Rais maana yako ipo mikononi mwa CCM, kifupi Chadema wamepigishwa magoti na CCM baada ya kurushiwa fupa la nyama.
Tangu lini changes zikaletwa na vyama vya siasa mkuu? Yaani mfano umwambie mtu kama Kibajaji katiba mpya inayotaka sifa ya mbunge iwe walau form six, muipitishe atakubali? Umwambie mbunge yeyote katiba mpya inayoweka ukomo wa kugombea ubunge au mbunge kufukuzwa na waliomchagua, waipitishe kweli?? Real changes lazima ziletwe na wananchi wenyewe mkuuu...
 
Hao wanasiasa wenyewe wanaodai katiba mpya hawajielewi.

Eti Mbowe, mtu anayedai katiba mpya, anaenda kufanya mkutano na rais, halafu anawaambia watu kuna maneno ya siri wamezungumza.

Halafu watu wanamshangilia!
Narudia, katiba mpya itaketwa na wananchi wenyewe, tena kwa kuidai, wanasiasa wao ni kiungo tuu... Mbowe kakaa gerezani miezi nane, hakuna hata mtu mmoja aliyepinga hadharani, na pengine hata kesi mahakamani wamehangaika wenyewe na wanachama wake na familia yake. Hata kipindi anavunjiwa na kuharibiwa Mali zake Kuna aliyemsaidia???
 
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!
SIO sahihi Katiba ni Takwa la Wananchi Rais anapaswa Kuwasikiliza Wananchi Waliompigia Kura Wanataka Nini kama ilivyo kwenye Kampeni wanaanchi Wanapotaka Hospitali,Barabara vivyo hivyo na KATIBA
 
Kuna nchi ambayo inaweza kufanya mchakato wa katiba mpya bila maamuzi ya serikali?.Maana katiba mpya ni mchakato wa serikali na serikali iko chini ya Rais sasa hebu niambie nikwajinsi gani rais atakua hatoi kibali cha serikali yake kufanya huo mchakato.Tofauti na rais ambaye ni kiongozi wa serikali kuamua kuendesha huo mchakato sisi wengine kama wananchi kazi yetu inaishia kuipush serikali kwa hoja ili ione umuhimu wakufanya huo mchakato nasio zaidi ya hapo.Kwahiyo rais ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kwenye hili.
Kwani Katiba Mpya ni ya serikali au ya wananchi?
 
Katiba kwa kiasi kikubwa ni suala la kisiasa zaidi kuliko matakwa ya mtu binafsi.

Tumeona namna ccm waliibeba ajenda ya JK ya Katiba Mpya na hatimaye kuibwaga baada ya kuona rasimu ya Warioba haina maslahi kwao.

Chadema na wapinzani wengine wanapaswa kuifanya Katiba Mpya iwe ajenda yao ya uchaguzi ili wapate uhalali wa kisiasa.

Kinyume cha hapo, wataishia kupambana peke yao na ccm (dola). Mahala pekee wanapoweza ungwa mkono ni wakati wa uchaguzi pekee.

Busara wangeunga mkono mabadiliko ya sheria walau kuifanya Tume ya Uchaguzi iwe na kaunafuu. Waingie kwenye uchaguzi
 
Swala la katiba ya nchi ni zaidi ya vyama vya siasa.Kwahiyo kama ulishindwa kujibu swali la mtoa mada bora ungekaa kimya ukasoma comments za wengine.
Well said kiongozi... Yaani nchi ina watu milioni 60, sasa unataka kikundi cha watu wachache eti ndiyo waeapiganie katiba huku wao wako juu ya stuli kwenye bar/groceries wanakunywa...
 
Wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi!

Rais yupo chini ya wananchi. Hayupo juu ya wananchi.

Na ndo maana wananchi wanaweza kumtoa Rais madarakani.

Unabisha?
Wanaweza kumtoa madarakani kwa njia gani?
 
Back
Top Bottom