Hivi ni kweli suala la Katiba Mpya ni suala la Rais kulikubali au kulikataa?

Hivi ni kweli suala la Katiba Mpya ni suala la Rais kulikubali au kulikataa?

Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!

Unahoja ngoja nimalizie hii konyagi ntachangia moshi baridi sana leo
 
Wewe jifunze kiswahili kwanza ujue kwamba hata watu wawili wanaweza kufanya mkutano, halafu ndiyo uje kujadili mengine.

Watanzania wana haki ya kikatiba ya kujua nchi yao inaendeshwa vipi.

Hilo si jambo ninalosema mimi, katiba hii tuliyo nayo sasa ndiyo inasema hivyo.

Sasa huyo Mbowe anayedai katiba mpya wakati hii ya sasa hawezi kuitimiza anajielewa?

Halafu kiongozi kusema kuna maneno ya siri umezungumza ni ujinga.

Kwa sababu ukishasema kuna maneno ya siri, umevunja siri na kuwapa watu maswali kibao kuhusu siri hii ni juu ya nini, wengine wataamini the worst possible case.

Ndiyo maana sasa hivi kuna minong'ono Mbowe kawa compromised.
Acha kuniletea tafsiri ya kingereza kwenye kiswaili.Lakini pia wewe ni nani hadi utake kuambiwa kila kitu.Muhusika kasema mazingumzo mengine ni siri sasa wewe kinachokusumbua hapo ni nini?.
 
Wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi!

Rais yupo chini ya wananchi. Hayupo juu ya wananchi.

Na ndo maana wananchi wanaweza kumtoa Rais madarakani.

Unabisha?
Kwa katiba tuliyonayo Rais yuko juu ya katiba, hivyo anaweza kuamua kufanya cho chote na hakuna wa kumuhoji wala kumshtaki.

Wananchi wanachoweza ni kupiga kelele kudai katiba mpya. Kwa kufifisha kelele za wananchi Rais anapandikiza vibaraka wake katika vyombo vya maamuzi kama Bunge na Mahakama. Ndiyo sababu Magufuli alipandikiza vibaraka wake bungeni na kuteua majaji kanjanja kuongoza mahakama. Pia aliamua kununua wapinzani na kuwazawadia vyeo serikalini na hakuna mwana CCM hata mmoja aliyeinua pua yake kupinga. Magufuli alitumia polisi na mahakama kunyamazisha wote waliotaka kumpinga hivyo watu wote waliufyata kuogopa kupotezwa.

Kwa hiyo Rais akiwa na msimamo wa chuma kamwe katiba mpya haiwezi kupatikana kwa njia za amani na kidemokrasia.

Kinachosubiriwa sasa hivi ni watu kuchoshwa na watawala (Rais) ili wafanye maamuzi magumu ya kumuondosha madarakani kwa msaada wa jeshi!
 
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!

Ni yeye na wewe, hemu fanya mambo basi
 
Ni nini kinachomfanya Rais awe juu ya katiba? Katiba ndo imetamka hivyo?
 
Ni nini kinachomfanya Rais awe juu ya katiba? Katiba ndo imetamka hivyo?
Ndiyo ni katiba! Hakuna mahali ambapo katiba imetamka wazi wazi kuwa yupo juu ya katiba lakini kwa mamlaka aliyopewa kikatiba tafsiri yake ni kuwa yupo juu ya katiba!

Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kukiri kwa katiba tuliyonayo inaweza kumfanya Rais kuwa dikteta. Marais waliomtangulia Magufuli waliongoza kwa busara tu lakini Magufuli alitumia fursa zote alizopewa na katiba kutawala.

Kumbuka Nyerere ndiye aliyetengeneza katiba hii na alifanya hivyo kwa makusudi ili kupunguza upinzani ambao angeupata. Alipo hakikisha hakuna upinzani wa kutishia utawala wake akaamua kutawala kwa busara na kutumia logic. Hata hivyo kuna wengi waliumizwa na utawala wa Nyerere kwa vifungo vya muda mrefu.
 
Kuna watu humu utafikiri siyo Watanzania. Eti Mkutano unaweza fanya hata na Watu wawili..Pheeew. Hao akina Siro watakupa hiyo nafasi. Umeambiwa Mikutano ya Kisiasa ni marufuku mpaka wakati wa Uchaguzi. Utafanyiwa wapi?
 
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!

Ni kweli kabisa uamuzi wa kuwa na katiba mpya ni wa wananchi wote kupitia sanduku la kura. Kamwe hauwezi kuwa uamuzi wa rais au chama cho chote cha siasa. Uamuzi wa wananchi unaweza kufanyika kupitia ilani za vyama vya siasa kwenye uchaguzi mkuu.

Kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 chama cha CCM kwenye ilani yake hakikuwa na kipengele hicho cha katiba mpya. Hivyo baada ya kushinda uchaguzi mkuu huo, hakina uhalali wo wote wa kuchomekea hilo suala nyeti la katiba mpya. Hata chama cha chadema hakikulinadi suala la katiba mpya kwenye kampeni zake za uchaguzi mkuu wa 2020. Hata kama walilinadi, kwa sababu walishindwa katika uchaguzi mkuu huo si halali hata kidogo kulilazimisha wakati huu. Wanapaswa wasubiri uchaguzi mkuu wa 2025 waje kulinadi tena kwa nguvu zote ili wananchi waje watoe uamuzi.
 
Ujamaa hegemony

Ujamaa ulilemaza jamii ikawa tiifu kwa mamlaka.

Maamuzi mengi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi tuliyaacha mikononi mwa kakikundi (chama) kalikofikiri kwa niaba ya wengi. Mawazo shindani yalipigwa nyundo.

Mizizi ya mfumo huo bado tungalinayo, jamii mfu ya watu wasiohoji, ukondoo na unafiki kwa watawala (uchawa).

Hata hivyo nyakati zimebadilika, nguvu ya machinga na vijana waliokosa ajira inaongezeka. Wamekosa jukwaa/mtu wa kuwasemea .
Ukishashindwa kwenye Maisha utasingizia kila kitu.
 
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!

Leo ndiyo mnaona raisi yupo juu ya kila kitu?
Lile chizi LENU lilipokuwa likipora UHAI wa watu mlikuwa mnaona sawa tu?
Mbona hamkuhoji liliposema kuna mhimili uliokochimbia China zaidi ya mingine? Mbona hamkuliuliza lile chizi liliposema KATIBA SIYO KIPAUMBELE CHA UTAWALA WAKE?
Mnakosoa leo? Unafiki tu
Hatutaki raisi asiyefuata sheria hapa
Anayeuwa watu wanaomkosoa.
Anayenyima watu uhuru wa kujieleza
Anayepora uchaguzi na kuturudisha mfumo wa chama kimoja.
 
Kifungu gani cha katiba kinachompa mamlaka ya kuweza kutaka au kutotaka katiba mpya?

Sipo Deep sana BUT ninachofahamu kisheria ni kwamba mchakato ukikamilia President inatakiwa atie sahihi... ndio Katiba ianze kufanya kazi.

Asipofanya hvo tafsiri yake ndio amekataa/ hajataka,, na bila yeye kuidhinisha sidhani kama kuna Alternative kisheria.

Kama sipo sawa nirekebishwe
 
Wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi!

Rais yupo chini ya wananchi. Hayupo juu ya wananchi.

Na ndo maana wananchi wanaweza kumtoa Rais madarakani.

Unabisha?
Kamuulize Ndugai kama Rais Yuko cihini ya Wananchi. Wewe mpaka Leo umejificha vichochoroni, si Bora hata Mbowe na Lissu tumewahi kuwaona wanapigania Katiba?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Mchakato wowote wa kuandika ama kuboresha KATIBA ni LAZIMA uhusishe IKULU yaani Rais, ukifanya nje ya RAIS basi inageuka UHAINI.
 
Vyama vya upinzani Tanzania shida yao wanataka majimbo na ruzuku basi ndio lengo lao kuu.

Juzi Mbowe baada ya kuitwa Ikulu kaaidiwa neema kedeke kuhusu maslahi yake leo kapiga gia angani.

Ukisema katiba mpya ipo mikononi mwa Rais maana yako ipo mikononi mwa CCM, kifupi Chadema wamepigishwa magoti na CCM baada ya kurushiwa fupa la nyama.
Wewe mchango wako ni upi kwenye kudai Katiba mpya au naww ni wale wale wanaolala nakutegemea wengine wahangaike kutafuta Katiba mpya
 
Ndo inavyoonekana, maana alisema anajenga uchumi kwanza.....
 
Hujasikia Mbowe amesema ni siri atakuwa anatoa kidogo kidogo, na amesema katiba mpya sio muhimu kwa sasa.

Nawaonea huruma wale vijana na tisheti zao #katibampya watavalia wapi tisheti zao.
Hahaha kwa hayo ndio yanatosha kumfanya aonekane ni basi tena?
Wabongo bwana, wape kichwa cha habari watatunga story hata kama hawazijui
 
Kwenye video hii, Tundu Lissu anazungumzia suala la katiba mpya na kudai kwamba Rais [kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan] ndiye mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la!

Anzia dakika ya 6:00 - 6:16 hivi.

Hivi ni kweli kabisa Rais ndiye mwenye uwezo huo?

Tukiachana na mazoea ya kijinga, uoga, na upumbavu wetu kiujumla, uwezo huo Rais wetu anautoa wapi?

Rais wetu yupo juu ya kila kitu? Yupo juu ya katiba? Yupo juu ya wananchi?

Kwa nini yeye ndiye awe mwenye uwezo wa kuamua tupate katiba mpya au la and not we the people?

Hii nchi kila kitu mambo ni kinyumenyume tu!

Yes sasa kama rahisi hataki ela mtapata wapi?

Hao ambao wataandika na kuandaa wanalipwa nn?

Nani anaweka signature kuwa hii ndio katiba ianze kutumika?

So hapo kila kitu ni mama aamue
 
Hao wanasiasa wenyewe wanaodai katiba mpya hawajielewi.

Eti Mbowe, mtu anayedai katiba mpya, anaenda kufanya mkutano na rais, halafu anawaambia watu kuna maneno ya siri wamezungumza.

Halafu watu wanamshangilia!

Ww Leo ukiitwa na rais hautokwenda?
 
Back
Top Bottom