Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
MaCCM yakijaribu kujenga nchi huku yakiamini kuwa Rais ni Mungu mtu👇🤡🤡🤡
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!
Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.
Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?
Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?
Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?
Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?
Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!
Hao wananchi wenye uamuzi wa mwisho lini waliandamana au kupaza sauti zao popote pale kuitaka hiyo Katiba mpya?Wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi!
Rais yupo chini ya wananchi. Hayupo juu ya wananchi.
Na ndo maana wananchi wanaweza kumtoa Rais madarakani.
Unabisha?
Tumia vizuri akili zako. Umuhimu wa katiba siyo suala la Chadema tu ila ni suala la nchi nzima ya Tanzania na wananchi wake. Ni kwa faida ya nchi. Ombwe ya kukosa katiba nzuri liko dhahiri. Kusema eti tume ya uchaguzi huru idaiwe kwanza ni kutotaka kupanua mawazo yako na ubinafsi wa wanasiasa. Wao wanafikiria kushika madaraka tu.Katiba kwa kiasi kikubwa ni suala la kisiasa zaidi kuliko matakwa ya mtu binafsi.
Tumeona namna ccm waliibeba ajenda ya JK ya Katiba Mpya na hatimaye kuibwaga baada ya kuona rasimu ya Warioba haina maslahi kwao.
Chadema na wapinzani wengine wanapaswa kuifanya Katiba Mpya iwe ajenda yao ya uchaguzi ili wapate uhalali wa kisiasa.
Kinyume cha hapo, wataishia kupambana peke yao na ccm (dola). Mahala pekee wanapoweza ungwa mkono ni wakati wa uchaguzi pekee.
Busara wangeunga mkono mabadiliko ya sheria walau kuifanya Tume ya Uchaguzi iwe na kaunafuu. Waingie kwenye uchaguzi na mtaji wa wapenda mabadiliko na vijana waliopigika na msoto wa maisha chini ya ccm.
Hii vibe ya Katiba Mpya haitawafikisha kokote , waigeuze iwe ajenda yao ya uchaguzi.
Uwezo wa Rais kuamua tuwe na katiba mpya unatoka wapi?
Hata leo CDM wakishika madaraka kupitia Katiba hii hii, usitarajie kama wataibadilisha.Kifupi Tanzania haijawahi kuwa na Katiba ya Wananchi. Iliyopo ya mwaka 1977 ilitungwa na kakikundi kadogo ka watawala wakina Pious Msekwa na wenzie.
Watawala wanajua turufu iko kwao wakiamini mwamko wa kisiasa wa wananchi bado ni mdogo. Ukitoa kipindi cha uchaguzi, siasa za wabongo zimelala usingizi wa pono. Harakati mingi ziko ndani ya vyama kuliko wananchi wa kawaida
Ndio ni ukweli....yeye ndiye mwenye kauli.Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?
Katiba ya Sasa imempa mamlaka makubwa sana, mpaka kutuamulia tunachotaka.Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?
Huo ndio ukweli, Rais wa Tz ndiye mamlaka kuliko hata hiyo katiba, hayo ya kusema hayupo juu ya katiba ni maneno tu ya kujifariji......ila kiuhalisia hata hiyo katiba haimzui kufanya anachotaka.Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?
Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?
Ni suala la nchi ndio nakubaliana nawe asilimia zote.Tumia vizuri akili zako. Umuhimu wa katiba siyo suala la Chadema tu ila ni suala la nchi nzima ya Tanzania na wananchi wake. Ni kwa faida ya nchi. Ombwe ya kukosa katiba nzuri liko dhahiri. Kusema eti tume ya uchaguzi huru idaiwe kwanza ni kutotaka kupanua mawazo yako na ubinafsi wa wanasiasa. Wao wanafikiria kushika madaraka tu.
Wakishindwa tuwaondoe.Hata leo CDM wakishika madaraka kupitia Katiba hii hii, usitarajie kama wataibadilisha.
Hiyo Katiba Hakuna mwanasiasa mnufaika asiyeipenda.
Unaweza kushika madarakani ukajiimarisha.Wakishindwa tuwaondoe.
Hakuna jambo kubwa kwa wanasiasa kama nguvu ya wananchi. Leo hii ccm wakitolewa watashika adabu, na yeyote atakaechukua madaraka atakua na heshima kwa wananchi
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!
Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.
Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?
Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?
Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?
Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?
Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!
Nazungumzia nguvu ya wananchi kuweka viongozi wawatakao kidemokrasiaUnaweza kushika madarakani ukajiimarisha.
Marais wa Uganda walikuwa wanapinduliwa tu, Leo kwanini haiwezekani kumtoa Museven.
Leo Mbowe Ni kila kitu ndani ya CDM kwasababu amekaa muda mrefu, na amejiimarisha. Hata mwenyekiti atayerithi Ni atakayemtaka yeye.
Watanzania siyo watu wa kupigania wanasiasa au maslahi ambayo Ni siasa related.Nazungumzia nguvu ya wananchi kuweka viongozi wawatakao kidemokrasia
Kifungu gani cha katiba kinachompa mamlaka ya kuweza kutaka au kutotaka katiba mpya?Mkuu yeye ndio anapitisha,, so anaweza kuacha kupitisha, kuchelewesha na mengine kibao kukwamisha...
Ingekuwa inatumia ule mfumo kama wa CAG ingekuwa hana hayo mamlaka,, kwa vile ile report huwa kwake inapita ili ailete bungeni na asipoleta baada ya 7days, CAG mwenyewe anapeleka...
Ila kwa katiba akitaka yeye ndio inawezekana, Taka ya Rais ndio taka,, za wengine wote ni takataka
Ujamaa hegemonyWatanzania siyo watu wa kupigania wanasiasa au maslahi ambayo Ni siasa related.
Uliona juzi Machinga wanaandama kupinga kutolewa soko la Karume mpaka wakaanza KUCHOMA tairi barabarani.
Unadhani kwanini hawafanyi hivi kupigani Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi?
Wewe ulitakaje? Yaani aitwe na Rais halafu akatae wito?Hao wanasiasa wenyewe wanaodai katiba mpya hawajielewi.
Eti Mbowe, mtu anayedai katiba mpya, anaenda kufanya mkutano na rais, halafu anawaambia watu kuna maneno ya siri wamezungumza.
Halafu watu wanamshangilia!
Kwenye Katiba iliyopouwezo huo Rais anautoa wapi?